Parabolic
JF-Expert Member
- Dec 3, 2013
- 2,922
- 3,252
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Mohammed Ali Kawaida, amewakosoa vikali baadhi ya vijana hasa wale wa CHADEMA kwa kile alichokiita kejeli na kubeza hotuba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa uzinduzi wa Tume ya Rais ya Uchunguzi wa Ghasia na Ukiukaji wa Sheria Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.
Soma zaidi: Rais Samia: Tumeamua kuwashirikisha wenzetu kutoka Uganda na Namibia kupata muono mpana
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya viongozi wa Seneti za Vyuo na Vyuo Vikuu, Kawaida ameeleza kuwa kejeli hizo hazina afya kwa taifa na zinalenga kuvunja moyo na kudhoofisha jitihada za Rais Samia za kuleta maridhiano ya kisiasa, haki, na ukweli nchini.Kawaida amesisitiza kuwa UVCCM na vijana wa CCM wanaunga mkono kwa 100% kuundwa na kuanza kazi kwa Tume hiyo.
Katika hatua ya kuonesha msisitizo wa uwazi na haki, Kawaida amewataka makamishna na watendaji wa Tume hiyo kufanya kazi yao kwa weledi mkubwa bila kumwogopa au kumwonea mtu yeyote muhali.
