Uungwana ni vitendo: Je, CHADEMA watarudisha Tsh. 38 milioni zilizotolewa na hayati Magufuli kumtoa Msigwa jela?

Uungwana ni vitendo: Je, CHADEMA watarudisha Tsh. 38 milioni zilizotolewa na hayati Magufuli kumtoa Msigwa jela?

Siku hizi uungwana ni vitendo sio maendeleo hayana vyama?!
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ikumbukwe kuwa hayati Magufuli kama mwanafamilia alichangia Tsh. 38,000,000 katika mchango wa wanafamilia ili kuwezesha malipo ya faini ya mchungaji Msigwa.

Pamoja na ukweli kwamba fedha hizi zilitumika kumtoa Freeman Mbowe kwani mchungaji Msigwa alibahatika kutoka kwa michango ya wanachama na sisi wadau wa siasa.

Je, CHADEMA watarudisha hizi tsh 38m kwa familia ya mwendazake Magufuli?

Uungwana na Vitendo.

Jumapili njema!
 
Kiungwana Msigwa anatakiwa kurufisha ile pesa. Ni kama umechangiwa hela ya arusi halafu ukahairisha.

..Dr.Mashinji alitolewa na CCM-DSM hivyo fedha itarudi kwenye chama.

..Msigwa inasemekana Magufuli alichangia kama mwanafamilia hivyo fedha zitarudishwa kwenye FAMILIA nao wataona namna ya kugawana..

..Wafungwa wengine 7 walitolewa kupitia michango iliyosimamiwa na CHADEMA hivyo fedha hizo zitarudi ktk chama chao.

NB:

..Dr.Mashinji hakuwa miongoni mwa wakata RUFAA, lakini mahakama kuu imeamua kwamba hata yeye atafaidika na kufutiwa hukumu kama waliokuwa wafungwa wenzake.

Cc Fundi Mchundo
 
Kumbukumbu zangu zinanikumbusha offer ya Msigwa kutolewa kwa mchango huo chama na msigwa mwenyewe waliikataa.mwenye kumbukumbu nzuri atuletee kwa rejea.
Mchungaji Msigwa alikataa offer ya CCM kupitia kwa Polepole.

Ila " mzigo" wa wanafamilia wa mchungaji Msigwa ulipokelewa na chama!
 
Mchungaji Msigwa alikataa offer ya CCM kupitia kwa Polepole.

Ila " mzigo" wa wanafamilia wa mchungaji Msigwa ulipokelewa na chama!

..hapo unapotosha.

..fedha zilizochangwa na familia ya Msigwa + Magufuli ziliwasilishwa mahakamani na mkurugenzi wa habari wa Ikulu Gerson Msigwa akiambatana na kaka yake Mh.Msigwa.

..Chadema hawakupokea fedha hizo.
 
Ahsante kwa ufafanuzi.

Halafu nani alitolewa baada ya malipo haya?
 
Chama ni nini? Ni sare za chama? au katiba ya chama? Je walisukumwa na mambo binafsi au imani ya chama? Kasome kamusi.
Huo muktadha wako hauingii kwenye kesi hiyo, wao walishitakiwa Kama mtu mmoja mmoja sio chama, na hukumu ikatoka Kwa muktadha huo huo ndio maana kila mtu alipigwa faini yake peke yake na viwango tofauti pia
 
Wataenda kuongezea zege kwenye kaburi lake ili ata siku ya ufufuko ashindwe kutoka afe Tena. Ikiwezekana resho ya sementi waeke Kali sana yani mifuko 2 ya sementi kwa ndoo 5 za mchanga
Angewekewa jiwe kubwa juu ya kaburi abaki kuzimu,milele na milele.
 
..Dr.Mashinji alitolewa na CCM-DSM hivyo fedha itarudi kwenye chama.

..Msigwa inasemekana Magufuli alichangia kama mwanafamilia hivyo fedha zitarudishwa kwenye FAMILIA nao wataona namna ya kugawana..

