Kamgomoli
JF-Expert Member
- May 3, 2018
- 1,896
- 4,058
Hesabu za wanasiasa huwa ni za kujua wao wenyewe tu. Hivi kweli Chato kunahitajika uwanja mkubwa wa mpira wa miguu kama wa Taifa (kwa Mkapa) wa kazi gani?
Kama huu mmoja Dar na uwingi wote wa watu tunashindwa kuujaza je Chato? Huu utakuwa ni upotevu mwingine wa fedha kama za ESCROW.
Sifa zikizidi haya ndo madhara yake. Nilitegemea uwanja kama huu ujengwe kwenye Majiji makubwa kama Mwanza, Mbeya, Arusha au Morogoro. Kiukweli kwa hili hata kama ndio charity begins at home, this is too much.
Mimi niko pamoja na mzee Meko na nakubali mambo mengi anayoyafanya ila kwa hili HAPANA. Hapa ndipo Kagame anapotupiga bao. Hesabu zake ni very strategic. Hakurupukagi. Mwezi uliopita tumeona Rwanda wakiufungua uwanja bora na wa kisasa kabisa maarufu kama Kigali Arena.
Sisi bado maamuzi yetu ni ya sifa sifa na mihemko. Kagame anaijenga Kigali inaonekana. Sisi hatueleweke mara, tujenge Arusha tunaacha tunahamia kuijenga Dodoma. Wakati huo huo Dar nayo inatakiwa ijengwe sasa tunahamia Chato.
Sisemi mikoa mingine isijengwe lakini kuna miradi ya kimkakati ambayo inahitaji kufikiri na kutafakari kwa kina. Yawezekana kwa sasa kipaumbele cha watu wa Chato ni hospitali ya kisasa au vyuo vya ufundi na si uwanja mkubwa kiasi hicho. Hakunaga mipango ya namna hiyo!
Nadhani Chato wanahitaji uwanja mdogo tu kama wa Azam Complex unawatosha.
Wahusika tafakarini. Kwa mipango yetu mibovu ndio maana hadi leo hii hatuna ukumbi wowote wa maana kwa ajili ya kuhost mikutano mikubwa, hatuna kumbi kubwa za kisasa za burudani. Na hakuna anayeona hilo.
Cheap political popularity inatugharimu sana tena sana.