Utofauti ya watu wa Dar na watu wa mkoani ni huu

Ndio maana mimi nikipata nafasi ya kwenda kumtembelea ndugu Dar, wakikaa vibaya napiga mashine mke wa bro, piga mashine beki tatu wao na kama usiku lazima niwapake mafuta nyumba nzima
 
Wa kijijini wana ukarimu flani hivi amazing kwa kuwa wanajua umetoka town una vichenchi na pia kijijini maadili yapo high, ila hata na wao wakiishi mjini wanachange na kuwa kama hao wa mjini uliowasimulia
Ubinadamu kazi sana mazoea hujenga tabia tabia hufanya mambo mabaya tuone ni yakawaida
Chenchi mnatoa wapi.

Mkifika bush mnakosa hata nauli za kurudia Mjini.

Kitu mpo nacho ni stori za kitapeli tu.
 
Umeongea uhalisia mkuu... Ila niwaibie tu siri nyie watu wa mikoani, ukishaona ndugu yako wa Dar anakitoto kinaitwa Junior au Brian ukimtembelea tegemea mambo kama haya.
Ha ha ha sasa ka Jr si kanafuata malezi kaliyopewa?
 
Ungeanza na mfano Mxieeeeww..!! 😹😹

Mimi mdogo wangu usinione humu ninavyowajibu hovyo watu, nje huku nina heshima hata shem wako nikimpa maji kwanza nayaombea, kisha napiga goti mpk amalize kunywa ndo nainuka.!! 🏃‍♀️🏃‍♀️🏃‍♀️

Basi kuna mikenge itaguna na mingine itabisha 😹🤣🤣
Mimi nimeguna na nabisha
 
Umeenda semina Njombe, una ndugu yako kule. Unamtaarifu unakuja kumtembelea. Anakuambia karibu sana. Anakuelekeza panda daladala za Ramadhani shukia kwa Sanga. Unashuka stendi unamkuta ndugu yako na mkewe na watoto stendi wamekuja kukupokea! Mnatembea kitambo na kufika kwake. Watoto waliobaki home wanakuja ulipokaa, wanakushika kichwani kukusalimia. Wakubwa kidogo wanakuja wanapiga magoti "shikamoo baba mkubwa!".

Wanakuzunguka kuulizia habari za ndugu zao unawasimulia, huyu std 2, huyu std 7, kaka yenu form 2. Ndani kumechangamka kila mtu yuko engaged nawe in one way or another.
Mama anahangaika na msichana kukuandalia chakula. Baada ya muda mke wa mdogo wako anakuja kupiga magoti kukuambia karibu chakula. Unaenda mezani, anakuja kukunawisha mikono huku akisema "tusamehe shemeji mboga zenyewe hivyo hivyo.." Unakula unashiba.

Baadaye unaaga. Nyumba nzima wanafunga, wanakusindikiza hadi kituoni. Watoto wanakuaga, "ba mkubwa msalimie Jerry na Irene. Ukija tena uje nao" Unaondoka kwa heshima zote.

Siku ya siku nduguyo naye kapata kitrip cha Dar. Anakuambia nakuja kukutembelea. Unamwambia tumehamia kwetu Mbezi panda mwendokasi hadi mbezi mwisho. Anafika anakupigia, unasema kuna bodaboda hapo mpe niongee naye. Unaongea na boda "huyo jamaa mlete kwangu geti linatazamana na kituo cha afya cha Mbezi, lina waya za umeme juu".

Anafkishwa. Anagonga kengele, mko ndani familia, unaagiza housegirl, "si mnasikia kengele? Kafungueni geti" Housegirl anaenda kufungua. Ndugu yako anaingia sebleni anawakuta. Anawasalimu unaitikia marahaba, we mkubwa! Mkeo anaangalia tamthilia kakaa chini. Anageuka, karibu shemeji, za siku! "Nzuri". Amemaliza, anaendelea na tamthilia yake.

Wanao wanacheza game kwenye computer hata hawajashituka kuna mtu kaingia. Unawaambia, nyie msalimieni baba yenu mdogo. Wanatupia shikamoo bila hata kumuangalia usoni, game limekolea!

