Utofauti wa mishahara katika Utumishi wa umma, kunavunja moyo na kusababisha watu kubeza kusoma sana

Utofauti wa mishahara katika Utumishi wa umma, kunavunja moyo na kusababisha watu kubeza kusoma sana

Wakati watu wanahimizwa kusoma tangu utotoni na kujiendeleza hata wakiwa makazini, ila ukweli ni kwamba, kusoma sana na kupata ma-degree mengi, sometimes huwa hakuna maana sana na hii ni kutokana na ulipaji wa mishahara serikalini kutegemea mtu anafanya kazi katika taasisi au shirika gani la umma.

Unaweza kuwa na masters ila kama uko wizarani au katika Halmshauri, unawezakuta unazidiwa mshahara na mtu mwenye Bachelor au hata Diploma anaefanya kazi katika taasisi (mara nyingi hizi Authority) za serikali. Hapo bado marupurupu.

Kwa mfano, dereva mwenye form iv anaeanza kazi pale BOT au TRA, sijui kama anazidiwa mshahara na mtumishi anaenza kazi akiwa na Diploma au Bachelor katika Halmshauri zetu.

Haya mambo ya kila taasisi kuwa na scale zake za mishahara, sometimes kunaondoa kabisa maana nzima ya kukaa darasa moja na kusotea degree ile ile wakati mkija kuajiriwa mmoja anakuwa yuko mawingumi na mwingine ardhini.

Kuna umuhimu wa serikali kutazama upya jambo hili na kufanya harmonisation ya mishahara serikalini ili kuondoa hali hii.Mambo ya kusema kuna taasisi zinazalisha au zinaingiza fedha serikalini hakutoia uhalali wa huu upendeleo kwani elimu waliyonayo wangeipata wapi bila mwalimu au wakiuguwa bila daktari au nesi watakuwa na afya ya kukusanya hizo hela na kuzipeleka serikalini au kutoa gawio kwa serikali?

Kama huu utofauti ni lazima uwepo (haukwepeki!), basi uwe reasonable na sio kuwa na ma- gape makubwa na ya kukatisha tamaa kwani ukweli wote tunategemeana. Wewe unaelipwa mshahara wa mamilioni, bila Polisi usalama wa mali zako ungetoka wapi?

Siku tukipata mtawala ataeamua kuweka wazi/hadharani scale za mishahara kwa watumishi wa umma, nadhani siku hiyo mitandao ya kijamii itashindwa kuhimili mijadala itayoibuka baada ya hapo jna huyo Raisi atajizolea sifa nyingi iwapo atahakikisha kunawakuwa na harmonisation ya mishahara.

Kama mnasema kila mtu na bahati yake, basi hata wakati wa ukoloni wazungu na wahindi ilikuwa sahihi kulipwa mishahara minono kutokana na bahati yao ya kuwa na ngozi nyeupe.

sasa tukiwaita nyumba mtakasirika. kwenda kote shule miaka 20 unatafuta mshahara? damn
 
Shirika la Umma linazalisha kwa faida na kut

Unataka kusema nini.
Mishahara inapangwa kutokana na mnachozalisha.hii iliwekwa kwa makusudi ili watu wajitume
TTCL na ATCL zilikuwa zinapiga hasara kila mwaka na mashirika yalikuwa yanakaribia kufa mbona mishahara yao haikushuka kama kweli haya mashirika yanajilipa?
Kuna vitu mnakaririshwa lakini uhalisia sio hivyo.
 
Mtu anaona kabisa pale wanalipa vizuri kuliko hapa. Badala ya kuhamia wanakolipa vizuri anataka wamuongezee pesa nyingi akiwa pale pale na uzalishaji ule ule[emoji3][emoji3]

Aisee unatakiwa kuhama ndugu.

