KERO Uwanja wa Mkapa unatia aibu, nani awajibike?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Lisu anasema ni kwa sababu ya Katiba tuliyonayo
 
Ule uwanja wangetoa kandarasi watu washindane kwenye tenda ya kuuendesha watu binafsi.
Sisi nchi hii tunaweza mizagamuano pekee huko ndiyo tunafanya vizuri sana nami nikiwamo.
 
Hizi timu kongwe zilitakiwe zipewe hata miaka 5, ziwe zimejenga viwanja vyao.

Wee uwanja kila wiki mechi mbili, unategmea nini hapo. Hata ukitunzaje lazima utazidiwa.
Sidhani kama shida ni mara ngapi unatumika. Taratibu za kuumwagilia inavyotakiwa hazifuatwi. Leo nilivyofungua channel sikudhani kama ni taifa. Na hadi kushindwa kusafisha vyoo utasemaje?

Labda uniambie matumizi yasiyo ya michezo yapungue au yazuiwe kabisa maana nadhani juzi tu hapa kulikuwa na tamasha pale inawezekana ndiyo limeharibu uwanja.
 
Uwanja ulitakiwa uwe na hadi speakers kutoa matangazo mbalimbali na hata kuhamasisha mashabiki wa timu mwenyeji kwa kupitia nyimbo
 
Uwanja unatia aibu sana sana! Hebu kumbuka siku tulipokabidhiwa tunapaita kwa mchina na leo? Sisi tuna matatizo mazito [emoji31]

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Nina uhakika Uwanja wa Taifa una meneja wake na chini yake ana supervisors wake wa kusimamia usafi na matunzo ya kiwanja, na huyo meneja ana mwajiri wake, tuanze na huyo meneja na bodi au mwajiri wake amwajibishe, hii kitu rahisi sana tusiende mbali, aliyemwajiri meneja wa kusimamia usafi afanye kazi yake...FUKUZA MENEJA WA UWANJA WA TAIFA FULLSTOP!!!!
 
Kwa akili yako mbovu,kwa vile uwanja ni mmoja,ndio uharibiwe?

Halafu una maana gani ukisema uwanja ni mmoja?Husifu hata jitihada za hii serikali kwamba sasa Namungo,Kagera,Dodoma soka linachezwa muda wowote?

Acha ujinga na wewe uliwahi kuwa kiongozi wa hii hii serikali

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Kuhusu elimu wala usiwe na hofu,maana ndiyo kigezo cha kuajiri watu kwa sasa.

Lakini elimu haina lolote iwapo mtu hana akili.

Wengi mnachanganya akili na elimu.Ni vitu viwili tofauti sana.
Unaweza kuwa na vyeti lakini ukawa huna akili.Ni jambo la kawaida tu

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Ili kubaini mtu anayeshindwa kuungalia huo uwanja, inabidi tujue kwanza mapato yanaingia wapi!,

Kwamba, mapato ya uwanja huwa yanaingia kwenye akaunti ya uwanja na meneja anapanga matumizi au mapato yanalipwa kwa control namba yanaenda serikali kuu halafu ndio serikali inarudisha bajeti ya uwanja kwa ajili ya matunzo?

Mzembe ni nani kati ya meneja wa uwanja, wizara, baraza la michezo, au ni nani?

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Hatari sana hii, wakati tunakabidhiwa huu uwanja kulikua na garden nzuri sana nje, kiukweli ulikua unavutia sana! Baada ya miezi miwili garden ikawa imekauka, then baadae ikawa wiki kwenye vifaa vya vyooni na uharibifu uliokithiri hakuna aliyejali! Sasa ndio tunaelekea kwenye pitch yenyewe nayo itafikia wakati itakua kama ya Jamhuri Morogoro tu! Mwenyezi Mungu atasaidie sisi baadhi ya Waafrika ili tuweze kusimamia rasilimali zetu vizuri hatuna yeyote atakayesimamia ni sisi wenyewe!!
 
Sijui huyo meneja wa uwanja, na viwanja vingine vingi mikoani huwa wanalipwa mishahara kwa kazi gani wanayofanya?

Najua, wengi wao huwa wana mambo mengine nje ya hizo kazi, ndio maana ufuatiliaji wa karibu kwao unakuwa mdogo sana.

Hii nchi tunajiendea tu, kuna zile nyasi bandia, tangu Samia aseme anataka kuona viwanja vyetu vikiwekwa nyasi zile, mpaka leo kimya, hakuna muendelezo wowote wa lile suala, mpaka siku Rais akumbushe tena ndio wahusika washtuke usingizini!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…