Yehoshafati Elton
Member
- Aug 7, 2022
- 12
- 1
Utangulizi na kauli kuhusu tatizo
Biashara ya samaki ni biashara inayokua kwa kasi sana hapa kwetu nchini Tanzania. Na hii ni kwa sababu ya uhitaji mkubwa sana wa samaki kama kitoweo chenye gharama nafuu na chanzo cha protini miongoni watu walio wengi, hasa wale wa hali ya chini na chanzo cha kuzalisha bidhaa zingine. Kwa hiyo uwepo wa biashara hii unasaidia sana upatikanaji wa chakula cha kutosha, si hivyo tu hata utengenezaji wa ajira, hivyo kuboresha maisha ya watu na taifa kwa ujumla.
Namna nzuri ya samaki na bidhaa zake kuwafikia watumiaji bado imekuwa ni changamoto kubwa. Changamoto hii inasababishwa na sababu kadha wa kadha zikiwemo zile za bidhaa zenyewe na zile zinazosababishwa na watu, kama ifuatavyo; uwezo wa kuharibika wa bidhaa hii, uhitaji wa uchakataji kwa ajili ya kupunguza uzito na kuongeza thamani kabla ya kuipeleka kwa watumiaji, kukosekana kwa mwunganiko mzuri kati ya wavuvi/wazalishaji/wakulima, watu wa kati na watumiaji/wanunuzi. Pia ukosefu wa vifaa maalumu kwa ajili ya kuchakata na kutunzia bidhaa ya samaki, hizi ni changamoto miongoni mwa wafanyabiashara walio wengi. Pia maarifa ya namna ya kutafuta masoko miongoni mwa wakulima na wazalishaji ni miongoni mwa changamoto pia.
Kumekuwepo na utumiaji wa namna nyingi za kuhakikisha kwamba bidhaa hii ya samaki inawafikia watumiaji kwa muda mwafaka na namna rafiki, kama utumiaji wa watu wa kati (middle men), kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kama facebook, whattap, instagram n.k. Na hii inafuatana na maendeleo makubwa ya sayansi na tekinolojia ambayo yamepelekea mwamuko wa kuanza kutumia mitandao kwenye kuuza na kusambaza bidhaa hii muhimu.
Maendeleo yameshuhudiwa kupitia utumiaji huu wa mitandao, lakini bado kuna changamoto kwamba mwunganiko mzuri haujawekwa kati ya wazalishaji na watumiaji.Wakati mwingine watu wa kati wanateneneza faida kubwa kuliko wazalishaji/wavuvi hivyo kuwaacha wazalishaji katika hali ambayo si nzuri. Wakulima na wazalishaji wanajikuta wakitengeneza faida ndogo kwa kuwauzia watu wa kati kwa bei ambayo ni ndogo sana. Lakini pia ukosefu wa vifaa bora vya kutunzia samaki kama friza baada ya kuvuliwa ama kuvunwa.
Maana na malengo ya biashara
Biashara hii inahisu uuzaji na usamabazaji wa samaki (wabichi, wakavu na waliokaangwa) katika jiji la Dar es Salaam kupitia aplikesheni maalumu ya samaki kiganjani mwako. Biashara hii inahusisha utumiaji wa aplikesheni yenye kuonyesha kila bidhaa ambayo itakuwa sokoni katika siku husika, halafu mteja mwenye aplikesheni hii ana uwezo wa kuchagua bidhaa anayoipenda, na baada ya hapo atapelekewa popote atakapokuwa ndani ya jiji la Dar es Salaam. Biashara hii itakuwa na mfano wa uendeshaji wa kampuni za usafiri za uber na bolt, kwamba mtu ana uwezo wa kuomba bidhaa aitakayo kupitia aplikesheni hii maalumu ya samaki kiganjani mwako, wakati wowote na akaipata katika muda ambao ni mwafaka kabisa, kwa hiyo upekee wa biashara hii upo hapa kwenye namna ya uendeshaji wake.
Kwa hiyo biashara hii itakuwa inaundwa na sehemu kuu tatu ambazo ni; ukusanyaji wa samaki kutoka kwa wavuvi na wakulima wa samaki kwenye masoko ya samaki na sehemu za mabwawa, utunzaji na uchakataji (hapa kutakuwa na vifaa maalumu kwa ajli ya kutunza na kuchakata samaki kama friza na majiko maalumu) na mwisho ni usambazaji (hapa kutakuwa na vifaa vya usafiri kama pikipiki n.k) na hapa mtumiaji anatakiwa awe na aplikesheni ya samaki kiganjani mwako. Biashara hii pia, inalenga kurahisisha upatikanaji wa samaki miongoni mwa watumiaji kupitia aplikesheni hii maalumu.
Picha. Kuonesha mfano wa mfumo, namna biashara inavyoundwa.
Faida za biashara
Biashara hii itasaidia kurahisisha upatikanaji wa samaki katika namna nzuri na rafiki kwa watumiaji, kwa kutumia fursa adhimu kabisa ya intaneti kupitia aplikesheni ambayo itatumika na inatumika sana kwa sasa hasa maeneo ya mijini, kuokoa muda kwa wale watu wanaokosa muda wa kutembelea sehemu za masoko ya samaki.
Mbali na hayo yote biashara hii itasaidia kuongeza thamani ya samaki kwa sababu watu wa kati watapungua sana, na pia mwunganiko wa wazalishaji na watumiaji utaimarishwa sana. Kuongeza ajira kwa vijana na watu wengine kupitia utumiaji chanya wa fursa ya aplikesheni na intaneti kwa ujumla wake kwa sababu kuanzia wavuvi, wakulima, wabeba samaki na madreva wote wanaenda kufaidika na biashara hii, hivyo maisha ya watu yataboreka na taifa kwa ujumla wake. Intaneti inaendelea kuonesha matokeo makubwa sana kwenye sekta ya hii ya biashara hivyo utumiaji wa mitandao kwenye namna ya chanya ya biashara hii inaenda kuleta sura nyingine kabisa.
Hitimisho
Intaneti ikitumiwa vizuri inaweza kuleta matokeo chanya kwenye kufanya biashara, hasa biashara hii ya samaki. Biashara hii inahitaji uweledi mkubwa, kuanzia maarifa na vifaa vyenye ubora kwa ajili ya kuifanikisha. Matumizi ya aplikesheni ni namna mojawapo ambayo itakuwa msaada mkubwa kwenye kuifanikisha biashara hii.
Ni jambo la kuaminika kabisa ya kwamba matumizi ya intaneti yameshika kasi sana na yanatumiwa na watu walio wengi hasa maeneo ya mijini. Kwa hiyo fursa ya kutumia intaneti kwa mfumo wa aplikesheni inaenda kuleta sura mpya na maendeleo makubwa kabisa katika sekta hii ya biashara ya samaki.

Upvote
3