Utoto bwana,acheni tu

Utoto bwana,acheni tu

Ahahahaha mzee mi nilikuaga msumbufu saana kwanza chakula cha usiku nikiwahi kulala afu wale chakula wasiniamshe nikiamka asubuh nataka kwanza cha jana afu ndo nimalizie na chai kisipo kuwepo ndalia siku nzima
 
Wakati nipo darasa la pili tulikua tukitoka shule na bro wangu tunakuta mother katuachia msosi kwenye sefuria ko tunainua loote. sasa siku moja mama aliacha wali na nyama mbili moja kubwa moja ndogo broo akaniwah akachukua kubwa nililia akabugia mdomoni fasta hapo hapo namimi nikashusha suruali nikakojolea kwenye msosi
 
walikuaga wanatuambia kuwa ukikojoa afu ukipaka pilipili kwenye mkojo dyudyu inaanza kuwasha mi nilikuaga napenda kuhakikisha kama ni kweli siku tupo na jamaa yangu tukaiba pilipili ndani tukazunguka nyuma ya nyumba tukakojoa chini tukaweka na pilipili baada ya dakika tano ivi tukaona ni uongo hamna kinacho tokea tukashauliana tupake pilipili kwenye vichwa vya dyudyu mzee kilicho fwata ni kilio mtaa mzima walikuja kutushangaa. wakaanza kutumwagia maji kwenye dyudyu mpaka zikapoa baada ya nusu saa iv tukatulia tukaanza kuchekana mzee kumbe mikoni bado pilipili bado ipo so nikapeleka mikono machoni kujifuta machozi moto ukawaka tena
 
Ghetto tulikua tunalala na mabro zangu wawili siku hiyo umeme ulikatika afu nilikua muoga saana kutoka usiku kwenda chooni siku hiyo kimba lilinibana mida ya saa sita nawaamsha mabro wanisindikize wanakausha wanajifanya awaskii kumbe wananichekea kwenye ma blanket. kimba lilipo nizidi nikavua nguo hapohapo nakushusha. mzee harufu iliyo kuwepo mle ndan hakuna aliye vumilia
 
Ukimi kufika kwenye matundu ya pua hiaya ni matango pori
Hadi sasa hivi nina uwezo wa kufikisha ulimi wangu kwenye matundu ya pua,kama unahisi ni matango Pori BET nikulie hela yako
 
Utoto bwana mda wa kula tulikua tunapakuliwa kwenye senia sababu ya uvivu wa kutokula nikila pekeyangu basi tukimaliza kusali naanza na nyama yangu nikimaliza nalilia za wenzangu wakininyima watagombezwa kwamba hawaoni me mdogo wanipe wakigoma bmkubwa atanipa hata yake ilimradi tu

Mda wa kuoga nachuka mda mrefu bafuni nikiskia miguu ya mtu anakuja namwagamwaga maji ovyo ilimradi ujue naoga ila nikitoka bafuni miguu tu ndoimeloana maji sehemu nyingine ya mwili kavu nilipewa mikwaju sikumoja na bmkubwa ikawa ndo mwisho wa hiyo tabia


Cc Kingsmann
hiii ya kuoga nadhani hata mimi nilikua nayo,nilikua sipend kuoga maji baridi mimi Ikafika wakati nikisema naoga ntaigia bafuni ntaoga ila mgongo utatoka mkavuuuuuu.

ikawa ndio kipimo changu kwamba nikitoka bafuni dada aambiwe anikague mgongoni na akinikuta mkavu anichape.
 
Na mimi nikuwe muwazi

wakati niko na umri mdogo nilikuwa naamini sex is like kuiba ( dhambi rejelea kwenye dini )

Maana yake hata wanandoa hawaruhusiwi kufanya 😂😂😂
Mimi nilikua nikiona watu wanafanya hivyo nasema (wanafanya dhambi),bhasi rafiki angu alikua ananiambia twende tukaangalie wafanya Dhambi (hapo anamaanisha twende tukacheki X)

kaka ake rafiki angu ndo alikua na mkanda wa X na alikua anauficha ila rafiki angu alikua anajua unafichwa wapi
 
Enzi hizo kuna rafiki angu mmoja tulikua majirani babake alikua ana gari landlover flani hizi zile za kizamani

Ilikua ikifika jumapili anatuchukua anatupeleka kanisani watoto wake pamoja na sisi,..barabara ya kuelekea kanisani ilikua na miti pembezoni sasa kilichokua kinanistaajabisha ilikua naona et miti inarudi nyuma ...

Nilikua nashangaa sana najiuliza hii kitu namna gani..gari likiwa taratibu unaona miti inarudi nyuma taratibu hapo tunaanza kuhesabu miti 1,2,3.....ila gari likichanganya tunachanganyikiwa miti inarudi nyuma haraka haraka tunashindwa kuhesabu tena
 
Mi nlikuwa naogopa mashine ya kukoboa na kusaga nafaka, yaan naweza ongozana na mama kwenda mashineni unakuta mashine imezimwa hadi wateja wawe wengi sasa ikiwashwa ule mlio na mtetemo wa ardhi kama hujanishika mkono vizuri utankuta mtaa wa pili, na treni nlikuwa naziogopa kwa zilivyokaa lile bichwa na mlio wake hasa ikiwa ndo inawashwa. Kuku mwenye vifaranga nakaa nae mbali maili 100.
 
Mi nlikuwa naogopa mashine ya kukoboa na kusaga nafaka, yaan naweza ongozana na mama kwenda mashineni unakuta mashine imezimwa hadi wateja wawe wengi sasa ikiwashwa ule mlio na mtetemo wa ardhi kama hujanishika mkono vizuri utankuta mtaa wa pili, na treni nlikuwa naziogopa kwa zilivyokaa lile bichwa na mlio wake hasa ikiwa ndo inawashwa. Kuku mwenye vifaranga nakaa nae mbali maili 100.
Hatujatofautiana 😂 😂 😂
 
hiii ya kuoga nadhani hata mimi nilikua nayo,nilikua sipend kuoga maji baridi mimi Ikafika wakati nikisema naoga ntaigia bafuni ntaoga ila mgongo utatoka mkavuuuuuu.

ikawa ndio kipimo changu kwamba nikitoka bafuni dada aambiwe anikague mgongoni na akinikuta mkavu anichape.

Hatari sana mkuu


Cc Kingsmann
 
Halafu kuna wabibi walikua wanakuja home wanaanza kuniita mmewangu..mmewangu

nilikuaga namind kinyama
ha ha ha ha ha upo kama mimi yaniiiiiii nilikua sipendiiiiiiii😂😂😂😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom