Tatizo la watanganyika wengi wamekariri maisha na hawako well informed. Mbona watu wanaoweka fedha kwenye fixed account benki ambako riba yake ni ndogo sana watu hawapigi makelele kwamba hao wanaoweka hela kwenye hizo fixed account ni wajinga ni bora wangefanyia biashara?
Kama baadhi ya wadau humu walivyosema, hii mifuko ya UTT ni kwa ajili ya uwekezaji either wa muda mfupi au mrefu. Lengo ni kuhifadhi fedha zako kwenye hii mifuko kwa muda unaotaka huku hiyo fedha yako ikikupatia riba/faida kulingana na kiasi ulichowekeza kwenye mfuko.
Na mara nyingi wanaowekeza kwenye hii mifuko ni watu ambao wana fedha lakini kwa wakati huo hawataki kuzitumia hizo fedha kutoka na malengo yao waliyonayo kwa baadae. Lakini pia wengine wanaweka akiba zao kidogo kidogo kila siku, wiki, au mwezi kwa lengo la kuraise kiasi fulani cha fedha ili aweze kutimiza lengo lake la baadaye wakati huo huo hiyo akiba yake akipata faida/riba.
Hivyo lengo la kuweka fedha kwenye hiyo mifuko ya UTT au hata kwenye Fixed account za benki siyo biashara bali kuhifadhi fedha zao ambazo wna malengo nazo kwa baadae. Lakini pia biashara siyo rahisi kama tunavyoaaminshwa na motivational speakers wa humu JF ambao hajawai hata kuuza pakiti moja ya Peremende (Pipi).
NOTE: BUSINESS IS NOT FOR EVERYONE (SIYO KILA MTU ANAWEZA KUFANYA BIASHARA). HIVYO ACHENI KUKARIRI MAISHA.