Kuna ile screen huwa iko off muda wote, halfu kuna mwamba (manager) wa ule uwanja yupo tu, anakula salary.
Sijui hizi kazi huwa wanapeana vipi, inafaa ifike wakati tuhoji,
Yaani tufahamu hii management ya huu uwanja, tuone elimu zao, kisha tuone walipataje hizi nafasi. Kuna haja.
Suala SIO Elimu mkuu. Achana na watu wanaoitwa wasomi . Hao ndio wezi wabaya sana. Wasomi wasipodhibitiwa Hawana aibu kabisa . Ni watu Wa hovyo kabisa wanapoona Kuna mitandao ya Wizi. Wasomi wanajua mbinu zote za Wizi. Siku Hizi Wana mpama magrupu ya kupeana mbinu za Wizi na Namna ya kulimbikiza Mali ndani na NJE ya nchi.
Msomi anatishwa na serikali yenye meno tuu Kwa sababu wasomi ni waoga Wa kufungwa au kunyongwa.Wasomi wanaogopa kupoteza au kuteswa. Wasomi wanapoona Kuna Rais mkali na wanakoromewa wanakaa kwenye Mstari ndio Maana miaka mitatu iliyopita wasomi waliokua wanakusanya mapato kwenye NHC ,Tanesco na mabenki kama NMB na CRDB na TTCL ,Airtel na Posta Kisha kugawa gawio Kwa serikali leo wanapiga pesa za faida na kujilipa pisho za Sikukuu na kutengeneza vipepereshi Kisha kusema hakuna faida wapewe ruzuku na Kwa sababu ni wataalam Wa kudanganya kisomi na kimikakati wanapewa ruzuku wanaendelea Kupiga wakiambiwa basi waachieni watu Binafsi wanaleta tena sababu za kisomi Huku serikali ikizidi kupata hasara na Wao wakizidi kujenga majumba na kusomesha watoto Wao mashule ya gharama kubwa NDANI na NJE ya nchi.
Wanaopewa Tenda Tote za kukusanya mapato au Ushuru na kusimamia maeneo kama viwanja vya mpira ,stendí za mabasi, masoko,kandarasi za kujenga madaraja na barabari vijijini na Hata mijini ,mabasi ya mwendo Kasi ama ni wasomi au Nyuma ya Tenda hizo kuna wasomi walioko madarakani. Suala Hapo SIO uwezo Wa kusimamia mapato ya nchi Bali Suala ni uwezi Wa KUFANYA ujanja ujanja Wa kukwapua pesa za umma na Kwenda kugawana. Kwa hiyo asiyeweza kuiba na kuwapelekea wakubwa waliompa Tenda pesa za Asante ajue hawezi kupata tenda Sehemu nyingine.
Jiulize ni mwaka Wa 62 Tangu Tupate uhuru lakini mdudu anayeitwa Mbu ameshindikana kumalizwa na Wataalamu wanaogharamikiwa mabilioni ya pesa za Mikopo Huku Mbu Hao Wakiwa wanaomaliza maelfu ya watu Kila Siku.Yani Mbu binadam msomi ameshindwa kumaliza Mbu wakati Mbu anawamaliza bindam na dawa ya kumaliza ni ndogo tu na kuna nchi walitokomeza Mbu zamani sana.
TATIZO ni nini ?
Kuna kitu kinaitwa Mradi Wa malaria ambao umekua ni Biashara kubwa Kati ya wasomi wanaosimamia na Wazungu wanaofanya na Kugharamikia utafiti Wa kujua Tabia na mabadiliko ya Mbu na mazingira yake na jinsi malaria inavyoweza kuwa Biashara kubwa ya kuimarisha viwanda vya kutengeneza dawa na kuuzia serikali.
Wasomi wanafurahia uwepo Wa malaria mana wanapigwa pesa za utafiti na Kisha Kwenda kujilimbikizia Mali au kujenga mahospitali Yao .
Kwa Hali hiyo hakuna kitakachofanywa na Wasomi kwanye nchi zetu maskini kama hakuna mkono Wa chuma Wa kuwaambia "nyie wasomi tumewasomesha Kwa pesa zetu na tunawategemea hivyo ninawapa Miezi Sita muhakikisha mnakuja na Suluhu ya kumaliza Mbu WOTE na mazalia yake Ili serikali iachane na Suala la KUTUMIA mabilioni ya pesa Kila mwaka kwenye miradi ya Malaria na kutibu Malaria isiyoisha " na mkishindwa kamwe hampati Tenda na mradi Wowote Wa malaria na ikiwezekana nawatimua kwanye seikali yangu Ili wakafanye madili Yao NJE ya serikali."
Wasomi ukiwachimba mkwala kama huo hakina nakuambia Leo hii Suala la Mbu na malaria limgekua historia.