Yanga Vs Simba......Udhaifu na Ubora wao Kuelekea Kariakoo Derby.
Kama utakuwa umezicheki Simba na Yanga kwa jicho la haki kabisa .Basi Utakubaliana na mimi kuwa......
■ Simba.
Simba imekuwa bora sana kwenye eneo la juu la ushambuliaji. Simba wana options zaidi ya Sita za kuchagua nani Aanze nani abaki benchi na hata subs hazina mashaka sana....Deo Kanda,Luis Kondeboy,Bocco,Dilunga,Chama,Kahata,Kagere,Kichuya na hata Ibrahim Ajib.
Mabeki wa pembeni Shabalala/Gadiel au Kapombe /Shamte nao wanajitahidi kupanda na kuongeza watu juu na kuifanya Simba ishambulie na watu 7 hivi...Ndo maana Simba ina idadi kubwa sana ya magoli ya kufunga na GD. Asilimia 90 ya wachezaji wa Simba wanapenda kupanda kufunga...hata Wawa na Erasto unawaona tu ni attacking minded players kuna muda wanaenda juu
Tatizo la Simba ni Ukabaji....Simba haina mchezaji mwenye character ya ukabaji toka. ameondoka James Kotei.......Sio Mzamiru wala Mkude.....Mkude ni holding midfielder( Kiungo mtuliza timu) na sio diffensive midfielder .Mzamiru nae ana kiherehere cha kwenda mbele sana japo anajitahidi.
So udhaifu mkubwa wa Simba upo kwenye mfumo wao wote wa kukaba..Simba wanaamini njia bora ya kuzuia ni kushambulia ndo maana Simba wamewekeza sana kwenye attacking minded players
.....Sasa ukitaka umpate Simba basi wewe Piga presha kwa kushambulia tu( Yanga chukueni hiyo).
■ Yanga.
Yanga imekuwa bora sana kwenye spirit ya mechi ,hasa zile mechi muhimu.......Yanga ina wachezaji ambao wanaweza kujituma na kufunika madhaifu ya timu. Wachezaji wa Yanga ni wapambanaji sana na wakiamua kukichafua unaweza kushangaa...
Papy Shishimbi ,Haruna Niyo,Balama Mapinduzi ,Kelvin Yondani .......Hawa wana mapafu ya mbwa na wanaweza kucheza Jihad na kulazimisha matokeo....Pia Yanga wana Morrison ambae amejiamini mapema licha ya ugeni wake kwenye VPL..
Kama Yanga wataweza kupandisha juu ari yao mapema na kujituma wanaweza kufanya kitu maana wakati mwingine soka ni nidhamu na kujituma.
Madhaifu makubwa ya Yanga yapo kwenye Idara ya Ushambuliaji...Yanga hawana strikers wa uhakika....Wale Molinga ,Yikpe na Tariq bado sana...Nchimbi anajikongoja ila bado hajauzoea mfumo wa Yanga na nadhani anachezeshwa eneo ambalo sio.( Simba chukueni hii)
Mwisho
Kwa Quality ya Mchezo Simba ipo vizuri ila kwa spirit ya mechi nadhani Yanga wapo vizuri zaidi.
Nani atapigwa kesho?
Kwanza kajiangalie kwenye kioo kama ukifumba macho unapendeza halafu Chukua mzani pima madhaifu na ubora wa timu zote kama nilivyoelezea hapo juu ..unaweza kumpata mshindi.....