UTT AMIS naona kwenye account yangu ya UTT hela imeongezeka kidogo

UTT AMIS naona kwenye account yangu ya UTT hela imeongezeka kidogo

UTT Amis ni sahihi na sio utapeli ila mpaka umueleze mtu anayetegema Maguire ajiunge ndio apate hela ni vigumu sana akakuelewa. Ndio maana watu tukilalamika kina Kalynda kwanini hawafungiwi, sasa ona mifuko ya serikali inayofanya kazi tangu 2006 ikipata faida na haijawahi tapeli mtu inakuwa overshadowed na platforms za kitapeli zinazoibuka na kupotea kila miezi mitatu.

Chukulia mfano una hela milioni 20, hutaki kuiwekeza kwenye biashara maana una kazi zako ofisini zinakubana au ushawekeza unabakiza hela ya emergency mambo yasiponyooka, ukisema utunze hiyo hela haiongezeki thamani na labda inakuwa na makato. Hapo ndio unaiweka UTT Amis. Ninavyoielewa kwa machache iko hivi:

Ni low risk investment ambayo ina low return. Hufanyi kazi unatunziwa hela tu, vipande unavyonunua vinaongezeka thamani. Je wao wanafaidika vipi na kutunza hela zako?
Wao ni wataalamu wa uchumi na biashara wanafanya analysis na kukopesha au kuwekeza biashara zinazoleta faida. Badala ya wewe uingie DSE kununua hisa za CRDB, NMB, TBL, TOL, Jatu au nani unachanganyikiwa na huna uelewa basi unaweka hela UTT wao wanafanya portfolio kuwekeza sehemu za uhakika na tofauti. Wakiunganisha gawio au mrejesho wanaopata sehemu tofauti ndio wanakupatia kiasi chake ambacho kwa mwaka unaweza pata mara nyingi ni 11% ya hela uliyoweka.

Ukitaka kuwekeza lazima utumie muda kusoma au kuelekezwa. Hufyatuki tu kama Kalynda wanakupa link za YouTube ukiuliza kidogo wanakwambia "hujaona ITV wanatangaza, mbona mimi nimepokea hela, hujaona mabango yetu, si tuna ofisi na tumesajiliwa na BRELA".

Mimi binafsi siwezi weka hela UTT, ninao muda wa kuifanyia investment mwenyewe na hiyo hela kwanza sina. Ila sio dumb kusema ni matapeli, bongo hamna holding companies na hedge funds kama Berkshire Hathaway ya mzee Buffett, kilichomfanya awe ni billionaire ni hiki. Ila kama unataka hela ya haraka huku sio mahali pako. Na uzuri hawatumii nguvu kukuita, nadhani marketing yao haiko vizuri sana.

Factos
 
Kwa nini majina ya ajabu kama vipande. Watu bado wanalea majeraha ya Kalynda, tena anajitokeza mwingine na utapeli. Kwanza hilo jina vipande ni tosha kuanza kuwa na shaka. Ebu tuelrze wenye kampun ni nani na wako wapi, maana wasijekuwa nje ya nchi ambapo hatuwapata wakiisha tuibia. Ukiskia kuna kampuni inalipa riba tosha kwa mwezi juwa uk karibu kuliwa. Watatoa mgao kuhaKIkisha watu wanawaamini. Baadaye watapandisha dau au watu kuongeza dau kwa sababu walikuwa wakipata elfu kumi, ishirini, thelathini. Tukishaanza kuamini tunaamuwa faida ibaki hukohuko ili dau liwe kubwa. Wengine wataongeza mtaji. Kufumba na kufumbua mtaambiwa ofisi zimefungwa, wahusika hawaonekani. CHUNGA SANA.

Mkuu utt ipo toka 2008 fatalia tu
 
Mm nimewapigia na nimepata ELIMU kubwa mnooo.
Screenshot_20220923-231958_OneDrive.jpg
 
Kwa nini majina ya ajabu kama vipande. Watu bado wanalea majeraha ya Kalynda, tena anajitokeza mwingine na utapeli. Kwanza hilo jina vipande ni tosha kuanza kuwa na shaka. Ebu tuelrze wenye kampun ni nani na wako wapi, maana wasijekuwa nje ya nchi ambapo hatuwapata wakiisha tuibia. Ukiskia kuna kampuni inalipa riba tosha kwa mwezi juwa uk karibu kuliwa. Watatoa mgao kuhaKIkisha watu wanawaamini. Baadaye watapandisha dau au watu kuongeza dau kwa sababu walikuwa wakipata elfu kumi, ishirini, thelathini. Tukishaanza kuamini tunaamuwa faida ibaki hukohuko ili dau liwe kubwa. Wengine wataongeza mtaji. Kufumba na kufumbua mtaambiwa ofisi zimefungwa, wahusika hawaonekani. CHUNGA SANA.

Unajua UTT imeanza lini lakini?

Na wanafanyaje kazi?

