Utumishi hivi mnatumia mfumo upi katika kupanga waomba ajira kulinga na kada zao?

Utumishi hivi mnatumia mfumo upi katika kupanga waomba ajira kulinga na kada zao?

knownless

Senior Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
172
Reaction score
47
Natumaini wote ni wazima. Imenibidi nianzishe uzi huu nikiwa naamini baadhi ya wahusika wa Utumishi wataona na wachangiaji wengine watatoa maoni yao.

Utumishi wametangaza kazi nyingi sana, ambalo ni jambo jema kwa sisi wasaka ajira.

Tatizo linaanzia kwa baadhi ya wasaka ajira kushindwa kuomba kazi wakiwa na vigezo na wakiwa wamesomea course husika. Wakiomba ujumbe unaokuja ni FAILED.

Nitatoa mfano mmoja wapo, nimejaribu kuomba nafasi ya Afisa Habari (Information Officer) nikiwa nimesomea Public Relations & Marketing lakini inakataa. Sasa mtu aliesomea Public Relations alafu mnamzuia kuomba kazi ya Afisa Habari sasa ataomba kazi ipi?.

Kibaya zaidi ukiingia kwenye account yako unakuta wamekuwekea ajira ambazo unaweza kuomba kulingana na course uliyosomea, lakini ukijaribu kuomba inakataa.

Fanyieni marekebisho haya kwani watu wengi wamekuwa wanalalamikia kitu kama hiki kwenye kada nyingine pia.
 
Afisa Habari anatakiwa kuomba mtu wa Mass Communication au Journalism.
Hio degree yako unatakiwa kuomba kazi za Mahusiano ya Umma mfano Public Relation Officer.
kulingana na majukumu ya kazi yaliyoainishwa, mtu aliyesoma course ya Public Relations anafanya kazi vizuri tu ya Afisa Habari.
 
Afisa Habari anatakiwa kuomba mtu wa Mass Communication au Journalism.
Hio degree yako unatakiwa kuomba kazi za Mahusiano ya Umma na Masoko mfano Public Relation Officer au Marketing Officer.
wangekuwa wanatafuta Mwandishi wa Habari hapo ingekuwa sahihi zaidi, lakini kama ni Afisa Habari, graduate wa Public Relations sioni unamkataa kwa kutumia vigezo gani.
 
Ungesoma Mass Communication au Journalism ungeomba na kuitwa Interview ila hio degree yako haihusiani na hio kazi.
kulingana na majukumu ya kazi yaliyoainishwa, mtu aliyesoma course ya Public Relations anafanya kazi vizuri tu ya Afisa Habari.
 
Hio degree yako haina uhusiano na kuwa Afisa Habari, wewe ni Mahusiano ya Umma na Masoko.
wangekuwa wanatafuta Mwandishi wa Habari hapo ingekuwa sahihi zaidi, lakini kama ni Afisa Habari, graduate wa Public Relations sioni unamkataa kwa kutumia vigezo gani.
 
Ukweli ni kwamba inawezekana wanaopanga au waliopanga hizi criteria za za ajira portal hawajui au hawana uelewa kuhusiana na bachelor degrees zinazotolewa Tanzania na zinahusiana na Mambo gani Kuna mkanganyiko Sana huko ajira portal na Nina wasiwasi Kuna baadhi ya advertised post huwa zinabaki bila kuombwa kwa kigezo Cha JOB APPLICATION FAILED
 
Hata degree ya mass communication inakataa mi ni muhanga pia katika nafasi hiyo ya information officer na Nimesoma masscommunication
hili ndio tatizo ninalozungumzia hapa, kama na wewe wa Mass Communication inakataa sasa nani ataomba hiyo nafasi? kuna tatizo kubwa katika huko Utumishi.
 
Hio degree yako haina uhusiano na kuwa Afisa Habari, wewe ni Mahusiano ya Umma na Masoko.
mkuu kama hii nafasi ingekuwa inahitaji Mwandishi wa Habari ningekubaliana na wewe kabisa kwa sababu mtu aliesoma Public Relations kuna baadhi ya vitu vichache anakosa. Ila kwa Afisa Habari, mtu aliesoma Public Relations anaimudu vizuri sana. Labda kama hautojali unaweza share hapa ni kitu gani kinamfanya mtu aliesoma Public Relations ashindwe?
 
Ukweli ni kwamba inawezekana wanaopanga au waliopanga hizi criteria za za ajira portal hawajui au hawana uelewa kuhusiana na bachelor degrees zinazotolewa Tanzania na zinahusiana na Mambo gani Kuna mkanganyiko Sana huko ajira portal na Nina wasiwasi Kuna baadhi ya advertised post huwa zinabaki bila kuombwa kwa kigezo Cha JOB APPLICATION FAILED
Haya pia ni mashaka yangu. Nahisi watu wa Utumishi wanapaswa kutembelea vyuo mbalimbali waweze kuongeza maarifa kuhisiana na ufahamu wa Degrees zinazotolewa.

Utumishi walishawahi kutoa kazi za Customer Services kupitia TTCL, alafu mtu aliesoma Public Relations hawezi kuomba, unabaki unajiuliza hivi hawa wanaopanga criteria hizi wanaelewa vizuri haya mambo?
 
Itakua labda kuna shida maana mimi nimesoma Bcom Marketing ila nikiomba kazi ya Afisa Biashara inagoma na vigezo wamesema watu wa Shahada/Stashahada ya juu ya Masoko.
 
Itakua labda kuna shida maana mimi nimesoma Bcom Marketing ila nikiomba kazi ya Afisa Biashara inagoma na vigezo wamesema watu wa Shahada/Stashahada ya juu ya Masoko.
Utumishi wanatakiwa wajitathimini upya kwenye kazi wanzotoa, isije kuwa hizi nafasi zinatumika kisiasa. Zinaonekana zimetolewa kazi 1900 kumbe ambazo zinatakiwa kujazwa ni 200 tu.
 
Suluhisho ni nini sasa?? Maana ofisini pia hawapo wameachwa walinzi tu ndio nao hawaelewi, ukifika unapewa karatasi uandike jina na I'd namba yako na tatizo lako, unamuachia mlinzi
 
Endelea kuomba Kila baada ya mda au siku mie ishanitokea mara moja nilijaribu kuapply kazi akagoma na sifa ninazo nikaachana nayo baada ya siku kazaaa jamaa yangu akaniambia ajira Portal Kuna kazi flan umeiona nikamuambia ndio nilijaribu kuapply ikakataa akasema yeye now kaapply imekubari na mie nikaenda kujaribu Tena ikakubali ikaenda sehemu ya kuwekaa barua so chap nikaandika barua nikatuma so Kuna wakati inakataa na Kuna mda inakubali
 
Back
Top Bottom