Utofauti wa mishahara katika Utumishi wa umma, kunavunja moyo na kusababisha watu kubeza kusoma sana

Its as simple as that wakati unajua wazi kuna ufinyu wa nafasi...be real hata kidogo! I don't believe you are this dumb.

Au unafikiri kwenda huko ni kama kwenda maliwatoni!?
Nafasi ni finyu? Kwani ni wapi ambapo nafasi ni nyingi? Soko la Ajira ni tight miaka yote.

Nafasi huwa zinatangazwa... apply then nenda huko katengeneze hela.

Hata mimi nilikuwa nafanya kazi kwenye sehemu yenye mshahara "mdogo". Nafasi ikatangazwa sehemu yenye mshahara "mkubwa". Nikaaply nikapata.

Siku nikiona mahali kuna mshahara "mkubwa" kuliko hapa nilipo nitaaply huko.
Nikipata I'll move there... ndio maisha yalivyo.

Wewe unakaa hapo unataka aliyejuu ashuke ili mlingane....c'moon man
 
TTCL na ATCL walikua wanaingiza hasara kila mwaka hadi mashirika yalitaka kufilisika mbona mishahara haikupunguzwa kama kweli mashirika yanajilipa yenyewe?
 
Unataka kusema dereva wa tanapa anaiingizia serikali pesa nyingi kuliko dereva wa halmashauri. Tanapa wanaingiza pesa nyingi kutokana na majukumu waliyopewa na serikali kama taasisi. Hizo mbuga wangepewa halmashauri wangeingiza hizo pesa pia
Safi Sana kwa kuelewa. Sasa anzisha mada ya mbuga kunyang'anywa Tanapa na kupewa halmashauri ili mishahara yenu ipande au siyo?
 
Mbona unachagua mifano isiyolingana. Dereva wa TRA na wa halmashauri ambao wote wanamuendesha ofisa wa kawaida kwa nini mishahara yao itofautiane kama wana uzoefu na elimu sawa?
Chagua mifano linganifu ili discussion iwe nzuri
 
Kuelewa kwako utofauti wa dereva wa judge na dereva wa halmashauri ni Jambo zuri Sana na linajibu hoja yenu ya utofauti wa mishahara.[emoji2936]
 
Mkuu mfano wako unafanana kabisa na wangu,
 
TTCL na ATCL walikua wanaingiza hasara kila mwaka hadi mashirika yalitaka kufilisika mbona mishahara haikupunguzwa kama kweli mashirika yanajilipa yenyewe?
My point is damn clear.

Kama hapo ulipo wanalipa mishahara midogo, HAMA HAPO.

Nenda kwenye shirika lenye mishahara mikubwa. Hayo mashirika yapo na huwa yanatangaza nafasi za kazi.
Aply hapo, Ukipata make money there.

Ila acha uchawi wa kutamani wenzako washuke ili mlingane.
 
Mbona unachagua mifano isiyolingana. Dereva wa TRA na wa halmashauri ambao wote wanamuendesha ofisa wa kawaida kwa nini mishahara yao itofautiane kama wana uzoefu na elimu sawa?
Chagua mifano linganifu ili discussion iwe nzuri
Kwa nini huutaki mfano wangu? Unaona unakubana kwenye kona?

Point ya mwanzisha uzi ni LEVEL YA ELIMU.
Kwamba kama level ya elimu ni sawa, basi mishahara ilingane regardless ya taasisi inayoajiri.

Sasa ndio ninakuuliza. Dereva wa tanesko mwenye level ya elimu sawa na Dereva wa Rais, Je walipwe sawa?

Wote walipwe lets say laki 4 kwa sababu ya elimu zao kuwa sawa.

Hilo ndilo swali unalopaswa kulijibu.
 
HR wa Halmashauri wenye Bachelor Degree za Mzumbe na HR wa Tanroads, Tasac, TPA, TCAa, tena waliohitimu intake moja wanatofautiana Sana Mishahara. Kwa Mimi na Wanatumikia Serikali moja?
 
