Ramark, p
Haya ni maswali ya msingi sana.
Hebu niyajibu kadiri ya ufahamu wangu, moja baada ya jingine:
SWALI: Hiyo tume itaundwa wapi?
JIBU: Tume itaundwa kwa mujibu wa sheria. Hivyo, Bungeni ndio mahali mwafaka. Lakini, safari ya kufika Bungeni inaweza kuanzia mahakamani, kama kutakuwepo na haja ya kupata amri/mwongozo wa Mahakama.
SWALI: Mswada utapelekwa na nani?
JIBU: Muswada wa sheria ya kufanya mageuzi kwenye sheria za NEC na Katiba ya Nchi, unaweza kupelekwa Bungeni na mbunge yeyote wa CDM kama hoja binafsi au ukapelekwa na mwanasheria mkuu wa serikali kama hoja ya serikali. Kunahitajika mchakato wa ushawishi na utetezo kumfanya mwanasheria wa serikali akubali kubeba hoja hii.
SWALI: Mswada utaandaliwa na nani?
JIBU: Muswada wa sheria ya kufanya mageuzi kwenye sheria za NEC na Katiba ya Nchi, unaweza kuandaliwa na mbunge yeyote wa CDM kama hoja binafsi au ukaandaliwa na mwanasheria mkuu wa serikali kama hoja ya serikali. Kunahitajika mchakato wa ushawishi na utetezo kumfanya mwanasheria wa serikali akubali kuandaa muswada huu.
SWALI: Mfumo WA maoni ya wadau utazingatiwa vipi na nani [atayakusanya]?
JIBU: Maoni ya wananchi tayari yanafahamika kupitia Tume ya jaji Warioba, Tume ya jaji Nyalali na Tume ya Jaji Kipenka. Kinachohitajika ni desk-reserach pekee.
SWALI: Je, wanadau na wabunge wanajua tume tunayoitaka [au Tume inayotakiwa]?
JIBU: Sio wadau wote wanajua Tume inayotakiwa. Lakini, ripoti za Tume ya jaji Warioba, Tume ya jaji Nyalali na Tume ya Jaji Kipenka zinatoa mwanga kuonyesha aina ya Tume inayotakiwa kulingana na maoni ya wananchi waliotoa maoni yao. Bandiko langu hapa na makala za waandishi baki tayari zimetoa fursa kwa umma baki kujua muundo wa Tume unaotakiwa na wananchi hao.
SWALI: Ninyi wapinzani mna majority ya kupitisha jambo linalichefeua serikali na dola yake?
JIBU: Kwa mujibu wa party caucuses tulizonazo, wapinzani hatuna majority ya kupitisha muswada wa Tume huru. Lakini, endapo Bunge litabeba hoja hii kama hoja ya kitaifa, badala ya kuichukulia kama hoja ya wapinzani, majority support itapatikana Bungeni. Kuna kazi kubwa ya ushawishi na utetezi inahitajika hapa. Na kama kazi ya ushawishi na utetezi haitafanyika vizuri, huenda kipengele hiki kikawa ndio show stopper!
SWALI: Mnaweza kuwabadilisha wabunge vilaza WA ccm kufikiri kama binadamu WA taifa hili?
JIBU: Uwezo wa kuwabadilisha kwa hoja zenye ushahidi (logical appeal) tunao. Uwezo wa kuwabadilisha kwa hoja zenye hisia (emotional appeal) tunao. Na bahati nzuri wabunge wa CCM wanaofikiri kiitikadi hawazidi 49% ya wabunge wa CCM. Uwezo tunao, nia tunayo na sababu tunazo.
SWALI: Mnaweza kuunda tume huru kwa dikrii ya rais?
JIBU: Hapana, Tume Huru haiwezi kuundwa kwa decree ya Rais kwa kuwa Tanzania ni Jamhuri. Bunge lazima lifanye kazi yake kwa niaba ya umma.
MWISHO:
Kuna swali ambalo hujauliza. Ni hili: Je, nyie wapinzani mnayo fedha kwa ajili ya kuendesha kampeni ya mageuzi katika Tume ya Uchaguzi kama maswali hapo juu yanavyoonyesha?
Jawabu langu ni rahisi. Nimemsikia Mbowe anasema kuwa ajanda hii ni kipaumbele chake cha kwanza. Huenda ameshafanya mchanganuo wa kibajeti na kuendesha harambee ya kutafuta fedha inayohitajika.
Ni maoni yangu kuwa kiasi cha TZS 1,000,000,000/= zinahitajika ili kufanikisha ajenda ya Tume Huru ya Uchaguzi. Yaliyotokea juzi wakati wa kulipa faini ya viongozi waliofungwa yanaonyesha kuwa Freeman Mbowe anao uwezo wa kutafuta fedha hizi kwa haraka. Tunaomba mchango wako Mhe. Ramark!