All in all
New Member
- Jun 7, 2023
- 1
- 1
Utangulizi
Uwajibikaji waweza kuwa ni njia ambayo inaweza kuleta chachu ya mabadiliko na maendeleo katika jamii. Uwajibikaji waweza kufanywa na mtu mmoja au zaidi na pia unaweza kuhusisha kikundi Cha watu wenye mipango ya kutimiza malengo Fulani katika jamii yao.
Uwajibikaji ni hali ya kujihusisha au kufanya jukumu Fulani la kimaendeleo. Uwajibikaji Kati ya mtu au watu katika jamii husababishwa na utawala bora, ambapo kila anaweza kuona na kujua wajibu wake katika sekta mbalimbali. Uwajibikaji na utawala bora waweza kudhihirika katika nyanja mbalimbali.
Uwajibikaji katika nyanja ya Afya.
Afya ni mojawapo ya sekta muhimu Katika jamii ambayo ni kiashiria kinachoonesha maendeleo yaliyopo ndani ya nchi. Maendeleo katika sekta ya Afya ndio huonesha utawala bora ndani ya nchi.
Sekta ya Afya ni kitengo muhimu ambacho kikifanyiwa uzembe Hali ya maendeleo itashuka au kuporomoka kwa kiwango kikubwa maana sehemu isiyokuwa na Afya nzuri huitaji gharama sana kutibu au kurekebisha. Sekta hii inategemea sana uwajibikaji na utawala bora, ambapo utawala bora utasaidia katika suala la ufatiliaji na utimizwaji wa Sheria bila ushurutishaji na kupelekea uwajibikaji Kati ya watu na viongozi wao bila kulazimishwa katika kutimiza majukumu au wajibu wao
Mfano kwa utawala bora wa Rais Mheshimiwa Mzee Benjamin Mkapa aliwezesha kukamilisha ujenzi wa hospitali katika mkoa wa dodoma iitwayo Benjamin Mkapa hospital (BMH),na pia katika utawala wa raisi Mheshimiwa Dkt John Magufuli alifanikisha ujenzi wa vituo mbalimbali vya Afya,mjini na vijijini,Hawa ni baadhi ya viongozi katika utawala wao.
Uwajibikaji ni njia ya kuandaa viongozi Bora na kujenga taifa
Viongozi na watendakazi wenye chachu ya maendeleo wenye tija ya kuliinua taifa katika hatua moja kwenda nyingine huanza kwa njia ya uwajibikaji.watu katika jamii inayotuzunguka hupenda kujifunza kutoka kwa watu wengine,ukiangalia saivi vijana wengi na watoto wamekuwa wakiwaangalia viongozi wa nchi Kama vioo au watu ambao Wana wahamasisha vijana na watoto kuwa Kama wao, kwa mfano mabinti wengi wameweza kujiamini na kujenga ujasiri ulio ndani yao kutokana na kuwepo kwa Rais mwanamke ndani ya nchi ya Tanzania ambaye ni Mheshimiwa, Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa akiongoza kwa utawala bora na uwajibikaji.hivyo basi viongozi wanapokuwa wawajibikaji ndivyo wanavyopandikiza mbegu ya utawala bora katika kizazi kilichopo na Cha baadae ambapo vizazi hivi vitapambana vikali dhidi ya matumizi mabaya ya uongozi.
suala ambalo hufanya au husababishwa kutokuwepo kwa uwajibikaji ni matumizi ya rushwa na uzembe walionao watekelezaji katika Hali ya kuachiana majukumu ambayo sio ya lazima kugawana na kupelekea uzembe,suala hili lisipo chukuliwa kwa umakini sio uzembe tu utakaoneka,pia utumiaji vibaya wa madaraka, huu hautaonekana Kama ni utawala bora bali Ila utaonesha kuwa Kuna uwepo wa watawala .
Hitimisho
Ubora katika kila sekta husababishwa na utawala bora na uwajibikaji walionao viongozi na ushirikiano wanaonesha kwa jamii inayowazunguka ambao huwapa mrejesho wa kuitikia wito katika masuala mbalimbali.ni jukumu la kila mmoja wetu kuwajibika na si kuwaachia viongozi maana ambapo hamna utekelezaji sisi ndio ambao huona kwanza kabla ya viongozi,yatupasa wote kujua Sheria za nchi na miongozo mbalimbali ili kujua haki na wajibu wa kila mwananchi.
Zifuatazo ni picha zinazoonesha uwajibikaji katika sekta ya Afya
1. Katika ufunguzi wa vituo vya Afya picha ya kulia ni picha inayoonesha ufunguzi wa kituo Cha Afya Cha Bwanga.
2. Uwajibikaji na utawala bora ,huandaa viongozi wa baadae( mtoto Georgina aketi katika kiti cha Raisi Dkt Samia Suluhu ,mtoto huyo an ndoto ya kuwa Rais skate) imetolewa na kitengo Cha habari leo.

Attachments
Upvote
1