Uwanja mkubwa wa mpira Chato wa nini?

Uwanja mkubwa wa mpira Chato wa nini?

Kamgomoli

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2018
Posts
1,896
Reaction score
4,058
Hesabu za wanasiasa huwa ni za kujua wao wenyewe tu. Hivi kweli Chato kunahitajika uwanja mkubwa wa mpira wa miguu kama wa Taifa (kwa Mkapa) wa kazi gani?

Kama huu mmoja Dar na uwingi wote wa watu tunashindwa kuujaza je Chato? Huu utakuwa ni upotevu mwingine wa fedha kama za ESCROW.

Sifa zikizidi haya ndo madhara yake. Nilitegemea uwanja kama huu ujengwe kwenye Majiji makubwa kama Mwanza, Mbeya, Arusha au Morogoro. Kiukweli kwa hili hata kama ndio charity begins at home, this is too much.

Mimi niko pamoja na mzee Meko na nakubali mambo mengi anayoyafanya ila kwa hili HAPANA. Hapa ndipo Kagame anapotupiga bao. Hesabu zake ni very strategic. Hakurupukagi. Mwezi uliopita tumeona Rwanda wakiufungua uwanja bora na wa kisasa kabisa maarufu kama Kigali Arena.

Sisi bado maamuzi yetu ni ya sifa sifa na mihemko. Kagame anaijenga Kigali inaonekana. Sisi hatueleweke mara, tujenge Arusha tunaacha tunahamia kuijenga Dodoma. Wakati huo huo Dar nayo inatakiwa ijengwe sasa tunahamia Chato.

Sisemi mikoa mingine isijengwe lakini kuna miradi ya kimkakati ambayo inahitaji kufikiri na kutafakari kwa kina. Yawezekana kwa sasa kipaumbele cha watu wa Chato ni hospitali ya kisasa au vyuo vya ufundi na si uwanja mkubwa kiasi hicho. Hakunaga mipango ya namna hiyo!

Nadhani Chato wanahitaji uwanja mdogo tu kama wa Azam Complex unawatosha.

Wahusika tafakarini. Kwa mipango yetu mibovu ndio maana hadi leo hii hatuna ukumbi wowote wa maana kwa ajili ya kuhost mikutano mikubwa, hatuna kumbi kubwa za kisasa za burudani. Na hakuna anayeona hilo.

Cheap political popularity inatugharimu sana tena sana.

download.jpeg
 
Mkuu, sisi hatushindani na Rwanda wala inchi yoyote.
Kama chato ipo ndani ya eneo ya United Republic of Tz kwani kuna tatizo gani mkuu??

Mbona SGR inajengwa From Dar to morogoro watu wa mtwara na Tanga hawajalalamika??

Binafsi sioni tatizo, maana kiwanja cha chato sio ndio kitakuwa cha mwisho kujèngwa... Mwanźa, Arusha, Mbeya, Kigoma vitajengwa tu mkuu, tujipe muda boss
 
Ndo yale yale ya kutaka kusikia kila kitu kinafanyika dar ndo mfurahi wacha Rais Magufuli afanye yake ilimradi hajavunja sheria maana huo uwanja unajengwa ndani ya Tanzania.
Na siku zote mwamba ngoma uvutia upande wake. Jiulize Uwanja wa Mpira wa Kaitaba, Bukoba una mkeka safi lakini Kaitaba haipo ndani ya jiji.

Je, ni majiji mangapi hapa Tanzania yana viwanja vya mpira lakini havina nyasi bandia? Nadhani utajua ni kwanini Kaitaba waliwekewa mkeka safi na hakuna mtu alielalamika maana alieshikilia mpini kwa wakati huo alikuwa anajulikana.
 
Shida wengi mnakimbilia kucoment bila kusoma. Sijasema Chato pasijengwe kiwanja,lakini kijengwe kiwanja chenye kuendana na idadi ya watu. Hilo li uwanja likubwa watu gani wataingia? Si bora vijengwe viwanja vidogo vidogo vingi katika mikoa tofauti yenye uhaba mkubwa wa viwanja? Simple logic.
 