Mnazungumza kigogo, unamuuliza habari ya Dodoma. Kabla hajakujibu unashika simu unaanza kuchat, mke wako naye anachat! Sitting room imejaa watu, lakini kila mtu kama hayupo vile. Mara housegirl anawakaribisha chakula. Mama anapokea "shemeji karibuni chakula"

Unamgeukia mdogo wako unamwambia "aisee we jitegemee, hapa kima mtu anakula kwa wakati wake.!". Mgeni anainuka kwenda kupambana na meza peke yake. Maji ya kunawa hakuna! Bahati nzuri dada wa kazi anakatiza, anaulizwa maji yakunawa, anajibu kanawe pale kwenye "Hw basin" maji yanatoka!

Anaenda kunawa kinyonge. Anakula peke yake, anamliza na kurudi sitting room. Mnaongea issues kidogo za kifamilia na wazazi kijijini. Muda unafika wa ndugu kuaga. Unamwambia subiri kidogo. Unapiga kwa boda boda. Anakuja, unatoa elfu kumi unampa, unamwambia chukua hii utalipa hiyo bodaboda.

Boda inafika, ndugu yako anaaga, unasimama unamtoa hadi mlangoni. Wanafamilia wengine wanaagia sitting room bila kuinuka. Mama bado yupo busy na simu anachat. Watoto game limekolea, hawataki kutoa macho kwenye computer. Ndugu yako anawaaga hata hawamuangalii usoni. Wanatupia kwa mbaali "kwa heri ba mdogo" wanaendelea na game. Ndugu anakamata mchuma na kuondoka.
____
Wengi tunaoishi mijini tuna maisha ya aina hii, na tunaona ni sawa. Tunajifanya tupo busy kwenye mambo yasiyo na msingi na kupuuza utu wa wengine. Hata watoto wetu tunawalea ktk mazingira ya kuthamini zaidi vitu kuliko utu. Hii si sawa hata kidogo. Tuwatendee wengine kama tunavyotaka kutendewa.

C&P
Watu wa Dar siyo watu😂😂😂😂🙌🏿
Heri huyo hata amepokea simu ya ndugu yake
Huwa wanazima kabisa.

Yaani ndugu wa Dar
Ule upendo wa zamani haupo tena.
Wachache sana bado tunao huo upendo na aina hiyo ya mapokezi.

Tulioishi vijijini tumeexperience haya mapokezi ya mwanzo, mgeni akija wote mnakaa attention kumpokea. Baba anawaita wote
Anaanza kuwatambulisha mmoja baada ya mwingine.
 
Kuna Mjomba wetu alitembelea familia yenu miaka ya 70 kwenda 80 alikuja na familia yake kwa kutumia gari la kazi.. baada ya Baba kuona ugeni mkubwa km huo .. akachinja kambako la ng'ombe na kuita wananzengo kumsherehesha mgeni..ndani ya siku 3 ilikuwa ni kuogelea kwenye minofu iliyonona..na siku aliyoondoka mjomba akafungiwa furushi la nyama zilizokausha na kupewa ngozi ya yule ngombe aliyechinjwa kulingana na mila na desturi zetu... miaka ikapita mimi na kaka yangu tukamtembelea mjomba..tuliyokuta huko loading.............
 
Mimi nimeguna na nabisha
😹😹😹 Sema kweli??
Ila RRONDO umenichekesha wewe huwa unatafuta makosa yangu, kuna siku nilizingua mahali ukanishushua…!! 🤣
 
ukija tena njombe ramadhani nitafute naishi mitaa ya getini apa😌
 
Umeenda semina Njombe, una ndugu yako kule. Unamtaarifu unakuja kumtembelea. Anakuambia karibu sana. Anakuelekeza panda daladala za Ramadhani shukia kwa Sanga. Unashuka stendi unamkuta ndugu yako na mkewe na watoto stendi wamekuja kukupokea! Mnatembea kitambo na kufika kwake. Watoto waliobaki home wanakuja ulipokaa, wanakushika kichwani kukusalimia. Wakubwa kidogo wanakuja wanapiga magoti "shikamoo baba mkubwa!".

Wanakuzunguka kuulizia habari za ndugu zao unawasimulia, huyu std 2, huyu std 7, kaka yenu form 2. Ndani kumechangamka kila mtu yuko engaged nawe in one way or another.
Mama anahangaika na msichana kukuandalia chakula. Baada ya muda mke wa mdogo wako anakuja kupiga magoti kukuambia karibu chakula. Unaenda mezani, anakuja kukunawisha mikono huku akisema "tusamehe shemeji mboga zenyewe hivyo hivyo.." Unakula unashiba.

