Uwanja wa New Jos | Ligi ya Mabingwa Afrika' Plateau United Vs Simba SC

Mkuu naona unawapa moyo eeh
Siwapi moyo huo ndio ukweli. Hawa jamaa kwanzia itokee janga la corona ligi yao ikasimamishwa. Na hawakucheza mchezo wowote ule na ligi ya Nigeria hadi sasa bado haijaanza tena. Sasa wachezaji wanapataje fitness? Je kikosi kinatengenezwaje kwa kutocheza mechi ili kujipima? Sima wana advantage sana ya kufuzu hatua inayofuata
 
Sasa hapa sijajua goma kitarushwa live youtube ama vp
20201129_132347.jpg
 
Leo tunataka sare au ushindi ila kocha tukipigwa hamsa ni bora ubakie huko huko na upitilize kwenda kwenu
Kocha uchebe ndo mpuuzi kutuharibia CV ugenini tafuta sare ukija ushindi ni bora zaidi yeye alikuwa akifunguka ile mbaya bila kuwa na tahadhari, sasa rekodi ile hakuna tena kwa sasa kwa Kocha huyu Vanderbroeck

Angalia alivyosema kwenye uzi hapo
 
Ligi ya Mabingwa barani Afrika kuendelea kupigwa leo November 29, 2020 ambapo, Klabu ya Plateau United, inawakaribisha Mabingwa nchini Tanzania Simba SC, Mnyama kunako dimba la New Jos nchini Nigeria.

Mchezo unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua kwa muda wote wa dakika 90 hasa ukizingatia kwamba kila timu inataka kuanza vema kwenye michuano hii ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kocha wa Simba SC, Sven Vanderbroeck amesema " Hatuna taarifa kuhusu wao lakini mwanzoni tutaanza kwa kuimarisha eneo la ulinzi na kuangalia uimara na udhaifu wao upo eneo gani na baada ya hapo tutaangalia cha kufanya.

" Kila kitu kipo sawa na kila mmoja yupo tayari kwa mchezo na wana furaha kwa hilo, tulichofanyia kazi kwa wiki kadhaa inabidi tukitumie leo, mipango yetu imejikita zaidi upande wetu ili kuhakikisha tunapa ushindi" amesema Sven Vanderbroeck

Kulitaka Mwana, Kulipewa Mwana

Kumbuka mtanange huu wa kombe la Klabu Bingwa Afrika ni kuanzia saa 10: 00 za huko, saa 12: 00 kwa za Tanzania. Usikose Ukaambiwa..!

Update:

=======

Klabu ya Plateau United imezuia kuonyesha matangazo ya moja kwa moja (mubashara) mchezo huu, hata hivyo viongozi wetu chini ya mtendaji mkuu Barbara Gonzalez wanapambana ili mchezo huu uwe Live kwenye Runinga View attachment 1637428
Mwaka jana tuliishia Hamsa, mwaka huu tunaanzia hapo kwenda juu! Lazima tujue namba za kiarabu
 
Nguvu ya Mamba Kumayi..Mk 14 yupo tayari kuwashangaza Plateau United
Screenshot_20201129-135719.jpg
 
Ligi ya Mabingwa barani Afrika kuendelea kupigwa leo November 29, 2020 ambapo, Klabu ya Plateau United, inawakaribisha Mabingwa nchini Tanzania Simba SC, Mnyama kunako dimba la New Jos nchini Nigeria.

Mchezo unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua kwa muda wote wa dakika 90 hasa ukizingatia kwamba kila timu inataka kuanza vema kwenye michuano hii ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kocha wa Simba SC, Sven Vanderbroeck amesema " Hatuna taarifa kuhusu wao lakini mwanzoni tutaanza kwa kuimarisha eneo la ulinzi na kuangalia uimara na udhaifu wao upo eneo gani na baada ya hapo tutaangalia cha kufanya.

" Kila kitu kipo sawa na kila mmoja yupo tayari kwa mchezo na wana furaha kwa hilo, tulichofanyia kazi kwa wiki kadhaa inabidi tukitumie leo, mipango yetu imejikita zaidi upande wetu ili kuhakikisha tunapa ushindi" amesema Sven Vanderbroeck

Kulitaka Mwana, Kulipewa Mwana

Kumbuka mtanange huu wa kombe la Klabu Bingwa Afrika ni kuanzia saa 10: 00 za huko, saa 12: 00 kwa za Tanzania. Usikose Ukaambiwa..!

Update:

=======

Klabu ya Plateau United imezuia kuonyesha matangazo ya moja kwa moja (mubashara) mchezo huu, hata hivyo viongozi wetu chini ya mtendaji mkuu Barbara Gonzalez wanapambana ili mchezo huu uwe Live kwenye Runinga View attachment 1637428
Hapa nasali Simba wapigwe kipigo cha mbwa koko.
 
Simba ndiyo waliokataa huo mtanange usioneshwe na TV za hapa nyumbani lakini huko nigeria watu wanaangalia live
 
Back
Top Bottom