Uwanja wa Mpira Dodoma umeyeyuka? Hayati Magufuli angekuwepo ingekuwaje?

Uwanja wa Mpira Dodoma umeyeyuka? Hayati Magufuli angekuwepo ingekuwaje?

Uwanja wao wenyewe wa Mohammed V haufikii huo. Halafu uwanja wa mpira hakitakiwi kuwa kipaumbele huko Dodoma kwa sasa bali miundombinu ya kisasa kuwezesha serikali ifanye kazi kwa ufanisi.
Wakati wa JPM kuna jambo lilikuwa linasuasua hapo Dodoma?

Uwanja wa Mpira ni mhimu mno hasa kipindi hiki ambacho Yanga inachanaj mbuga.
 
Wakati wa JPM kuna jambo lilikuwa linasuasua hapo Dodoma?

Uwanja wa Mpira ni mhimu mno hasa kipindi hiki ambacho Yanga inachanaj mbuga.
Kwa sasa uwanja wa Jamhuri unajitosheleza. Serikali ijenge mifumo imara ya mawasiliano na TEHAMA kuepusha watu kuhitaji kwenda Dodoma kufuata huduma za serikali.

Haya mambo ya kuanzisha miradi mikubwa halafu "wateja" wakubwa wakiwa ni watumishi wa serikali ni matumizi mabaya ya rasilimali za nchi. Walianza na kutuzoesha magari ya kifahari, zikaja ndege za ATCL, sasa hivi reli mpya eti ili watumishi wawe wanakwenda Dar weekend, na huu uwanja yote ni ubinafsi tu.
 
Una toja gani? Usha wahi kuwaza Serikali iingile kato kutoa mikopo kwa Graduatevwalio jazana mitaani? Akili za ajabu sana hizi, Impact ya huo uwanja ni ipi kwa uchumi wa nchi?
Kwa uandishi wa aina hii nastahili kujibizana na wewe kweli?
 
Mfalme wa Morocco alitoa mpunga wa kajengea uwanja dhalim akajengea mahoteli kule kijijini kwake.
 
Angalia hii Picha afu nambie iwapo mwamba angekuwa hai Dodoma pangekuwa pamefikia hatua gani?

Ujenzi huu ulitakiwa Kuanzia mara baada tu ya Ujenzi w msikiti wa BAKWATA pale Kinondoni. Mfadhiri alishaahidi kutoa pesa.. mfalume wa Morocco.

Ushauri wangu kwa Ikulu; Fuatilieni hii ahadi.

View attachment 2630021
Ombi lilimzidi uwezo, kwa hiyo mfalme akajikuta akikubali tu kwa kutoa jibu la kimtindo bila ya yeye kuridhia kutoka moyoni mwake. Kuwa ombaomba ni gharama, kwani mtu maskini huishia kusema ahadi ni deni. Nchi kama inakopa kila siku, inashindwa nini kufanya hivyo kwa ajili ya ujenzi wa uwanja huo!?

Serikali ya CCM imezoea vya kunyonga, vya kuchinja itaviiwezea wapi? Yaani viwanja vingi vilivyojengwa na nguvu ya wananchi imejimilikisha yenyewe, halafu inataka vingine wajengewe na Waafrika wenzao kutoka nchi nyingine!?

Suala ni dogo tu! Rudisha viwanja vyote viwe chini ya halmashauri ndipo bajeti itengwe ili miundombinu iboreshwe na viwe vya kisasa zaidi. Tamaa ilimponza fisi, kisa tu kupenda vya kudoea.
 
Kamfufue aje kujenga..... huo uwanja uliahidiwa tangia 2016 lakini kwa miaka yote haikujengwa mpaka Magufuli anakufa mwaka 2021 na ukaona ni sawa, leo hii ndio unakumbuka kuhoji
Msukule wa Chato
Nchi ina watu wajinga sana. Wengi wanasumbuliwa na ujinga wa kihalaiki.walijingishwa vibaya sana. Kumne kweli yule ngosha angetaka angetawala zaidi ya miaka 10 sema kabetri kalizima ghafulaq. Ahahahaha
 
Yule Mfalme Ni Janjajanja Nyingi Tu, Hakutoa Cash Yoyote
Alichotoa Ni Ile Cash Ya Msikiti Pale Kinondoni Nayo Pia Ndani Ina Ukakasi Kidogo
Ulishawahi kuiona bajeti ya miradi ya chato? Au japo kusikia tenda za zabuni zikitangazwa?
 
