Uvumi kuwa Mzee Kikwete yupo nyuma ya Uongozi wa Rais Samia unaweza kuwa Kikwazo cha Ufanisi na chanzo cha kuhujumiwa kwake

Uvumi kuwa Mzee Kikwete yupo nyuma ya Uongozi wa Rais Samia unaweza kuwa Kikwazo cha Ufanisi na chanzo cha kuhujumiwa kwake

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
8,018
Reaction score
16,802
Kuna hatari fulani nimeanza kuiona, kuna maneno fulani nimeanza kuyasikia na kuna Mipango fulani ya kukomoana na kuhujumiana ndani kwa ndani nimeanza kuisikia pia.

Mimi sina uhakika kuwa kwa sasa Rais Samia ni TV Screen tu ila Rais Mstaafu Kikwete ndiye Remote Control kama watu wasemavyo, ila kama hili lina Ukweli basi kuna Hatari moja Kubwa ndani ya CCM na Serikali naiona inaenda kuja (kutokea)

Na wewe Rais Mstaafu Kikwete kama ni kweli una Ushawishi mkubwa katika Utawala huu wa Rais Samia tafadhali jishtukie upesi, kaa mbali nae na mwachie Mama nae atengeneze Legacy yake kwa huongelewi vyema na Watu wa Kanda ya Ziwa hasa baada ya Tukio Kubwa nchini la tarehe 17 Machi, 2021.

Kuna Taa Nyekundu ninaiona mahala!
 
Sukuma gang watulie, zama zao zimekwisha rasmi.

Hakuna cha kanda ya ziwa wala kanda bongoman.

Hebu tuwahi Zanzibar tukapokee ndege zetu mpya.

Ndio mjuwe hizi ni zama nyingine, si zama zile za kila siku jitu moja tu kwenye matukio yote na kujiona ndio ana akili kuliko watu wote.
 
Kwa Ubongo Uharo ulionao kamwe hutoweza kunielewa na ni vyema tu ukakaa Kimya au ukawapisha wale Brainy Members wa JF walionielewa waujadili (wajadili) sawa?
 
Sukuma gang watulie, zama zao zimekwisha rasmi.

Hakuna cha kanda ya ziwa wala kanda bongoman.

Hebu tuwahi Zanzibar tukapokee ndege zetu mpya.

Ndio mjuwe hizi ni zama nyingine, si zama zile za kila siku jitu moja tu kwenye matukio yote na kujiona ndio ana akili kuliko watu wote.
Asante kunisaidia kuwajibu hao sukuma Gang,..kipindi cha mwenda zake walijiona wenyewe ndo vijeba😂😂😂
 
Sukuma gang watulie, zama zao zimekwisha rasmi.

Hakuna cha kanda ya ziwa wala kanda bongoman.

Hebu tuwahi Zanzibar tukapokee ndege zetu mpya.

Ndio mjuwe hizi ni zama nyingine, si zama zile za kila siku jitu moja tu kwenye matukio yote na kujiona ndio ana akili kuliko watu wote.
Hii akili ya Sukuma Gang kwa kila andiko ni kufilisika kimawazo na ni lugha chafu ya kiubaguzi. Mimi si Msukuma ila naamini usawa na udugu tulioujenga kwa miaka mingi. Jadili hoja acha kuhamisha mjadala kwa lugha zako mfilisi za ukabila .SHAME ON YOU
 
Bi mkubwa naona hana INNER CIRCLE, wengi wamemtenga anapambana peke yake. Msukuma aliweza kuwakabi wapinzani wake chaman kwa kutumia nguvu ya dola.

Alipoondoka mavampaya yanarudi kwa kasi yanamuhujumu waziwazi na mama mzito kutumbua watu. Huruma yake ya umama na inferiority complex yake kutokana na jinsia yake inamuangusha. Ccm B inarudi ngoje tuone uchaguzi ndani ya chama mwakani ndio tutapata picha kamili
 
Leo umeongea point kubwa mwenye maskio na asikie, na hizi kejeli zinazoendelea juu ya Hayati Magufuli tujipe muda tu.

Kwa ufupi watu wa kanda ya ziwa kwa 100% wanajua ya kwamba kuna kitu kibaya kilitendeka kwa Hayati
 
Si wangemuacha hata chenkapa,

Kosa lake ni kumpigia debe yule jamaa ndo iwe hivo kweli........!
 
Sio kila uvumi ni WA kutilia maamani,mengine ni upuuzi kwa hiyo unapotezea..

Hata hivyo hivyo JK ni mtu wa heshima na amefanya Kazi kubwa Tzn na ndio Mkuu wa Nchi aliyebaki kwa ushauri baada ya wengine kitangulia,hata Mwendazake alikuwa ana mconsul na hakuna tatizo hata Samia kuwa nyuma yake.

Mwisho kwani hujawahi sikia Obama yuko nyuma ya Biden? Tatizo liko wapi?
 
Hii akili ya Sukuma Gang kwa kila andiko ni kufilisika kimawazo na ni lugha chafu ya kiubaguzi. Mimi si Msukuma ila naamini usawa na udugu tulioujenga kwa miaka mingi. Jadili hoja acha kuhamisha mjadala kwa lugha zako mfilisi za ukabila .SHAME ON YOU
Hawa viumbe ni watu wa ovyo sana.Wao wanaamini wanawakomoa wasukuma, Kila kitu wanajificha nyuma ya hoja ya sukuma gang.Kuna watu sio wasukuma na wala hawana mafungamano yyt na hilo gang lkn hawakubaliani na hali iliyopo. Kitendo cha wao kuendelea kuhubiri ubaguzi wa sukuma gang ni kutengeneza bomu hatari sana.
 
Kwa zile Kashfa, matusi mazito, kejeli, kuvuja kwa siri nzito za serikali kutokea sehemu ambayo huwezi dhania.

Kisha leo ghafla ukurasa uleule unageuka kuwa rafiki wa serikali mpya baada ya kifo cha Hayati Magufuli inatia mashaka sana nani ni mhusika wa ukurasa ule?

Aendelee kupumzika Shujaa wa Tanzania mpya.
 
Back
Top Bottom