Gospel KTV
JF-Expert Member
- Aug 23, 2025
- 343
- 493
Wakati natafakari swala hili kwa kina hakika Mungu amenipa jibu lifuatalo. Utofauti wa rangi na nywele za wanadamu ulitokana na kuzaliana kwa wanadamu wa kwanza baada ya uumbaji.
Biblia inaonyesha kwamba wanadamu walitokana na familia ya kwanza ya Adam na Hawa na wakaendelea kuongezeka kwa kuzaliana:
Mwanzo 1:28, Mungu aliwaambia, “Zaeni, mkaongezeke…”
Mwanzo 5:4, Adamu alikuwa na “wana na binti.”
Matendo 17:26, Mungu “alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja.”
Kwa hiyo, wazo kwamba tofauti za kimaumbile zilienea na kuonekana katika vizazi vilivyofuata kupitia urithi na kuzaliana linaweza kueleweka vizuri.
Kisayansi pia, mtoto hupokea mchanganyiko wa vinasaba kutoka kwa wazazi wake; vinasaba hivyo vinaathiri kiasi cha melanini, aina ya nywele, rangi ya macho na sifa nyingine.
Swali la kujiuliza labda Adamu na Hawa walikuwa na uwezo gani wa kijenetiki uliowezesha vizazi vyao kutoa watu wenye ngozi na nywele tofauti sana? Hapo ndipo genetics inaweza kusaidia sana kuelezea hoja hii.