Shida wengi mnakimbilia kucoment bila kusoma. Sijasema Chato pasijengwe kiwanja,lakini kijengwe kiwanja chenye kuendana na idadi ya watu. Hilo li uwanja likubwa watu gani wataingia? Si bora vijengwe viwanja vidogo vidogo vingi katika mikoa tofauti yenye uhaba mkubwa wa viwanja? Simple logic.

Kwamba wao hawana hamu ya kuwa na maendeleo ama? Hiyo ni logic simple tu imetumika apo. We unachotaka kufanya ni kukusanya uchumi sehem moja, which isn't okay at all. Lazma mechi zichezeke na huko Chato isogeze biashara zao pia.
 
Wewe acha ujinga economically kujenga uwanja mkubwa chato ni hakuna faida ni hasara tupu. Jamaa kaandika fresh uzi huu.

Economically kujenga kiwanja ni kusaidia chato kusogea: wale watu wa chato watapata pa kuuza endapo mechi zitakua zinachezeka apo: Tanzania Sio Dar tu, Raisi angekua ana mawazo kama yako ndo yale ya kenya nairobi uchumi mkubwa wakati turkana watu mil 1 wamekufa kwa njaa: Tunashukuru raisi hana akili kama yako
 
Katika suala la michezo siwezi kuongea kisiasa.

Hili la ujenzi wa uwanja nimelibariki kwa baraka zote maana kila mtu atakuwa na haki ya kutumia uwanja ule na mechi za kimataifa zitaenda pale.

Uwanja wa michezo kwangu mimi naona ni zaidi ya Ndege.
 
Kamgomoli,

Uwanja wa Mpira haujengwi kwa Kigezo cha eneo husika kuwa mbali au kwamba halina Watu wengi au halina Michezo.

Ujenzi wa Uwanja unaweza ukawa ndiyo chachu kubwa ya muamko wa Kimichezo katika eneo husika lakini pia Ujenzi wa huo huo Uwanja unaweza pia kuwa ni Chanzo cha Mapato kwa Halmashauri na Serikali husika ya Mkoa.

Kama haitoshi Uwanja huo huo mkubwa wa hapo unaweza kuwa ni Chanzo cha Kiuchumi hasa kwa Wakazi kwani wanaweza wakawa wanauza bidhaa zao pale Michuano ikiwa inachezwa hapo.

Baada ya Ujenzi wa Uwanja huo wenye Mamlaka nao wanaweza wakawa wanautumia kwa Kuukodisha kwa Timu Kubwa Kubwa nchini au hata wakawa Wanaandaa Mashindano ambayo yatazikutanisha hizi Klabu Kubwa hivyo Mapato Kuongezeka lakini hata na Hamasa ya Kimpira na Kimichezo eneo husika nayo ikaongezeka.

Na Viwanja havijengwi kwa matumizi tu ya sasa basi Viwanja vinajengwa hata kwa matumizi ya baadae na kwa Vizazi vijavyo.

Na Kinachofanya Uwanja Kujaa siyo Watu (Wakazi) husika wa hapo bali ni ' Hamasa ' na ' Mwamko ' unaojengwa na Wahusika wa Kimichezo kutokana na Mipango yao waliyonayo katika Kuendeleza Mchezo wa Mpira wa Miguu hapo.

Na hakuna mahala popote pale nchini Tanzania pameandikwa kwamba ndiyo pawe na Uwanja wa Mpira na pengine pasiwepo.

Umeleta Mada hii Kiuanaharakati / Kisiasa zaidi kwakuwa tu una Chuki zako na Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli kwa kuwa nae anatokea hilo eneo la Chato na huenda pia na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Na hii Serikali nina uhakika Uwanja huu huu ungesikia Unajengwa eneo jingine wala usingekuja na haya ' Majungu ' yako. Kwani sehemu atokayo Rais ikiwa na Maendeleo ni Kosa au Dhambi?
 
