Utulivu wa kijamii kwa maendeleo umepata manufaa kwa China na sasa inaisaidia Afrika

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
gfdsfdgfdgsd.jpg

Hali ya usalama barani Afrika mwaka 2021

Viongozi wa Afrika wamejitolea kwa muda mrefu kuondoa mizozo ya silaha, kukuza amani ya kudumu na maendeleo barani Afrika, ili kufikia malengo yaliowekwa na Umoja wa Afrika.

Hata hivyo, malengo ya kuondoa kabisa mapigano na migogoro hayajafanikiwa kama ilivyopangwa. Kwa mujibu wa Ripoti ya Kimataifa ya Ugaidi mwaka 2020, nchi saba kati ya kumi zilizo na ongezeko kubwa la ugaidi zilikuwa katika kanda ya kusini mwa Jangwa la Sahara.

Mwaka 2021 pekee Afrika imeshuhudia matukio makubwa ya machafuko ya wenyewe kwa wenyewe na ugaidi.

Serikali ya Ethiopia bado inapigana kulidhibiti kundi la Tigray People's Liberation Front, TPLF na kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji zaidi ya watu milioni 1.7 wamekimbia makazi yao Kaskazini mwa Ethiopia kutokana na vita hivyo na wanahitaji msaada wa dharura.

Nchini Guinea mapinduzi ya serikali kinyume na katiba yameiingiza nchi hiyo ya Afrika Magharibi katika mgogoro wa kiuchumi.

Vitendo vya kigaidi vya kundi la Boko Haram Kaskazini mwa Nigeria zimeendelea kuwafanya raia wengi kukosa makazi, na kusababisha vifo kwa maelfu ya watu wasio na hatia.

Na hivi majuzi bomu lililipuka karibu na kituo kikuu cha polisi katika mji mkuu wa Uganda Kampala na kuua watu 7 na kujeruhi zaidi ya 30.

Kukosekana kwa utulivu wa kijamii kumesababisha madhara makubwa kwa uchumi na jamii ya baadhi ya nchi za Kiafrika.

Suluhisho la China

Hata hivyo bara hilo linaweza kuiga mitindo ya uongozi na nidhamu ya kijeshi kutoka China, ambayo inasisitiza utulivu wa kijamii kwa ukuaji wa uchumi.

Kukiwa na jeshi lenye nidhamu nidhamu, uwezekano wa mapinduzi utapungua.

Ulinzi wa taifa wa China unalenga kuzuia na kupinga uchokozi; kulinda usalama wa kisiasa wa kitaifa, usalama wa watu, na utulivu wa kijamii; kulinda nchi, kuleta umoja na uadilifu.

Kwa mujibu wa "sera mpya ya China kuhusu Ushirikiano wa China na Afrika katika Enzi Mpya", iliotolewa Mei 2021 uzoefu mkubwa wa China katika kudumisha utulivu na maendeleo una manufaa makubwa kwa Afrika..

Sera hiyo inaonyesha kuwa ushirikiano wa amani na usalama wa Afrika na China ni fursa muhimu kwake katika kuondoa ukosefu wa usalama na utulivu na kukuza ustawi na maendeleo yake yenyewe.

Sera hiyo inaeleza kuwa, China imejitolea kuimarisha uaminifu wa kisiasa kati ya China na Afrika, kupanua ushirikiano wa kivitendo na Afrika katika nyanja mbalimbali, na kutoa msaada wake ili kuimarisha amani na maendeleo katika bara hilo.

Kubadilishana na kuimarisha ushirikiano

Katika ufunguzi wa Mkutano wa Nane wa Mawaziri wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) huko Dakar Senegal, Rais Xi Jinping wa China alitaja nguzo tisa muhimu za ushirikiano kati ya pande hizo mbili.

Mojawepo wa nguzo muhimu ni kwamba China itatekeleza miradi 10 ya amani na usalama barani Afrika, kuendelea kutoa msaada wa kijeshi kwa Umoja wa Afrika, kuunga mkono juhudi za nchi za Afrika za kudumisha usalama wa kikanda na kupambana na ugaidi, na kufanya mazoezi ya kijeshi ya pamoja kati ya walinda amani wa pande zote mbili.

China ilianza kushiriki katika oparesheni za kulinda amani chini ya Umoja wa Mataifa mwaka 1990 na kufikia sasa asilimia 80 yawalinda amani wake wako barani Afrika.

Sera ya Mei inaonyesha kuwa zaidi ya wanajeshi 30,000 wa kulinda amani wa China wametumwa ili kukuza amani na kujenga jamii barani Afrika.

Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2021 China ilikuwa na takriban walinda amani 2,000 katika maeneo yenye hali tete zaidi nchini Mali, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Abyei, Sudan Kusini na Western Sahara wakichangia katika kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja wa ubinadamu.

Viongozi wa Afrika wanapaswa kuunganisha malengo na vitendo

Amani na usalama barani Afrika haziwezi kupatikana katika mikutano, lakini katika kuweka malengo yanayoweza kufikiwa na kuyatekeleza kwa dhati.

Katika Kongamano la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la 2021 lenye maudhui ya "Kushughulikia Chanzo cha Mizozo", Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alisema utawala mbaya unasababisha vitisho vikubwa kwa amani na usalama wa kimataifa.

Swala linguine lililotambuliwa kama linalochangia migogoro ni ukosefu wa usawa wa kijamii ambao unafanya baadhi ya tabaka la watu katika nchi kuwa hatarini dhidi ya matajiri wanaotawala.

Amani na utulivu wa China umepatikana kutokana na nia dhabiti ya uongozi ya kuwatumikia watu kiasi kwamba kuna sababu ndogo za kusababisha machafuko ya kijamii.

Mwakilishi wa Kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Zhang Jun anasema Maendeleo ni "ufunguo mkuu" wa kutatua matatizo yote, akitaka kuwepo na sera ya maendeleo inayozingatia watu na kuwashirikisha watu wote.

Viongozi wa Afrika wanaweza kujikita zaidi katika kuweka na kutekeleza mipango ya kiuchumi ambayo inawanufaisha wananchi moja kwa moja ili kupunguza mizozo na kujenga zaidi utulivu wa kijamii
 
asante kwa taarifa chief
 
Back
Top Bottom