..Wafungwa wengine 7 walitolewa kupitia michango iliyosimamiwa na CHADEMA hivyo fedha hizo zitarudi ktk chama chao.

NB:

..Dr.Mashinji hakuwa miongoni mwa wakata RUFAA, lakini mahakama kuu imeamua kwamba hata yeye atafaidika na kufutiwa hukumu kama waliokuwa wafungwa wenzake.

Cc Fundi Mchundo
Swali langu ni jee wanafamilia wa Mswiga walikabidhi hizo pesa kwa Chadema au walilipa mojamoja kwa moja serikalini? Kama walikabidhi kwa Chadema, Chadema wanaweza kusema zilikuwa ni mchango wa pamoja wa kuwalipia faini wanachama wao na si mwanachama mmoja in particular. Ombi la Chadema lilikuwa ni kwa wanachama wao kwa ujumla wao na kila aliyechangia alijua hivyo. Kama ni hivyo Chadema watakuwa na haki ya kuzitumia kwa namna ambavyo wataona ina manufaa kwa chama. Ila wanafamilia wakidai warudishiwe basi bila shaka watawajibika kuwarudhia.

Lakini naona hapa tumeenda mbio sana. Wakina Yohana Mbatizaji wanataka watu waamini pesa zimeishatoka kama ilivyokuwa kwenye suala la ruzuku. Ni safari ndefu mpaka pesa zitoke. Na kuna uwezekano wasirudishiwe kabisa kama vile watumishi wanaoidai serikali wanavyofanyiwa. Wanataka tu kumwaga sumu.

Amandla....
 
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ikumbukwe kuwa hayati Magufuli kama mwanafamilia alichangia Tsh. 38,000,000 katika mchango wa wanafamilia ili kuwezesha malipo ya faini ya mchungaji Msigwa.

Pamoja na ukweli kwamba fedha hizi zilitumika kumtoa Freeman Mbowe kwani mchungaji Msigwa alibahatika kutoka kwa michango ya wanachama na sisi wadau wa siasa.

Je, CHADEMA watarudisha hizi tsh 38m kwa familia ya mwendazake Magufuli?

Uungwana na Vitendo.

Jumapili njema!
"Ikumbukwe kuwa hayati Magufuli kama mwanafamilia alichangia Tsh. 38,000,000 katika mchango wa wanafamilia ili kuwezesha malipo ya faini ya mchungaji Msigwa".

Kumbukumbu hizo zipo kwa sababu ziliwekwa wazi, ila pesa hizo kutumika kumtoa Mbowe ni mtazamo wako, na ni haki yako kuwa na mtazamo hasi ama chanya. Muhumu ni kutoharibu haki za wengine.

Na kama kutakuwepo madai yoyote juu ya pesa hizo basi litakuwa jukumu la Msigwa na familia yake.
 
Msigwa aligoma kutolewa na pesa za dhalimu mwendazake. Acha uongo. Hata gari la maccm aligoma kupanda.
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ikumbukwe kuwa hayati Magufuli kama mwanafamilia alichangia Tsh. 38,000,000 katika mchango wa wanafamilia ili kuwezesha malipo ya faini ya mchungaji Msigwa.

Pamoja na ukweli kwamba fedha hizi zilitumika kumtoa Freeman Mbowe kwani mchungaji Msigwa alibahatika kutoka kwa michango ya wanachama na sisi wadau wa siasa.

Je, CHADEMA watarudisha hizi tsh 38m kwa familia ya mwendazake Magufuli?

Uungwana na Vitendo.

Jumapili njema!
 
Pia wataondoa ule uzio wa mabati
Watazipeleka pale Chato kama rambirambi... au kama vipi ili kumuenzi wataukarabati ule uwanja wa ndege kwa kuweka majosho ya kuogeshea ng'ombe baada ya ng'ombe hao kuota jua uwanjani.
 
Back
Top Bottom