KERO Uwanja wa Mkapa unatia aibu, nani awajibike?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Ilikuwa garden kali sana! Palivyo siku hizi pale ni aibu tu

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Aibu pia iende kwa simba na yanga mpaka leo hawana viwanja wanatumia wa mkapa tu ni aibu
 
Ni aibu National Stadium nyasi kuisha na kuwa na mapengo ya vumbi. Serikali kwenye hili mnastahili lawama zote kwa kushindwa kusimamia huu uwanja.
Unauliza swali wakat jibu unalo. Wewe jamaa vipi!
 
Ac Milan na Inter Milan wote wanatumia uwanja mmoja miaka kwa miaka je umeshaona ubora wa ule uwanja umetetereka kama wetu?Tena wenzetu wana mashindano mengi kuliko sisi........suala la overuse sio kweli.....tatizo utunzaji umetushinda tu ndio umetushinda.
 
Soma Isaya 50:11.
Laana ya kukimbiza ni kulala kwa huzuni. Utafanya jambo litakuwa zuri kwa muda mfupi tu kisha litaharibika. Kila ukifanyalo kitaharibika
 
Hilo la Vyoo yaan ni kero, taa za kawaida hasa maeneo ya nje wa uwanja hasa upande ule wa Mgulani. Yaan tuko hovyo sana.
 
Tff wanachoweza ni kuwashonea yale masuti wale ma mechi commissioners
 
Suala SIO Elimu mkuu. Achana na watu wanaoitwa wasomi . Hao ndio wezi wabaya sana. Wasomi wasipodhibitiwa Hawana aibu kabisa . Ni watu Wa hovyo kabisa wanapoona Kuna mitandao ya Wizi. Wasomi wanajua mbinu zote za Wizi. Siku Hizi Wana mpama magrupu ya kupeana mbinu za Wizi na Namna ya kulimbikiza Mali ndani na NJE ya nchi.

Msomi anatishwa na serikali yenye meno tuu Kwa sababu wasomi ni waoga Wa kufungwa au kunyongwa.Wasomi wanaogopa kupoteza au kuteswa. Wasomi wanapoona Kuna Rais mkali na wanakoromewa wanakaa kwenye Mstari ndio Maana miaka mitatu iliyopita wasomi waliokua wanakusanya mapato kwenye NHC ,Tanesco na mabenki kama NMB na CRDB na TTCL ,Airtel na Posta Kisha kugawa gawio Kwa serikali leo wanapiga pesa za faida na kujilipa pisho za Sikukuu na kutengeneza vipepereshi Kisha kusema hakuna faida wapewe ruzuku na Kwa sababu ni wataalam Wa kudanganya kisomi na kimikakati wanapewa ruzuku wanaendelea Kupiga wakiambiwa basi waachieni watu Binafsi wanaleta tena sababu za kisomi Huku serikali ikizidi kupata hasara na Wao wakizidi kujenga majumba na kusomesha watoto Wao mashule ya gharama kubwa NDANI na NJE ya nchi.

Wanaopewa Tenda Tote za kukusanya mapato au Ushuru na kusimamia maeneo kama viwanja vya mpira ,stendí za mabasi, masoko,kandarasi za kujenga madaraja na barabari vijijini na Hata mijini ,mabasi ya mwendo Kasi ama ni wasomi au Nyuma ya Tenda hizo kuna wasomi walioko madarakani. Suala Hapo SIO uwezo Wa kusimamia mapato ya nchi Bali Suala ni uwezi Wa KUFANYA ujanja ujanja Wa kukwapua pesa za umma na Kwenda kugawana. Kwa hiyo asiyeweza kuiba na kuwapelekea wakubwa waliompa Tenda pesa za Asante ajue hawezi kupata tenda Sehemu nyingine.

Jiulize ni mwaka Wa 62 Tangu Tupate uhuru lakini mdudu anayeitwa Mbu ameshindikana kumalizwa na Wataalamu wanaogharamikiwa mabilioni ya pesa za Mikopo Huku Mbu Hao Wakiwa wanaomaliza maelfu ya watu Kila Siku.Yani Mbu binadam msomi ameshindwa kumaliza Mbu wakati Mbu anawamaliza bindam na dawa ya kumaliza ni ndogo tu na kuna nchi walitokomeza Mbu zamani sana.
TATIZO ni nini ?
Kuna kitu kinaitwa Mradi Wa malaria ambao umekua ni Biashara kubwa Kati ya wasomi wanaosimamia na Wazungu wanaofanya na Kugharamikia utafiti Wa kujua Tabia na mabadiliko ya Mbu na mazingira yake na jinsi malaria inavyoweza kuwa Biashara kubwa ya kuimarisha viwanda vya kutengeneza dawa na kuuzia serikali.
Wasomi wanafurahia uwepo Wa malaria mana wanapigwa pesa za utafiti na Kisha Kwenda kujilimbikizia Mali au kujenga mahospitali Yao .
Kwa Hali hiyo hakuna kitakachofanywa na Wasomi kwanye nchi zetu maskini kama hakuna mkono Wa chuma Wa kuwaambia "nyie wasomi tumewasomesha Kwa pesa zetu na tunawategemea hivyo ninawapa Miezi Sita muhakikisha mnakuja na Suluhu ya kumaliza Mbu WOTE na mazalia yake Ili serikali iachane na Suala la KUTUMIA mabilioni ya pesa Kila mwaka kwenye miradi ya Malaria na kutibu Malaria isiyoisha " na mkishindwa kamwe hampati Tenda na mradi Wowote Wa malaria na ikiwezekana nawatimua kwanye seikali yangu Ili wakafanye madili Yao NJE ya serikali."
Wasomi ukiwachimba mkwala kama huo hakina nakuambia Leo hii Suala la Mbu na malaria limgekua historia.
 
Then utashangaa kwanini watu wa nje wanatudharau waafrika, tunashindwa kuwa wastarabu kabisa kwa ujinga wetu.
 
Ile mistari kwenye pitch imepauka haiionekani vizuri.

Sijui ni nani mtunzaji wa huo uwanja.

Akakula mapato tu kazi Hana.
Meneja wa uwanja si yupo, huo uwanja ulitakiwa ukabidhiwe chini ya JKT
 
Tanzania kuna viwanja vingi sana kuliko nchi yoyote ya East Afrika Nyerere alijenga kila mkoa viwanjwa kama hujawai kutembelea kila mkoa nenda katembelee, atakama Serikali ikivikarabati viwanja vyote vikawa vizuri itakuwa kazi bure kama hicho cha Mkapa, Waziri anateua tu Meneja wa uwanja bila kuzingatia taaluma siyo mtu yoyote anaweza kuwa Meneja wa uwanja.
 
Tumpate Raisi tumbua tumbua tena wanyooke awa kenge
 
Hizi timu kongwe zilitakiwe zipewe hata miaka 5, ziwe zimejenga viwanja vyao.

Wee uwanja kila wiki mechi mbili, unategmea nini hapo. Hata ukitunzaje lazima utazidiwa.
Kwani Etihad wao kila wiki una chezewa mechi ngapi? au Emirate, Banabeu?
 
Viwanja Dar vipo zaidi ya vitatu(3). Sijui kwanini wanautumia uwanja wa Mkapa kila wiki.
Kuna uwanja wa uhuru na Azam. Huo uwanja wa Mkapa hata haujazi kwa 10% mechi nyingi tu.
Sasa huko si kupoteza resources?
 
Si walibadilishaga boss wa uwanja wakaweka mwingine, imekuaje naye hatimizi majukumu yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…