UTT AMIS naona kwenye account yangu ya UTT hela imeongezeka kidogo

Wabongo tulio wengi hatuna elimu kubwa kwenye swala la uwekezaji, au hisa ndio huwa tunapigwa za kichwa
 
Thamani ya vipande haishukagi?
Na ukitaka kuchukua hela yako, unauza vipande vyako? Ama unaichukua tu?
Inaweza kufluctuate kulingana na aina ya mfuko unaowekeza na mabadiliko katika mfumo.

Mfano kwenye mfuko wa Umoja wanawekeza sehemu ya pesa katika hisa hivyo hisa zikishuka huwa thamani ya kipande inaweza kushuka pia.

Ila kuna mfuko wa Liquid fund ambao wenyewe huwekeza katika hatufungani za muda mfupi (short term bonds) ambazo huwa na interest rate ya karibu uhakika (kufeli ni iwapo tu serikali ifeli). Hivyo hizi kwa kawaida zinakuwa stable zaidi na ni ngumu vipande thamani kushuka.

Hivyo ni kuangalia tu wewe unapendelea zaidi kiasi gani cha risk na aina ya uwekezaji na kuchagua mfuko ambao utakufaa.

Ukitaka kurudisha pesa yako unauza vipande vyako. Unatembelea ofisi zao na kujaza fomu ya kuuza vipande. Malipo hutegemea na aina ya mfuko.

Kuna mfuko wa Umoja huwa ni siku 7 hadi 10 za kazi... Pia kuna mfuko wa Liquid wenyewe ni siku 3 za kazi pesa inakuwa imeingia katika akaunti yako ya benki. Kuna mifuko mingine pia ambayo sifahamu kwa undani muda wa kulipwa ila range ni hiyo.
 
Shukrani Kiongozi[emoji120].
 

Hawana akili hao. Hawawezi kukuelewa kwa sababu watz wengi wanaangia Leo na si kesho. Yan wanata utajiri wa hrk hrk ilhali wamejaa umaskini, uwezo wa kufikiria Mdogo. Hawana commitment na consistency. Inshort wako hovyo sana
 
Sasa huoni hata kama una vipande 50000 ambavyo thamani yake ni milioni 70,000 bado utapata nyongeza ya Tsh 50000 pekee kama gawio ndo hilo

10m sawa na vipande 88,384. Iweje 70m iwe vipande 50,000?[emoji23][emoji23][emoji23]. Km hamjui vitu Bora kuuliza kuliko kujifanya mnajua.
 
Duuh labda kama mtu huna mawazo kabisa ya biashara au ni mtu mvivu.

10mil upate elfu 87 kwa mwezi ni bora utafute center nzuri mjini ufungue mpesa na wakala wa crdb/nmb.

Mzazi kafungue ww mbona simple sana
 
Hawana akili hao. Hawawezi kukuelewa kwa sababu watz wengi wanaangia Leo na si kesho. Yan wanata utajiri wa hrk hrk ilhali wamejaa umaskini, uwezo wa kufikiria Mdogo. Hawana commitment na consistency. Inshort wako hovyo sana
Mtu anataka aweke pesa leo mwezi ujao aangalie salio limeingia akanunue crown atambe mtaani 😄
 
UTT AMIS ni Taasisi ya Serikali.
 
Mimi niliitamani Malikia Acc ya CRDB kutokana na maelezo yake ya kwenye kipeperushi..
Kwamba unaweza chukulia mkopo hizo pesa zako unazoweka mpk asilimia 90 yake.

Nikavutiwa… kuna best angu CRDB nikamuuliza in details,, akanambia temana nayo, maana wana rate ndogo sana kwa mwaka ya asilimia 5.

Ili hali UTT rate yao kwa Liquid fund ni asilimia 12 kwa mwaka..

Vichwa ngumu imagine nna laki yangu UTT kwa mwezi wanipe rate ya 1 pasee ‘ ni efu 1.. ni heri kuliko hiyo pesa ingekuwa CRDB/ NMB nije kukuta kuna efu 98,000.
 
Bado haijakaa sawa, ina maana gawio itakuwa 0.0087 ya fedha uliyowekeza; mfano ukawekeza milioni 10, utapata gawio la 87,719.
NB: Hakuna taasisi ambayo iko tayari kukufanyia kazi wewe kwa faida
Kea mtu anayejua kuitafuta pesa mjini,
huu Ujinga hawezi kuufanya.

Bora hata hiyo mil 10 kuzungusha float kwenye miamala ya mpesa usubiri kamisheni kuliko huu ujinga wa elfu 87 kwa mwezi
 
Came on man..huu ni undezi wa ajabu yani niweke 10m nipata 88k per month..umasikini huu tunautafuta wenyewe huku tukitajirisha wengine.

#MaendeleoHayanaChama
Mambo ya kiwaki Sana haya,
Hiyo mil 10 Ni Bora nijenge chumban&sebule master nipangishe kwa 120k kila mwezi uku pia hiyo nyumba nikichukulia mikopo kwenye mabenki kuliko huo upuuzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…