Uwekezaji wa majengo Dodoma ni upotevu wa pesa
Dodoma haina mashabiki wa kujaza uwanja

Hata Airport ya Msalato uhakika wa kufuga popo ni mkubwa sana.

Kama JNIA yenyewe haijafikisha 4mil pax ndio Dodoma itaweza? Ambapo hakuna wafanyabiashara wa maana?

Hizo pesa serikali isomeshe walimu upya ili elimu isije tuletea Nigeria mpya
 
Nchi ina watu wajinga sana. Wengi wanasumbuliwa na ujinga wa kihalaiki.walijingishwa vibaya sana. Kumne kweli yule ngosha angetaka angetawala zaidi ya miaka 10 sema kabetri kalizima ghafulaq. Ahahahaha
Kuwaza ruksa.
 
Angekuwepo angepiga 1.5T nyingine ,angekuwepo watu wangeendelea kutekwa,angekuwepo matajiri wote wangekuwa washafilisika,angekuwepo wamachinga wangekuwa wanaendelea kufanya biashara katikati ya barabara!

Ikulu ya Dodoma imekamilika kwani alikuwepo wakati inajengwa?
 
Kwani mpaka useme flani angekuwepo. Hivi mlilogwa na nani Watanzania au huyo unaemsema yeye alikuwa na utofauti gani na wanadamu wengine. Kwani wewe unashindwa nini kufuatilia hizo pesa Uarabuni uje ujenge huo uwanja au na wewe umeshakufa. Kuamini kwamba bila mtu flani huwezi lolote ni uzwazwa wa kumuabudu binadam mwenzio. Unatakiwa kupaza sauti ili hayo unayotaka yatimie ila siyo kulalamika na kusema bora angekuwepo flani. Kwa hiyo Viongozi waliopo madarakani kwa sasa huoni wanayofanya au unataka huyo Mwarabu aitwe aje Tz kujibu kwa nini hajengi uwanja. Kumbuka hizo zilikuwa ahadi na pesa ni zake huwezi kumpangia. Km angekuwa ametoa pesa taslim na uwanja haujahengwa hapo ndiyo ungekuwa na nguvu ya kulaum na kutamani aliepita bora angekuwepo lakini siyo kwa ahadi hewa za Mwarabu. Tuache mahaba niue kwenye mambo ya kitaifa.
Mbona una hasira mkuu?!,kosa lake ni kumtaja tu jpm?,jifunze kuuficha udhaifu wako mkuu.
 
Kwani mpaka useme flani angekuwepo. Hivi mlilogwa na nani Watanzania au huyo unaemsema yeye alikuwa na utofauti gani na wanadamu wengine. Kwani wewe unashindwa nini kufuatilia hizo pesa Uarabuni uje ujenge huo uwanja au na wewe umeshakufa. Kuamini kwamba bila mtu flani huwezi lolote ni uzwazwa wa kumuabudu binadam mwenzio. Unatakiwa kupaza sauti ili hayo unayotaka yatimie ila siyo kulalamika na kusema bora angekuwepo flani. Kwa hiyo Viongozi waliopo madarakani kwa sasa huoni wanayofanya au unataka huyo Mwarabu aitwe aje Tz kujibu kwa nini hajengi uwanja. Kumbuka hizo zilikuwa ahadi na pesa ni zake huwezi kumpangia. Km angekuwa ametoa pesa taslim na uwanja haujahengwa hapo ndiyo ungekuwa na nguvu ya kulaum na kutamani aliepita bora angekuwepo lakini siyo kwa ahadi hewa za Mwarabu. Tuache mahaba niue kwenye mambo ya kitaifa.
JPM angekuwepo ungekuwa umejengwa...
 
Mfalme wa Morocco ni tapeli. Alichotaka ni uungwaji mkono arejeshwe uanachama wa AU aliloondolewa 1984 kwa kukalia kimabavu nchi huru ya Sahara Magharibi. Dikteta Magufuli akasaidia kurejeshwa. Ajenge uwanja wa nini tena? Msikiti sawa maana naye ni Muislamu.
 
Back
Top Bottom