Uwanja wa New Jos | Ligi ya Mabingwa Afrika' Plateau United Vs Simba SC

Uwanja wa New Jos | Ligi ya Mabingwa Afrika' Plateau United Vs Simba SC

Ligi ya Mabingwa barani Afrika kuendelea kupigwa leo November 29, 2020 ambapo, Klabu ya Plateau United, inawakaribisha Mabingwa nchini Tanzania Simba SC, Mnyama kunako dimba la New Jos nchini Nigeria.

Mchezo unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua kwa muda wote wa dakika 90 hasa ukizingatia kwamba kila timu inataka kuanza vema kwenye michuano hii ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kocha wa Simba SC, Sven Vanderbroeck amesema " Hatuna taarifa kuhusu wao lakini mwanzoni tutaanza kwa kuimarisha eneo la ulinzi na kuangalia uimara na udhaifu wao upo eneo gani na baada ya hapo tutaangalia cha kufanya.

" Kila kitu kipo sawa na kila mmoja yupo tayari kwa mchezo na wana furaha kwa hilo, tulichofanyia kazi kwa wiki kadhaa inabidi tukitumie leo, mipango yetu imejikita zaidi upande wetu ili kuhakikisha tunapa ushindi" amesema Sven Vanderbroeck

Kulitaka Mwana, Kulipewa Mwana

Kumbuka mtanange huu wa kombe la Klabu Bingwa Afrika ni kuanzia saa 10: 00 za huko, saa 12: 00 kwa za Tanzania. Usikose Ukaambiwa..!

Update:

=======

Klabu ya Plateau United imezuia kuonyesha matangazo ya moja kwa moja (mubashara) mchezo huu, hata hivyo viongozi wetu chini ya mtendaji mkuu Barbara Gonzalez wanapambana ili mchezo huu uwe Live kwenye Runinga

.....Kikosi cha leo kinachoanza;

1.Aishi Manula
2.Shomari Kapombe
3.Mohamed Hussein
4.Joash Onyango
5.Pascal Wawa
6.Jonas Mkude
7.Hassan Dilunga
8.Erasto Nyoni
9.John Bocco
10.Claotus Chama
11.Luis Miquissone

......Subs;

Beno Kakolanya
Gadiel Michael
Ibrahim Ame
Said Ndemla
Mzamir Yasin
Maddie Kagere
Bernard Morrison


View attachment 1637428
Mimi ni mshabiki wa Yanga ila nakuhakikishia Simba hawezi kutolewa na Plateau na hawezi kufungwa magoli matatu kwasababu Simba wana match fitness kuliko timu ya Plateau united ambayo imekaa zaidi ya miezi sita pasipo kucheza mchezo wowote ule wa kimashindano. Kumbuka hilo
Hii comment ihifadhi sehemu.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Looo naona manjagu yamekaa kila kona ulinzi mi mkali mno
 
Bado tuko nyuma sana katika teknolojia
Yaani huko Nigeria mpira unaoneshwa huku hatuwezi kuona
 
27' Bado milango ni migumu timu zikishambuliana kwa zamu, huku Plateau United wakipa kona tano mpaka ambazo hazikuzaa bao

Plateau United 0-0 Simba SC
 
Pascal Wawa anakuwa mzembe mzembe kurudi kuna kimjamaa kinamsumbua sumbua. Hawezi kurudi kwa kasi
 
Pascal Wawa wewe hicho kindululu unakipeleka wapi? kikate buti iwe kadi ya njano lakini mradi umekipunguza makali.
 
Onyango, Mohamed Hussein, Manula mpaka sasa wamefanya kazi nzuri

Plateau United 0-0 Simba SC
 
Simba 1;3 plateau kwa maoni ya wadau natabiri...!


hakuna.jipya.chini.ya.jua"
 
Ni free kick kuelekea Plateau United

Miquissone anapigaaaa, Inaokolewa huku Mohamed Hussein akionyeshwa kadi ya njano
 
Back
Top Bottom