Uwanja wa New Jos | Ligi ya Mabingwa Afrika' Plateau United Vs Simba SC

Uwanja wa New Jos | Ligi ya Mabingwa Afrika' Plateau United Vs Simba SC

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Ligi ya Mabingwa barani Afrika kuendelea kupigwa leo November 29, 2020 ambapo, Klabu ya Plateau United, inawakaribisha Mabingwa nchini Tanzania Simba SC, Mnyama kunako dimba la New Jos nchini Nigeria.

Mchezo unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua kwa muda wote wa dakika 90 hasa ukizingatia kwamba kila timu inataka kuanza vema kwenye michuano hii ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kocha wa Simba SC, Sven Vanderbroeck amesema " Hatuna taarifa kuhusu wao lakini mwanzoni tutaanza kwa kuimarisha eneo la ulinzi na kuangalia uimara na udhaifu wao upo eneo gani na baada ya hapo tutaangalia cha kufanya.

" Kila kitu kipo sawa na kila mmoja yupo tayari kwa mchezo na wana furaha kwa hilo, tulichofanyia kazi kwa wiki kadhaa inabidi tukitumie leo, mipango yetu imejikita zaidi upande wetu ili kuhakikisha tunapa ushindi" amesema Sven Vanderbroeck

Kulitaka Mwana, Kulipewa Mwana

Kumbuka mtanange huu wa kombe la Klabu Bingwa Afrika ni kuanzia saa 10: 00 za huko, saa 12: 00 kwa za Tanzania. Usikose Ukaambiwa..!

Update:

=======

Klabu ya Plateau United imezuia kuonyesha matangazo ya moja kwa moja (mubashara) mchezo huu, hata hivyo viongozi wetu chini ya mtendaji mkuu Barbara Gonzalez wanapambana ili mchezo huu uwe Live kwenye Runinga

.....Kikosi cha leo kinachoanza;

1.Aishi Manula
2.Shomari Kapombe
3.Mohamed Hussein
4.Joash Onyango
5.Pascal Wawa
6.Jonas Mkude
7.Hassan Dilunga
8.Erasto Nyoni
9.John Bocco
10.Claotus Chama
11.Luis Miquissone

......Subs;

Beno Kakolanya
Gadiel Michael
Ibrahim Ame
Said Ndemla
Mzamir Yasin
Maddie Kagere
Bernard Morrison


FB_IMG_1606633661279~2.jpg
 
Baada ya Wawakilishi wetu kombe la Shirikisho barani Afrika Namungo FC kufanya kazi bomba

Leo ni zamu ya Wawakilishi wetu kombe la Mabingwa Afrika Simba SC

Kila la heri Mnyama Mkali, Simba SC
 
Kumbuka mtanange huu kama hautakuwa live kwenye Television basi usisahau kuangalia kupitia channel yetu ya Simba SC kwenye YouTube
 
Mimi ni mshabiki wa Yanga ila nakuhakikishia Simba hawezi kutolewa na Plateau na hawezi kufungwa magoli matatu kwasababu Simba wa match fitness kuliko timu ya Plateau united ambayo imekaa zaidi ya miezi sita pasipo kucheza mchezo wowote ule wa kimashindano. Kumbuka hilo
Sijui amekuelewa mpaka hapo..! Hata hivyo Plateau United wanajua Simba SC ni Klabu kubwa
 
Mimi ni mshabiki wa Yanga ila nakuhakikishia Simba hawezi kutolewa na Plateau na hawezi kufungwa magoli matatu kwasababu Simba wana match fitness kuliko timu ya Plateau united ambayo imekaa zaidi ya miezi sita pasipo kucheza mchezo wowote ule wa kimashindano. Kumbuka hilo
Mkuu naona unawapa moyo eeh
 
Back
Top Bottom