Kwamba dereva anayemuendesha raisi alipwe sawa na dereva anayemuendesha afisa wa halmashauri?[emoji3][emoji3]

Au dereva wa Tanapa alipwe sawa na dereva wa halmashauri [emoji2960]

Hebu kaa chini fikiria kidogo reasons behind, kwanini mshahara uko tofauti?
Dereva wa halmashauri na wa tanapa wana tafouti gani kuweza kulipwa mishahara tofauti? Na kama wote wanawaendesha maofisa tu
Dereva wa judge na wa afisa naweza elewa utofauti ila ni kwa sababu dereva wa jaji anatakiwa awe na sifa za ziada kama TISS

Kuhusu kuzalisha unadhani halmashauri zingeruhusiwa zingeshindwa kukusanya mapato na wajilipe? Si wanabuni kodi mpya hadi wananchi watoke damu

Suluhisho ni kuharmonize misharaha ila watu walipwe bonus kutokana na uzalishaji wa taasisi na faida wanayotengeneza
 
Ndiyo maana Kuna mishahara mikubwa kwa sababu nafasi ni chache, na ukipata nafasi hiyo unaiingizia serikali pesa nyingi sana( mfano Tanapa) tofauti na halmashauri ambako mnaweza kuwa wengi lakini pesa mnayoingiza ni kidogo Sana
Unataka kusema dereva wa tanapa anaiingizia serikali pesa nyingi kuliko dereva wa halmashauri. Tanapa wanaingiza pesa nyingi kutokana na majukumu waliyopewa na serikali kama taasisi. Hizo mbuga wangepewa halmashauri wangeingiza hizo pesa pia
 
Tumechelewa Sana Ndugu Zangu
Tumeliwa Sana Ndugu Zangu
Tumechezewa Sana Ndugu Zangu
 
Katika kuharmonize mishahara tuwe tayari na matokeo yatakayopatikana. Ni kama kustandardize marks kwenye mitihani.
Wapo ambao watapanda kidogo. Wapo ambao watashuka kidogo wapo ambao watabaki pale pale.
Kuharmonize mishahara haiepukiki zama hizi za jpm. Asiogope watumishi wenye mishahara mikubwa hata kidogo kwana hadi hivi sasa ameshafanya majaribio makubwa na yakafanikiwa kwenye maslahi ya watumishi woote wa serikali na wa sekta za umma. Alipue tuu hilo bomu. Sisi wa halmashauri tutaweza neemeka kidogo japo sio sana kwa sababu watumishinwa serikali kuu na serikali za mitaa tupo wengi sana kulinganisha na wale waliopo mashirika ya umma ambao ni wachache.
 
Ndomana nimegoma kwenda kusomea masters,walinipa Hadi scholarship ya nje ya nchi,nikawaambia hali yangu hairuhusu kwenda, degree hii moja inanitosha Sana🙅👊🏼tena.
Mnajiendeleza holela, TMA haifutwi. Nani kakutuma kusoma Masters au PhD? Ukitumwa unaenda kusoma ukirudi Una nafasi Mpya ya Kazi na Cheo. Hujatumwa hautambuliki.
 
Kuongeza Maarifa na kujidai kwenye Jamii. Wengine Masters na PhD zetu zitakuwa za Kuzikwa. Zitasomwa Siku ya Last Respect.
 
Wakati watu wanahimizwa kusoma tangu utotoni na kujiendeleza hata wakiwa makazini, ila ukweli ni kwamba, kusoma sana na kupata ma-degree mengi, sometimes huwa hakuna maana sana na hii ni kutokana na ulipaji wa mishahara serikalini kutegemea mtu anafanya kazi katika taasisi au shirika gani la umma.

Unaweza kuwa na masters ila kama uko wizarani au katika Halmshauri, unawezakuta unazidiwa mshahara na mtu mwenye Bachelor au hata Diploma anaefanya kazi katika taasisi (mara nyingi hizi Authority) za serikali. Hapo bado marupurupu.