Umeshawahi kuona wakijitangaza Kwa nguvu Kama hizo kampuni za kina kalynda?

Jisomee ujiridhishe ukiona ni utapeli unaachana nayo.
 
Wakati mama muuza vileja kwa mtaji wa buku 6 anaingiza buku 12 per day faida yake ni buku 6 hata wauza kashata vivyo hivyo.
Ni uzuzu kuweka huko UTT mwezi mzima afu wakulipe tsh 7

Watu wanakiwa wafahamu utt sio biashara ni uwekezaji mfano-: mtu kanunua kiwanja kina miaka 6 hata msingi hakina kipo tu,Kufungua account kwa ajili ya watoto wako au kuwanunulia viwanja , kununua hisa za mabank au kampun ,kujiwekea akiba kuna watu wanaweka pesa bank, vibubu au kicheza mchezo na mwisho wa siku anapokea pesa yake ilele bila ongezeko lolote au kijumbe kachukua chake na wengine wanaoweka kwenye vibubu wanapokea ile ile hakuna kilichoongezeka ndio maana watu wanashauriwa uweke utt kwa mambo kama haya kama una uweze wa kupata faida ya 30000 kwenye biashara yako weka weka hata 2000 kama akiba au unavyocheza mchezo ukiona imefika laki 2 unatoa unafanya mambo yako ila itakua na ongezeko hata kama ni 5000 tofauti na ungetunza ndan
 
Watu wanatakiwa wafahamu utt sio biashara ni uwekezaji mfano-: mtu kanunua kiwanja kina miaka 6 hata msingi hakina kipo tu,Kufungua account kwa ajili ya watoto wako au kuwanunulia viwanja , kununua hisa za mabank au kampun ,kujiwekea akiba kuna watu wanaweka pesa bank, vibubu au kicheza mchezo na mwisho wa siku anapokea pesa yake ilele bila ongezeko lolote au kijumbe kachukua chake na wengine wanaoweka kwenye vibubu wanapokea ile ile hakuna kilichoongezeka ndio maana watu wanashauriwa uweke utt kwa mambo kama haya kama una uweze wa kupata faida ya 30000 kwenye biashara yako weka weka hata 2000 kama akiba au unavyocheza mchezo ukiona imefika laki 2 unatoa unafanya mambo yako ila itakua na ongezeko hata kama ni 5000 tofauti na ungetunza ndan
 
Milioni 10 gawio ni 88,390/= kwa kila mwezi. Hii ni hela kubwa mno kwa fedha iliyowekwa pending ktk biashara yaani iliyokua haina kazi. Hili gawio kwa cc walala hoi tunalipa bills nyingi sana kwa mwezi[emoji2957][emoji2957][emoji2957]
Came on man..huu ni undezi wa ajabu yani niweke 10m nipata 88k per month..umasikini huu tunautafuta wenyewe huku tukitajirisha wengine.

#MaendeleoHayanaChama
 
Came on man..huu ni undezi wa ajabu yani niweke 10m nipata 88k per month..umasikini huu tunautafuta wenyewe huku tukitajirisha wengine.

#MaendeleoHayanaChama

Inatakiwa ujiulize maswali mengi mno kwamba kufikisha hicho kiwango cha pesa huyu mtu kaziokota au alikua anafanya biashara. Pia inatakiwa ujue lengo la mtu kununua hati fungani ni nini. Kabla hujakosoa tafafakari vitu vingi. Usitafakari kwa negative pekee pia tafafakari kwa positive. Ukifanya hivyo utapata majibu ambayo ni mazuri sana kwako
 
Came on man..huu ni undezi wa ajabu yani niweke 10m nipata 88k per month..umasikini huu tunautafuta wenyewe huku tukitajirisha wengine.

#MaendeleoHayanaChama
Upo sahihi sana kwa Mentality ya Ki-Biashara. Pesa inatakiwa izunguke na izalishe, Kibiashara ukiwekeza 10m halafu upate return ya 88k monthly ni Failure.

Ila kwa mentality ya ki-Uwekezaji unakuwa haupo sahihi, hizi huwa na faida kwa muda mrefu, Ni sawa na Mtu anayepanda Miti leo na kutegemea avune baada ya 15 years. (hizi ndio aina ya investment vijana hatuwezi na tunaishia hupigwa na GET MONEY QUICK SCHEME kama Kylinda,Qnet,MrKUKU nk).

Cha msingi ni kuangalia rate zao kama zinaenda sawa na kushuka kwa thamani ya Pesa. na uzuri wa Bonds, Eg za BOT ni unaweza kuzitumia kuchukulia Mkopo(badala ya kuweka Nyumba, ardhi),
Yaani mfano kama ulinunua bonds za 100m, ukawa unapata gawio la 10m kwa mwaka, Unaweza Chukua mkopo wa hata 70m na ile faida unayolipwa ikatumika kulipa Mkopo na bado 100m yako ipo safe.

Maisha ni Akili.
 
Back
Top Bottom