Mimi siafiki wazo la kujenga uwanja wa ndege mwingine Bukoba ikibidi waboreshe uwanja uliopo kwa kuuwekea taa za kuruka na kutua wakati wowote. Pia iwekwe control tower ndogo kwa ajili ya mawasiliano. Ikishindikana huu ndio wakati wa kuumalizia uwanja wa kimataifa chato ili watoke Bukoba na kwenda kupandia ndege huko. Sana sana barabara njia nne ijengwe kutoka Bukoba hadi chato 211 km tu ni sawa na mtu wa Morogoro kupandia ndege Dar au mtu wa Shinyanga kupandia ndege Mwanza ni hali ya kawaida kabisa.Hata Geita,Kahama,Mara walipandia ndege Mwanza kabla ya uwepo wa Chatto.Hapa tuboreshe tu miundo mbinu unganishi na viwanja vyetu viweze kufifika kwa urahisi. Kwa sasa wakati wa kuboresha na kumalizia uwanja wa ndege wa Chatto ili kuhudumia Bukoba,Geita,Biharamuro,Ngara nk.vinginevyo huwezi kushindilia maviwanja mengi eneo moja la kanda ya ziwa maana hata huu wa sasa bukoba sidhani utafungwa baada ya kujengwa uwanja mwingine. Tutumie chato international airport tuache siasa za kushinikiza maendeleo,kila mkoa una mahitaji.