UTT Amis ni sahihi na sio utapeli ila mpaka umueleze mtu anayetegema Maguire ajiunge ndio apate hela ni vigumu sana akakuelewa. Ndio maana watu tukilalamika kina Kalynda kwanini hawafungiwi, sasa ona mifuko ya serikali inayofanya kazi tangu 2006 ikipata faida na haijawahi tapeli mtu inakuwa overshadowed na platforms za kitapeli zinazoibuka na kupotea kila miezi mitatu.
Chukulia mfano una hela milioni 20, hutaki kuiwekeza kwenye biashara maana una kazi zako ofisini zinakubana au ushawekeza unabakiza hela ya emergency mambo yasiponyooka, ukisema utunze hiyo hela haiongezeki thamani na labda inakuwa na makato. Hapo ndio unaiweka UTT Amis. Ninavyoielewa kwa machache iko hivi:
Ni low risk investment ambayo ina low return. Hufanyi kazi unatunziwa hela tu, vipande unavyonunua vinaongezeka thamani. Je wao wanafaidika vipi na kutunza hela zako?
Wao ni wataalamu wa uchumi na biashara wanafanya analysis na kukopesha au kuwekeza biashara zinazoleta faida. Badala ya wewe uingie DSE kununua hisa za CRDB, NMB, TBL, TOL, Jatu au nani unachanganyikiwa na huna uelewa basi unaweka hela UTT wao wanafanya portfolio kuwekeza sehemu za uhakika na tofauti. Wakiunganisha gawio au mrejesho wanaopata sehemu tofauti ndio wanakupatia kiasi chake ambacho kwa mwaka unaweza pata mara nyingi ni 11% ya hela uliyoweka.
Ukitaka kuwekeza lazima utumie muda kusoma au kuelekezwa. Hufyatuki tu kama Kalynda wanakupa link za YouTube ukiuliza kidogo wanakwambia "hujaona ITV wanatangaza, mbona mimi nimepokea hela, hujaona mabango yetu, si tuna ofisi na tumesajiliwa na BRELA".
Mimi binafsi siwezi weka hela UTT, ninao muda wa kuifanyia investment mwenyewe na hiyo hela kwanza sina. Ila sio dumb kusema ni matapeli, bongo hamna holding companies na hedge funds kama Berkshire Hathaway ya mzee Buffett, kilichomfanya awe ni billionaire ni hiki. Ila kama unataka hela ya haraka huku sio mahali pako. Na uzuri hawatumii nguvu kukuita, nadhani marketing yao haiko vizuri sana.