KERO Uwanja wa Mkapa unatia aibu, nani awajibike?

KERO Uwanja wa Mkapa unatia aibu, nani awajibike?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Naona huu mjadala umeanza kushika kasi. Inasemekana kwenye bajeti iliyopita zilitengwa fedha kwaajii ya ukarabati wa viwanja vitano lakini hakuna kilichofanyika hadi leo kwa mujibu wa Jemedari.

Tuendelee kusema!

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Kwa hiyo mbwaduke achambue mpaka kiwanja?

Anyway lawama ni muhimu, pitch ina muonekano wa hovyo.
Ndio! Inawahusu hiyo. Kama wanachambua hadi academies za watoto,kwanini isiwe viwanja? Watoto hujifunzia wapi?
Baadhi ni waandishi pia, kalamu zao zinafanya nini?
 
Wakuu,

Hivi kweli tumeshindwa kutunza huu uwanja? Usafi wa vyoo na maeneo mengine imekuwa tatizo sugu lakini aibu kubwa zaidi ni sasa hata pitch imetushinda.

Ni aibu National Stadium nyasi kuisha na kuwa na mapengo ya vumbi. Serikali kwenye hili mnastahili lawama zote kwa kushindwa kusimamia huu uwanja.

Hii nchi kwenye mpira tunachambua mambo mengi ya kijinga na wakati mwingine kuacha vitu fundamental.

Uwanja wa Taifa kuwa na pitch ya namna ile ni aibu ya Taifa. Watu wawajibike kwenye hili! Aibu! Aibu! Aibu!

Shame on us! [emoji35]

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
Kile kisa cha nabii aliyelewa na kukaa uchi akiwa na watoto wake watatu wazungu hukitumia kutaja asili ya rangi za binadamu kinanijiaga— kinauma lakini kama kweli vile?

Wanadai sisi babu yetu ni yule aliyemcheka mzee wakati mwingine hakucheka na yule watatu alimfunika mzee. Babu yetu waafrika alilaaniwa yeye na kizazi chake.

🇹🇿🇹🇿😇😇😭😭😭🇹🇿🇹🇿
 
Hizi timu kongwe zilitakiwe zipewe hata miaka 5, ziwe zimejenga viwanja vyao.

Wee uwanja kila wiki mechi mbili, unategmea nini hapo. Hata ukitunzaje lazima utazidiwa.
Hoja sio kuchezewa mechi mbili kwa wiki mbona misimu ya nyuma zilikua zinachezwa na hatukuona haya yanayotokea leo??ishu ni utunzaji..pesa zinaenda wapi?
 
Tunaenda kwenye Mashindano ya CAF Sasa hivi,wahusika wajitahidi kukarabati Uwanja mapema.
 
Na yale matamasha yao ya Dini wanayapeleka pale, wanategemea nini kama siyo uharibifu wa uwanja.

Ustaarabu hakuna ukiingia kwenye vyoo ndiyo balaa.
 
Kama tunakosa akili ya ku manage uwanja tutaweza hayo mandoto tunayoota? Vitu vidogo sana tunafeli. Hivi tumeshindwa kutunza walau, walau, walau eneo la kuchezea?

Aliyeturoga kafa!

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
Sijui SGR itakuwaje? naona tumlipe CEO mzungu tuu mwenye uzoefu na mambo ya reli aje aiendeshe, sina imani kama kina Kadogosa wataweza kuisimamia
 
Na yale matamasha yao ya Dini wanayapeleka pale, wanategemea nini kama siyo uharibifu wa uwanja.

Ustaarabu hakuna ukiingia kwenye vyoo ndiyo balaa.
Matamasha hayana shida na wanalipa kutumia uwanja, focus na issue uwanja hautunzwi unavyotakiwa na wanakusanya mabilioni lakini hata taa au kusafisha vyoo hawawezi, mimi ningeanza na msimamzi mkuu wa uwanja then meneja wa usafi na mazingira ya uwanja, ningesafisha wote hao bila chenga
 
Tuna Waziri Mzuri sana wa Michezo Mhe.Mchengerwa naimani watalishughulikia hilo jambo Kwa haraka...Kikubwa Taarifa imefikie na naimani wahusika watakuwa washaona Hali ya Uwanja ilivyo.
 
Boss uwanja ni mmoja, kuna timu kongwe zina miaka zaidi ya 80 hazina viwanja, zote zinatumia uwanja huohuo kama uwanja wa nyumbani, (Overuse) ,

Kumbuka kuna timu ndogo tu zinaanzishwa na tayari zina viwanja vyao na kumbuka kuna ile takataka inaitwa tff huwa inavifungia viwanja vyao wakati wowote (hasa pale hizi timu ndogo mpya zinaposhindwa kujiongeza [emoji383])

Nchi nzima tuna kiwanja kimoja,

Serikali hii ya hovyo bado haijaona umuhimu wa kujenga viwanja vingine hata viwili vyenye capacity ya 20-30k dodoma au moro au Arusha na dsm licha ya kukopa mabilioni ya pesa ulaya.
AC Milan na Inter Milan ni kongwe kuliko Simba na Yanga lakini hazina uwanja zinatumia uwanja wa umma wa Sansiro au Guissepe Meaza
 
Ni wakati serikali kunifunza.viwanja vikubwa havina maana tena, maana kuvijaza ni ngumu sana.

Ule uwanja unahitaji mapato ili ujiendeshe, mapato yenyewe yanategemea Simba na Yanga.

Viwanja vya Serikali vitaendelea kuwa vibovu.

Walivyo wapumbavu, wanajenga kiwanja kikubwa Dodoma hapo ndio watashangaa
 
Kiwanja kina chezewa siku tatu mfululuzo bila mapumziko mpaka nyasi zimeondoka uwanja umekuwa kipara kabisa

Sent from my SM-N950F using JamiiForums mobile app
 
Tunaambiwa CAF wametaka marekebisho kwenye pitch ili ufae kutumika kwenye Super league! Hivyo uwanja unalazimika kufungwa kwanza kupisha marekebisho.

Kama tungekuwa na mpango mzuri tusingefika huku.Huu ndio uwanja pekee unaokubalika na CAF kwasasa. Lipo tatizo mahala

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Kuna ile screen huwa iko off muda wote, halfu kuna mwamba (manager) wa ule uwanja yupo tu, anakula salary.
Sijui hizi kazi huwa wanapeana vipi, inafaa ifike wakati tuhoji,
Yaani tufahamu hii management ya huu uwanja, tuone elimu zao, kisha tuone walipataje hizi nafasi. Kuna haja.
Kazi walipata kwa connection kupitia vimemo.
 
Niliiona hili kwenye mechi hizi Mbili za kimataifa uwanja udongo mwekundu unaonekana
 
Back
Top Bottom