Baadaye unaaga. Nyumba nzima wanafunga, wanakusindikiza hadi kituoni. Watoto wanakuaga, "ba mkubwa msalimie Jerry na Irene. Ukija tena uje nao" Unaondoka kwa heshima zote.

Siku ya siku nduguyo naye kapata kitrip cha Dar. Anakuambia nakuja kukutembelea. Unamwambia tumehamia kwetu Mbezi panda mwendokasi hadi mbezi mwisho. Anafika anakupigia, unasema kuna bodaboda hapo mpe niongee naye. Unaongea na boda "huyo jamaa mlete kwangu geti linatazamana na kituo cha afya cha Mbezi, lina waya za umeme juu".

Anafkishwa. Anagonga kengele, mko ndani familia, unaagiza housegirl, "si mnasikia kengele? Kafungueni geti" Housegirl anaenda kufungua. Ndugu yako anaingia sebleni anawakuta. Anawasalimu unaitikia marahaba, we mkubwa! Mkeo anaangalia tamthilia kakaa chini. Anageuka, karibu shemeji, za siku! "Nzuri". Amemaliza, anaendelea na tamthilia yake.

Wanao wanacheza game kwenye computer hata hawajashituka kuna mtu kaingia. Unawaambia, nyie msalimieni baba yenu mdogo. Wanatupia shikamoo bila hata kumuangalia usoni, game limekolea!

Mnazungumza kigogo, unamuuliza habari ya Dodoma. Kabla hajakujibu unashika simu unaanza kuchat, mke wako naye anachat! Sitting room imejaa watu, lakini kila mtu kama hayupo vile. Mara housegirl anawakaribisha chakula. Mama anapokea "shemeji karibuni chakula"

Unamgeukia mdogo wako unamwambia "aisee we jitegemee, hapa kima mtu anakula kwa wakati wake.!". Mgeni anainuka kwenda kupambana na meza peke yake. Maji ya kunawa hakuna! Bahati nzuri dada wa kazi anakatiza, anaulizwa maji yakunawa, anajibu kanawe pale kwenye "Hw basin" maji yanatoka!

Anaenda kunawa kinyonge. Anakula peke yake, anamliza na kurudi sitting room. Mnaongea issues kidogo za kifamilia na wazazi kijijini. Muda unafika wa ndugu kuaga. Unamwambia subiri kidogo. Unapiga kwa boda boda. Anakuja, unatoa elfu kumi unampa, unamwambia chukua hii utalipa hiyo bodaboda.

Boda inafika, ndugu yako anaaga, unasimama unamtoa hadi mlangoni. Wanafamilia wengine wanaagia sitting room bila kuinuka. Mama bado yupo busy na simu anachat. Watoto game limekolea, hawataki kutoa macho kwenye computer. Ndugu yako anawaaga hata hawamuangalii usoni. Wanatupia kwa mbaali "kwa heri ba mdogo" wanaendelea na game. Ndugu anakamata mchuma na kuondoka.
____
Wengi tunaoishi mijini tuna maisha ya aina hii, na tunaona ni sawa. Tunajifanya tupo busy kwenye mambo yasiyo na msingi na kupuuza utu wa wengine. Hata watoto wetu tunawalea ktk mazingira ya kuthamini zaidi vitu kuliko utu. Hii si sawa hata kidogo. Tuwatendee wengine kama tunavyotaka kutendewa.

C&P
Hii yaan niliiona tangu nipo form 1 halafu ni kitambo saaaana, kuna ile nyingine inayohimiza vijana kabla hawajafika miaka 35/40 kuna vitu vya kua navyo na vitu vya kuachana navyo akadokeza uwe na walau kanzu 1 na balagashea 1 haijalishi wewe muislamu au mkristu pia uwe na suti walau moja ya dharula, emu tafuta tafuta ukiona tuwekee nijikumbushie
 
Binafsi nikienda popote nkahisi mapokezi sio au ujio wangu ni kero kwa niliowakuta huwa sikai zaidi ya dakika 15 naaga naondoka. Iwe ni nyumbani, ofisini, dukani, bar, mgahawa, kijiweni au popote tu. Huwa naona kuwa kero kwa mtu ni tabia mbaya.
 
Back
Top Bottom