Kwa mfano, dereva mwenye form iv anaeanza kazi pale BOT au TRA, sijui kama anazidiwa mshahara na mtumishi anaenza kazi akiwa na Diploma au Bachelor katika Halmshauri zetu.

Haya mambo ya kila taasisi kuwa na scale zake za mishahara, sometimes kunaondoa kabisa maana nzima ya kukaa darasa moja na kusotea degree ile ile wakati mkija kuajiriwa mmoja anakuwa yuko mawingumi na mwingine ardhini.

Kuna umuhimu wa serikali kutazama upya jambo hili na kufanya harmonisation ya mishahara serikalini ili kuondoa hali hii.Mambo ya kusema kuna taasisi zinazalisha au zinaingiza fedha serikalini hakutoia uhalali wa huu upendeleo kwani elimu waliyonayo wangeipata wapi bila mwalimu au wakiuguwa bila daktari au nesi watakuwa na afya ya kukusanya hizo hela na kuzipeleka serikalini au kutoa gawio kwa serikali?

Kama huu utofauti ni lazima uwepo (haukwepeki!), basi uwe reasonable na sio kuwa na ma- gape makubwa na ya kukatisha tamaa kwani ukweli wote tunategemeana. Wewe unaelipwa mshahara wa mamilioni, bila Polisi usalama wa mali zako ungetoka wapi?

Siku tukipata mtawala ataeamua kuweka wazi/hadharani scale za mishahara kwa watumishi wa umma, nadhani siku hiyo mitandao ya kijamii itashindwa kuhimili mijadala itayoibuka baada ya hapo jna huyo Raisi atajizolea sifa nyingi iwapo atahakikisha kunawakuwa na harmonisation ya mishahara.

Kama mnasema kila mtu na bahati yake, basi hata wakati wa ukoloni wazungu na wahindi ilikuwa sahihi kulipwa mishahara minono kutokana na bahati yao ya kuwa na ngozi nyeupe.
🔥🔥🔥👋👋👋👋💪💪🤛🤛🤛Salary Slip duuu hongera sana. Paragraph ya 5, 6,7 imemaliza kila kitu. Basi kama wao wanazalisha ndio kigezo cha kupata Mishahara Mikubwa tupeane Zamu. Mhasibu wa TRA au Tanroads aje
naye Halmashauri kutumika
 
Ninakuuliza swali na ninaomba unijibu hapa directly bila kuzunguka.

Dereva wa tanesko anayepeleka nguzo kwa wateja anatakiwa alipwe sawa na dereva wa mkuu wa nchi ikiwa wote wana elimu sawa?

Let's say dereva wa tanesko analipwa laki 5,unamaanisha na dereva wa rais

🔥🔥🔥👋👋👋👋💪💪🤛🤛🤛Salary Slip duuu hongera sana. Paragraph ya 5, 6,7 imemaliza kila kitu. Basi kama wao wanazalisha ndio kigezo cha kupata Mishahara Mikubwa tupeane Zamu. Mhasibu wa TRA au Tanroads sense naye Halmashauri kutumika.
TTCL na ATCL zilikuwa zinaingiza hasara kila mwaka. Mbona mishahara yao haijapunguzwa waliendelea kunyonya hazina?
 
Hata kukataa mwenzio kupandishwa mlingane au kutafuta average mlingane nayo ni roho mbaya
Nani kakataa mwenzake asipandishwe? Unaongea nini we jamaa!!
Acha kunilisha maneno.

Mimi nasema wenye mishahara midogo wapandishwe kwa kadiri inavyowezekana.

Na wenye mishahara wewe unayoiona mikubwa kama kuna uwezekano wa kupandishwa pia ipandishwe kama taasisi husika ina uwezo wa kuwalipa.

Lakini mtu yoyote asishushwe mshahara.

Ndio maana nasema tena, kama unaona mshahara hapo ulipo hautoshi... HAMA nenda kwenye taasisi nyingine yenye mshahara mkubwa. Ni simpo tu kama hivyo.
 
