Mama Amon,
Watu wanafikiri tume ya uchaguzi inaundwa na watu wasiyotoka kwenye jamii.
Ni vigumu kwa jamii isiyo na elimu na uelewa wa mambo kutenda haki.
Yako mazingira mengi sana yanayokwamisha ufalme wa Mungu.
Mazingira haya yanaanza chini kabisa ngazi ya familia na yanapanuka mpaka ngazi ya utawala na mamlaka.
Tazama kwa mfano, mfumo wa ndoa katika jamii zetu ; utaona unapinga ufalme wa Mungu.
Familia ambayo ndiyo kilele cha jamii na taifa yenyewe inapinga ufalme wa Mungu ; je hiyo inaweza kutenda au kusimamia haki?
Ninachotaka kusema hapa ni kuwa tunataka maendeleo, lakini hatujui nini tufanye ili tupate maendeleo.
Makosa yetu yako kwenye ndoa na familia. Hapa ndipo ufalme wa Mungu unapingwa vikali.
Hizi taasisi au mamlaka, mathalani tume ya uchaguzi zinaaksi mfumo wa ndoa na familia zetu.
Ukweli ni kwamba hakuna chama chochote cha siasa au tume ya uchaguzi inayoweza kubadilisha matokeo ya uchaguzi kama jamii husika ina elimu na uelewa wa mambo.
Ukitazama kwa mfano, sheria mama na sheria zingine zinavyosema juu ya tume ya uchaguzi, mtu makani anaelewa kabisa jamii hii elimu, uelewa wake wa mambo ni wa chini kabisa au haupo.
Tusifikiri makosa yako kwenye tume ya uchaguzi katika kufanya ufalme wa Mungu usifike. Kosa letu kubwa ni mfumo wa ndoa na familia turudi huko turekebishe na ufalme wa Mungu utafika.