Utofauti wa mwonekano na Bei za Behewa SGR Kenya vs Behewa SGR Tanzania

Utofauti wa mwonekano na Bei za Behewa SGR Kenya vs Behewa SGR Tanzania

Kwani yamenunuliwa mwaka Gani haya?
Story ziko nyingi hata kujua ipi ya kweli ni tatizo. Maza anaya kwake. Msigwa ana story yake, Kadogosa ana yake na Mbawala anayo story yake.... This is Tanzania. The Bongo land.
 
Hivi ni viungo gani vinakosekana kwenye fikra zetu hadi tushindwe kuweka treni zenye mabehewa kama haya kwenye reli yetu ya STG_TZ?....

 
ila picha si kweli. Treni ya Tanzania ni ya umeme. Hayo mabehewa ya chini mbona hayaoneshi ni ya umeme?
 
Kuna mambo yanaumiza lakini bado yanachekesha. Hii ndiyo TAMU-CHUNGU ya Tanzania.....
 
Jiulize hizo za kenya zinatumia umeme? Pia jiulize SGR ya kenya imeishia wapi? Hao wakenya wenyewe wanatushangaa tunavofanywa mazuzu na Kigwa mrupukaji
Kichwa ndio kinacho endeshwa na umeme lkn sio mabehewa.
 
Mkuu tuandaeni mikakati mapema lakini siyo hivi vyama viongozi wao wakiitwa pale fasta wanaenda kuyajenga.
Upinzani Tanzania wamedhibitiws hawapumui.

Mikajati inahitajika kupata balance ya wagombea huko upinzani
 
View attachment 2438117
✓ JUU: ni mwonekano wa behewa za SGR Kenya...

=== BEI YAKE:

Ni KES 52.2m
kwa behewa moja sawa na TZS 980M

✓ CHINI
: Mwonekano wa behewa za SGR ya Tanzania yaliyonunuliwa juzi kati hapa..

===BEI YAKE:

Ni TZS 2.5bn kwa behewa moja

NB: Kwa vijana wa UVCCM yeyote anayesema haya eti wanaanza kupiga kelele kuwa ni "msaliti wa nchi" na eti siyo "mzalendo..."

Yaani wezi na mafisadi wa CCM eti wanataka kutufundisha sisi wengine somo la uzalendo wa nchi hii..!!

Na tunaposema hawa watu watakufa wakiwa wamekenua meno kwa uovu wao huu muwe mnaelewa...!!

Waone: UHURU JR TUJITEGEMEE
Huu ni uongo!, hiyo sio Treni ya SGR ya Kenya!. Treni za SGR za Kenya site zina bendera ya Kenya,
1670615936315.jpeg

Mabehewa ya SGR yetu ni mapya!.
P
 
Wewe liongo sana.
1. Sgr ya kenya haitumii umeme, ni ya diesel. Hiyo picha ni ya treni ya umeme.
2. Hayo mabehewa unayodai ni ya sgr tz yako kwenye reli tayari, hivi mabehewa yaliyofika juzi yameshawekwa kwenye reli?
Ukitaka kuwa muongo next time jaribu kufikiri kwa undani kidogo!
 
Huu ni uongo!, hiyo sio Treni ya SGR ya Kenya!. Treni za SGR za Kenya site zina bendera ya Kenya, View attachment 2441241
Mabehewa ya SGR yetu ni mapya!.
P
Hii picha na ile ktk mada kuu tofauti yake ni nini eti..?

Bila shaka ni bendera tu, au siyo...?

Vipi kuhusu tofauti ya muonekano na bei zake?

Wewe Pascal Mayalla na mwenzako UmkhontoweSizwe mna lolote la kusema...?
Wewe liongo sana.
1. Sgr ya kenya haitumii umeme, ni ya diesel. Hiyo picha ni ya treni ya umeme.
2. Hayo mabehewa unayodai ni ya sgr tz yako kwenye reli tayari, hivi mabehewa yaliyofika juzi yameshawekwa kwenye reli?
Ukitaka kuwa muongo next time jaribu kufikiri kwa undani kidogo!
Yaani nyie na wenzenu wachache wajinga huko mmeng'ang'ana kubweka tu kama mbwa kichaa kusema "aah! uongo!, uongo!, uongo!" eti kwa sababu ya bendera kiasi cha kushindwa kabisa kuelewa mantiki kuu ya hoja....

Na hivi mnadhani ni kwanini kuna kutofautiana kwa kauli za viongozi wa serikali moja iyo hiyo?.... Yaani;

PM ndugu Kassim Majaliwa

✓ Waziri wa ujenzi Mbarawa

✓ DG wa TRC Kadogosa na


✓ Rais Samia mwenyewe..

✓ Lakini Gerson Msigwa naye anasema lake..

IMG-20221210-WA0002.jpg

Kuhusu jambo moja lilelile yaani mabehewa haya...? Rais anasema mtumba, huyu anasema mapya, na yule anasema vile...

Lakini nyie hata kukuemea tu tabia hii ya uongo wa viongozi wetu hawa mnashindwa mkidhani waovu hawa wanaweza kujitibu na kujiokoa wenyewe...

Hakuna, haiwezekani unless wanaambiwa waziwazi tena kwa herufi kubwa kuwa, NYIE VIONGOZI MNACHOFANYA SIYO...!!

Labda niwaambie tu kuwa, kwa hatua hii, hakuna mtu awezaye kuutetea "ufalme huu ambao umekwisha kufitinika" wenyewe tayari. Na dalili ya kufitinika kwenyewe ni hii kujichanganya kwao baada ya wizi kutokea...!

Hakika atakuwa ni mwendawazimu pekee. May be you're among of them....
 
Nilisha andika sehemu uzi wangu wakautupa. Mradi ccm ipo madarakani inchi tusahau kusonga mbele kimaendeleo maana ni wizi wizi wizi
Kuna mzee huwa anatembea mitaa ya posta , siku akiamua tu huwa anapita akipiga kelele huwa anasema bora angefia Uingereza na malkia maana hapa Tanzania kinachoendelea ni wizi tu.
 
Back
Top Bottom