Utoto bwana,acheni tu

Utoto bwana,acheni tu

Ni wakati muafaka wa kujua upumbaf mlio nao ni wa kuzaliwa au mliuanza baada ya kuingia JF
 
Hahahahaha.....juzi dogo kaja kusemelea eti “dada” anamtesa sana.nilishtuka mno nikaanza na kufikiria Adhabu/hatua za kuchukua.Ila kwa upole nikamuhoji binti yangu dada anamtesaje.akanijibu eti kila siku anamlazimisha kulala tu mchana,ya kiiiiila siku akitoka shule,anaoga,kula,KULALA!eti “mi SIPENDI kulala jamani!
Yaani nilicheka mpaka basi

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Inabidi ujue hadi sasa hiv bado upo katika mambo ya kitoto kutuletea Uzi kama huu
 
Huu uzi umenifurahisha sana, Mimi nilikuwa najua mdogo wangu ndo atakuja kuwa mtoto wangu nikiwa mkubwa,

Wakaka kuniita 'mchumbaa' nilikuwa nalia mpaka nasusa kula, cha kusikitisha sasahivi hao wachumba hata siwaoni, Life is not fair..!!
Jamani wewe!
 
Kuna kale katabia ka kukojoa afu unatema mate ulipokojolea.. nakumbuka bro mtoto wa bamkubwa aliniambia usipotemea mate mchawi akipita mama yako anakatika maziwa! Mimi nilijua ni watu tu wa eneo letu kumbe karibia ni katabia ka wanaume wote wa Tz.. Mpaka leo najua haina maana yoyote kuteama mate ila bado nadumisha hii mira.. tena nisipotema nahisi sijajitendea haki
[emoji16][emoji16]haka katabia sijaacha had leo
 
Mimi nilikuwa nawaogopa sanaa wavuta bhangi.Ila nnavyozitembeza siku hizi[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
 
Mimi nilikuwa najua watoto hawazaliwi bali wananunuliwa hospitalin
 
Halafu nilikuwa najiuliza hivi nyerere akifa rais atakuwa nani asa nikiwaza hivyo nakosa kabisa amani,najua nchi sasa ndo kushney
 
Utoto raha sana,Nilikuwa na katabia kuna kamlio nakatoa mdomoni kama mdomo nauchezesha hivi siku nikapita na hako kamlio karibu na wamama..we! Walinikosakosa na vifuu,wengine mawe Sikujua sababu yake mpaka siku nilipolala na yule binti kwa mara ya kwanza.
 
Kuna kale katabia ka kukojoa afu unatema mate ulipokojolea.. nakumbuka bro mtoto wa bamkubwa aliniambia usipotemea mate mchawi akipita mama yako anakatika maziwa! Mimi nilijua ni watu tu wa eneo letu kumbe karibia ni katabia ka wanaume wote wa Tz.. Mpaka leo najua haina maana yoyote kuteama mate ila bado nadumisha hii mira.. tena nisipotema nahisi sijajitendea haki
Hii hata mimi nimeshindwa kabisa kuiacha.
 
Tukiwa wadogo tuliambiwa ukila huku umelala mama yako anakufa. Siku moja baba alikuwa anaumwa sasa sijui alipewa nini cha kutafuna akawa anakula huku amelala wacha niangue kilio namvuta aamke asile amelala mama atakufa[emoji23][emoji23][emoji23] eti nilijua mama yangu mimi na yeye ndio mama yake
Hahaha...ulikuwa boya sana
 
Nilijuaga watu wazima hasa wababa hawajisaidii haja kubwa

Pia nilijua wazazi huwa hawakosei kabisa, wako perfect.
 
Back
Top Bottom