Umeambiwa dereva wa Tanesco sio mtu muhimu kwakuwa anapeleka nguzo site? Kwahiyo dereva wa Tanesco akipewa kumuendesha rais hataweza?
Huyo dereva wa rais ana kitu gani exclusive sana ambacho wenzake hawawezi kufanya?
Hizi ni branding tu.
Serikali ilinganishe mishahara alaf posho za huko kwenye taasisi zibaki kama zilivyo, kumbuka mishahara ina impact kwenye vikokotoo
Acha kuzunguka kwa maneno mengi. Hakuna aliyesema dereva wa tanesko sio mtu.
Jibu swali nililouliza.

Nauliza tena. Dereva wa tanesko anayepeleka nguzo site, anatakiwa alipwe mshahara sawa na dereva anayemuendesha Raisi?

Kama dereva wa tanesko analipwa laki 4, dereva anayemuendesha Raisi wa nchi naye anatakiwa alipwe laki 4??

Jibu linatakiwa liwe NDIO au HAPANA.
 
Nani kakataa mwenzake asipandishwe? Unaongea nini we jamaa!!
Acha kunilisha maneno.

Mimi nasema wenye mishahara midogo wapandishwe kwa kadiri inavyowezekana.

Na wenye mishahara wewe unayoiona mikubwa kama kuna uwezekano wa kupandishwa pia ipandishwe kama taasisi husika ina uwezo wa kuwalipa.

Lakini mtu yoyote asishushwe mshahara.

Ndio maana nasema tena, kama unaona mshahara hapo ulipo hautoshi... HAMA nenda kwenye taasisi nyingine yenye mshahara mkubwa. Ni simpo tu kama hivyo.
Napenda hiyo paragraph ya mwisho. Tatizo wengi wanalalamika ila hawaweki juhudi kusolve changamoto za mshahara mdogo
 
Mfano mzuri Mwalimu wa secondary mwenye masters analipwa 760,0000 ila akihamia Chuo chochote cha elimu ya juu mshahara wake unaanzia 2,500,000 ***** , hapo umesomanae vyuo vyote ila anakupiga gape la hatari
What is the problem with that "Kukupiga gape"?

Unataka awe chini kama wewe ili ufaidike na nini?
Kwanini na wewe usikaze ili uajiriwe kwenye hiyo taasisi yake ili na wewe ukunje 2.5M?

Hizi ndio mentality za umasikini + roho mbaya tunazosema
 
Umeambiwa dereva wa Tanesco sio mtu muhimu kwakuwa anapeleka nguzo site? Kwahiyo dereva wa Tanesco akipewa kumuendesha rais hataweza?
Huyo dereva wa rais ana kitu gani exclusive sana ambacho wenzake hawawezi kufanya?
Hizi ni branding tu.
Serikali ilinganishe mishahara alaf posho za huko kwenye taasisi zibaki kama zilivyo, kumbuka mishahara ina impact kwenye vikokotoo
Kwaio ww kwa ufikirivu wako unaona ni sawa au sahihi dereva wa tanesco an halmashauri awe na mshahara sawa na dereva wa raisi....hahaha this is so funny sijui kama kuna nchi dunian ina huu utaratibu Sina hakika
 
Mfano mzuri Mwalimu wa secondary mwenye masters analipwa 760,0000 ila akihamia Chuo chochote cha elimu ya juu mshahara wake unaanzia 2,500,000 ***** , hapo umesomanae vyuo vyote ila anakupiga gape la hatari
Labda ujaribu kutueleza kwamba kwa nini ww unaona ipo hivo wats the big deal kama Hawa wote ni walimu lakini wa secondary awe na mshahara mdgo kuliko yule wa chuo...na hii ipo almost ulimwenguni kote labda tujadili hapa nini chanzo au sababu za huu utofaut
 
Back
Top Bottom