JE HOTUBA ALIYOITOA RAISI TRUMP SEPTEMBER 2018 JUU YA AFRIKA KATIKA MKUTANO WA UMOJA WA MATAIFA NI MATUSI AU NDO UKWELI?
Haya ni mambo yaliyonukuliwa katika hotuba ya Raisi Trump akiongelea bara la Afrika. Naomba usome na utoe maoni yako. Akiwa anawasuta viongozi wa Afrika, Trump anahoji kwamba:
- lkiwa sasa imefika miaka 50 ya uhuru na bado viongozi wengi wa Afrika wameshindwa kuwa na miundo mbinu thatbiti kwa ajili ya watu wao, je hao viongozi ni binadamu kweli?
- Anaendelea kusema kuwa ikiwa ninyi viongozi mnakalia dhahabu, almasi, mafuta na uranium na watu wenu wanakosa chakula, je ninyi viongozi wa afrika ni watu kweli?
- Kama mnakaa kwenye madaraka na kununua silaha kutoka kwa wageni na kuua watu wenu, je ninyi ni binadamu kweli?
- Kama mnawaza kukaa madarakani mpaka mwisho wa maisha yetu, je ninyi ni binadamu kweli?
- Ikiwa mnatumia maliasili ya nchi zenu kwa maendeleo ya familia zenu, je ninyi ni watu kweli?
- lwapo hamjali kuweka miundo mbinu ya afya za watu wenu na badala yake mkiugua mnaenda kutibiwa nchi za nje, Je ninyi ni binadanu kweli?
- Mtaheshimikaje katika mataifa yenu wakati mnapiga risasi raia wenu kama vile ni mchezo?
*Amemalizia kwa kusema kuwa viongozi wa Afrika wataendelea kuwa kama wanyama hadi watakapo badili mtazamo wao na kuheshimu watu wanaowaongoza.
NB: Hadi kufikia hapo, unadhani Raisi Trump inatakiwa alaumie kutokana na tabia zake za kutukana waafrika, au labda anachosema ni kweli tukubaliane na yeye?
Una maoni gani kutokana na hotuba aliyoitoa huko kwenye kikao cha umoja wa mataifa? Hizi ni dharau za wazungu au kuna ukweli ndani yake?
.