#COVID19 UVIKO-19 Tanzania: upo au haupo?

Tukubaliane pamoja na mapungufu yote ya hayati JPM Alikuwa ni visionary leader !!
Acha kumung'unya maneno JPM alikuwa mwamba kwelikwel alikwamishwa na wanafki walioamua kum- yuda eskariot.
Hayo unayoita mapungufu ni unafki mwingine, unaogopa kuongea ukweli sababu utashambuliwa hapa na mapandikizi ya wanafki humu wasio hata na tone la aibu.
 
Hiyo ya enzi hizo ilikuwa kali sana. Mi nilipigwa 2021. Alimanusura... Ni jambo la kumshukuru Mungu. Kwa kweli usiombe. Mdudu kachukuwa mpaka maisha ya Rais wa nchi. Halafu mtu amekula makande yake huko anakuja hapa anajamba eti hakuna corona Tanzania!!
Nilipigwa na uviko mwaka 2020 mwanzoni, ila namshukuru Mungu kwa kunivusha salama maana shughuli yake sio mchezo.
 
UVIKO upo isipokuwa Tanzania haijawahi kuwa na mlipuko wa kuleta taharuki...

Nimeshuhudia wageni wengi wakiwa na maambukizi haswa wanaotoka ng'ambo lakini yanakuwa yasiyo na madhara kivileeee...
 
Noma sana! Nikikumbuka shughuli ya kubanwa mbavu na kukosa pumzi mpaka unahisi unaweza kukata moto muda wowote sio mchezo.
Mungu aepushe mbali isijirudie tena ile hali
 
Ugonjwa haupo, ila inabidi tuendelee kukusanya data feki ili taarifa za matumizi ya fedha tulizopewa zionyeshe tunaendelea kupambana
 
UVIKO upo isipokuwa Tanzania haijawahi kuwa na mlipuko wa kuleta taharuki...

Nimeshuhudia wageni wengi wakiwa na maambukizi haswa wanaotoka ng'ambo lakini yanakuwa yasiyo na madhara kivileeee...
Kilichoisaidia Tanzania ni umri wa watanzania wengi upo chini ya miaka 30, na wazee ni wachache sana, lakini pia wazee wengi wametangulizwa mbele ya haki, ila kwa kuwa wengi sio wale high profile figures, nobody cares !!
 
Hata mimi nilikuwa na akili kama hizo za kuamini uviko haupo.Uliponipiga wiki 5 kitandani hadi kwenye oksijeni hapo ndipo akili ilinirudia. Endeleeni kuubeza huu ugonjwa kwamba haupo.Ila ole wake yule abezaye.Ukikukamata ndiyo utajua hujui. Halafu uviko una tabia moja nzuri.Miamba ambao wanaudharau huwa lazima wapigwe siku moja sijui kwa nini
 
Ivi mkuu umefikisha 18 years kwel, mbna unakua hovyo Ivo, yaan mpaka Leo unaamini magu kaondoshwa na covid.
Pumbav kabsa!
 
Juzi nilichapwa Mafua Makali, koo kuuma Sana na kichwa. Yaani nilipiga sukutuo la chumvi na kuwahi hospital. Niliogopa isije ikawa imenirudia mara ya pili. Nilitumia antibiotics na natural herbs. Niko poa sasa. Hakika Mungu aendelee kutulinda na hili jitu. Mwaka jana lilitikisa Sana Moshi na Arusha na Baba lao DSM. Mwanza nako nasikia ilikuwa ni balaa. Shida hatuna statistics Ila tulizika Sana.
 

Kwani Mama anasemaje
 
halafu baada ya kufariki tu kasi ya ugonjwa nayo ikapungua!!!
 
mtu mzima mwenye taarifa kama hizi kichwani ni hasara kwa taifa.

kumbe sio ugonjwa wa moyo kama wasemavyo wataalam!!!
 
Mwaka 2020 kuna mzee mmoja alikuwa mbishi sana na uviko anakaa Moshi..
Aliniambia corona hakuna kabisa na alikuwa anamsikiliza na kumwamini Magufuli kwa asilimia 100.
Nikaja kukutana naye baada ya miezi mitatu mbele.. Amepungua vibaya sana kama kilo 15 hivi. Akitembea anapepesuka..
Nikahisi nimemfananisha akaniambia alilazwa December 2020 yote KCMC kisa Corona.. Hakuweza kula ilikuwa ni dripu.. Na kidogo aage Dunia..
Alisema kwa mdomo wake mwenyewe Corona haina masihara
 
Ivi mkuu umefikisha 18 years kwel, mbna unakua hovyo Ivo, yaan mpaka Leo unaamini magu kaondoshwa na covid.
Pumbav kabsa!
kuna kundi kubwa la wanaume kati ya miaka 18-40 ni wajinga kupita kiasi.

wanamiliki simu na wanajua kusoma na kuandika,ila hawachagui cha kusoma na kuandika.
 
corona haimlazi mtu mpaka kukonda,hukutafiti vyema anaumwa kitu gani.

corona ni siku kadhaa tu.
 
corona haimlazi mtu mpaka kukonda,hukutafiti vyema anaumwa kitu gani.

corona ni siku kadhaa tu.
Huyo Mzee alikuwa na presha ya kawaida.. Ila uviko ilivyompata presha ikakataa kushuka.. Akazidiwa.. Hamu ya kula ikapotea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…