Kuna Watu ni ' Mapopoma ' hapa duniani hadi najiuliza ni kwanini hata Mwenyezi Mungu alipoteza muda wake muhimu Kuwaumbeni. Uwanja wa Mpira haujengwi kwa Kigezo cha eneo husika kuwa mbali au kwamba halina Watu wengi au halina Michezo. Ujenzi wa Uwanja unaweza ukawa sasa ndiyo chachu kubwa ya muamko wa Kimichezo katika eneo husika lakini pia Ujenzi wa huo huo Uwanja unaweza pia kuwa ni Chanzo cha Mapato kwa Halmashauri na Serikali husika ya Mkoa. Kama haitoshi Uwanja huo huo mkubwa wa hapo unaweza kuwa ni Chanzo cha Kiuchumi hasa kwa Wakazi kwani wanaweza wakawa wanauza bidhaa zao pale Michuano ikiwa inachezwa hapo. Baada ya Ujenzi wa huo Uwanja wenye Mamlaka nao wanaweza wakawa wanautumia kwa Kuukodisha kwa Timu Kubwa Kubwa nchini au hata wakawa Wanaandaa Mashindano ambayo yatazikutanisha hizi Klabu Kubwa hivyo Mapato Kuongezeka lakini hata na Hamasa ya Kimpira na Kimichezo eneo husika nayo ikaongezeka. Na Viwanja havijengwi kwa matumizi tu ya sasa basi Viwanja vinajengwa hata kwa matumizi ya baadae na kwa Vizazi vijavyo. Na Kinachofanya Uwanja Kujaa siyo Watu ( Wakazi ) husika wa hapo bali ni ' Hamasa ' na ' Mwamko ' unaojengwa na Wahusika wa Kimichezo kutokana na Mipango yao waliyonayo katika Kuendeleza Mchezo wa Mpira wa Miguu hapo. Na hakuna mahala popote pale nchini Tanzania pameandikwa kwamba ndiyo pawe na Uwanja wa Mpira na pengine pasiwepo. Umeleta Mada hii Kiuanaharakati / Kisiasa zaidi kwakuwa tu una Chuki zako na Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli kwa kuwa nae anatokea hilo eneo la Chato na huenda pia na Chama Cha Mapinduzi ( CCM ) na hii Serikali ila nina uhakika Uwanja huu huu ungesikia Unajengwa eneo jingine wala usingekuja na haya ' Majungu ' yako. Kwani sehemu atokayo Rais ikiwa na Maendeleo ni Kosa au Dhambi? Mnafiki na Mshamba mkubwa Wewe!
Najiuliza tu,
1. Waliofanya uamuzi wa kujenga uwanja mkubwa Chato walizingatia vigezo gani? Yaani kwanini Chato na si sehemu nyingine tu?
2. Isingekuwa mkulu hatoki Chato bado wangefikiria kufanya uamuzi huo?
 
Shida wengi mnakimbilia kucoment bila kusoma. Sijasema Chato pasijengwe kiwanja,lakini kijengwe kiwanja chenye kuendana na idadi ya watu. Hilo li uwanja likubwa watu gani wataingia? Si bora vijengwe viwanja vidogo vidogo vingi katika mikoa tofauti yenye uhaba mkubwa wa viwanja? Simple logic.
nchi inakua hii mkuu, idadi ya watu pia inaongezeka kwa kasi (hasa kanda ya ziwa) watu wanazaa sana, sasa unaposema vijengwe viwanja vidogo vidogo, vipi miaka ijayo?
sisi tumeweka malengo ya miaka ijayo.
 
Tunataka Rais wetu awe anacheza mpira kama Pierre Nkurunzinza.
Halafu Chato ni lazima kupewe kipaumbele kuliko sehemu nyingine yoyote, Chato ni ardhi takatifu
Aisee ni Israel inchi ya ahadi
 
Back
Top Bottom