Askari jeshi anaesimama nyuma ya rais na cheo cha luteni kanali ana mshahara sawa na mwenzake mwenye cheo hicho aliyepo kikosini Makutupora tofauti itakuwa kwenye posho tu. Hata kwa dereva inawezekana
 
Mtoa mada una wivu wa ovyo sana. Huko kwenye hizo kazi za mishahara midogo si uliomba mwenyewe. Mie nimefanya kazi za Halmashauri, nikatoka nikaenda benki, nikatoka nikaenda Taasisi za mishahara mikubwa, nikatoka nikaenda nje na nikarudi nikafanya chuo kikuu kimoja nchini na sasa nimerudi Serikali kuu na mshahara wangu uleule na nilipo hapa Sasa nina mshahara mkubwa kuliko wote na sio CEO

Ushauri huwezi kupanda bila kuzunguka zunguka sehemu tofauti na hata kama mna elimu sawa hamuwezi kulipwa sawa maana mashirika yanatofautiana.

Hata kwenye biashara hamuwezi kuwa sawa hata mkiwa na elimu sawa na mtaji sawa baada ya muda mtazidiana tu kutokana na huduma zako na juhudi zako.
 
Ndomana nimegoma kwenda kusomea masters,walinipa Hadi scholarship ya nje ya nchi,nikawaambia hali yangu hairuhusu kwenda, degree hii moja inanitosha Sana[emoji135][emoji1363]tena.
Hauna maana kabisa. Elimu (haswa ya nje) ina maana kubwa sana katika maisha kwa ujumla haswa nje ya kazi.

Nje kama ni mjanja kunafungua sana akili. Sijajutia kwenda nje ktk maisha yangu nadhani ndio kumenifanya niwe zaidi ya wengi hapa nchini
 
Askari jeshi anaesimama nyuma ya rais na cheo cha luteni kanali ana mshahara sawa na mwenzake mwenye cheo hicho aliyepo kikosini Makutupora tofauti itakuwa kwenye posho tu. Hata kwa dereva inawezekana
Jibu swali nililouliza mkuu. Mbona unazunguka?

JIBU NIKICHOULIZA
 
Issue hapa ni utofauti wa mishahara, doesnt matter how many degree whom you studied.
Utofauti mkubwa sana wa mishahara ni sehem ya ubaguzi.
Leo hii daktari anaangaika kuokoa roho za watu pale hospitari, cha ajabu malipo yake yanazidiwa kwa kikubwa sana na mbunge wa viti maalum ambaye alikuwa anafanya kazi ya kukati kiuno tu jukwaani wakati wa kampeni then wameona ni bora wampe fadhira.
Mishahara itofautiane hata kwa laki mbili, tatu, nne hivi siyo mbaya.
Cha ajabu utakuta kuna mtu analipwa laki sita na mwingine analipwa milioni kumi na kitu huk........si upuuzi huu.!
 
Ieleweke kwamba sio kulinganisha mishahara ilingane lengo ni kuharmonize. Yaan kusiwe na gaps kubwa. Imagine lab technician wa TFDA anamzidi lab techician aliepo hospital za halmashauri au lab technician aliepo vyuoni au shule za sekondari kwa gap kubwa kama mbingu na ardhi. Muhasibu aliopo treasury au bot mwenye CPA anampiga gap kubwa muhasibu aliopo kwenye mamalaka za serikalinza mitaa au wizarani.
Ndo maana kusema harmonization kulinganisha mishahara.
Swali ni kwa nn magap yawe makubwa ivo.
Viwango vya elimu sawa na pengine majukumu ya kazi day to day, week to week na month to month almost hayatofautian afu deference ya salary inapishana hadi 3M plus.

Usilopenda kufanyiwa usiwafanyiwe wenzako.
Je ingekuwaje kama watumishi wa mamlaka za serikali za mitaa au serikali kuu wangekuwa wanalipwa incentives kama ivo je walioko mashirika ya umma si wangelalama.

Tujifunze historia vizuri na jinsi watu walipo anguka na kuingia machafuko. Sisi tusifanye kama wao.
Harmonization of salary is inevitable...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…