Uwanja wa Taifa | Dar Derby, Vodacom Premier League (VPL) Yanga SC yaibamiza Simba SC kwa goli 1 - 0 ; Morrison akata mzizi wa fitina

Pole Mtani. Ndo soka hilo.

Japo nasikitika mukidai tumefanya ndumba. Hivi zingekuwepo si tungekuwa tunawakimbiza kule kileleni? Au ndumba tunazitumia kwa Simba tu?
Hahaha ndumba timu zote mbili zinatumia mtani sema Jana babu yenu alituzidi.

Ukiachana na yote Jana mlikuwa kwenye ubora wenu mtani.

Mimi nakawa najisemea na hawa hawa yanga utoporo ama?
 
NAANZA KUWATAJA MMOJA MMOJA WALE NILIOKUWA NABISHANA NAO WIKI ILIYOPITA NILIWAAMBIA TUNASHINDA 🤣🤣🤣🤣

Bill
Naam mtani, nshakuwa nyau tena, umenikata sharubu tehe tehe, ila ubingwa sikuachii
 
Nilimkubali sana yule jamaa wa kibanda umiza jana... Mpira ulivoisha tu akaweka crop ya kile kipande cha Babalao sehemu hii

"Tumewachapa kidude, Kimewanasa kidude, Hakichomoki kidude, Wanatapatapa"

Endeleeni kutapatapa wakati kimoja tu, kitumbo ndii... mimba
 
Walisahau kumjumuisha refa kwenye Mipango yao
Alikuwepo kwenye intelijensia ila Mafyetelo Fc wakazembea... Walivobebwa ki-SGR wao wakanyoosha miguu, walivyowekwa miguu sawa kumbe walikuwa na viwembe, si wakachana mbeleko bana.... Hahahaaah!

Na wananchi si wamezoea kushikwa mkono na kuburuzwa na lijamaa lenye mihatua yake wakaamua kushikilia guu moja na kubembea... Kila likijaribu kupiga hatua moja liwaache nyuma, litakavopiga ya pili linakuta vimwananchi vipo mbele

Kiujumla Yanga jana walicheza mpira safi sana. Walitumia akili nyingi na maarifa ya kutosha, kuanzia kipa hadi mafowadi... Hata kama wangefungwa lakini mpira walicheza, hadi refa wa kati pale akashindwa afanyaje ili kuwabambikizia hata kapenati ka uongo tu... hahahaaah!
 
Nimeumia Sana Jana tumeshindwa kunywa supu ya vyura,kwani waliongeza Nini mpaka supu ikawa chungu ?any way asiyekubali kushindwa si mshindani.Tujipange kwa michezo ijayo na kuhakisha tunashinda Magoli mengi,mpaka UbInGwA SiMba[emoji123][emoji123] [emoji123] moja .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli kabisa, Yanga wamecheza mpira mkubwa Sana.
Hata ningekuwa mimi unaachaze zawadi nono ya m 200. Kwa kazi ya dakika 90 tu.
Hapo kila mchezaji hakosi M5 au Zaidi, Kwa usawa huu.
Hapo lazima mtu ajitume Kwa asilimia Zote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu jana tumeshuhudia kandanda safi na la kuvutia kwa timu zote mbili hasa timu iliyopata ushindi Dar es Salaam Young Africans.Sasa ni wakati wa kuchambua na kupata mchezaji stahiki wa kuwa Man of the Match.Kiupande wangu Feisal Salum Abdallah anastahili kuwa man of the match kwa kile alichoonesha mbele ya rais wa JMT na rais wa CAF ndugu Ahmad Ahmad.Alikua aggressive sana na utulivu wa hali ya juu katika kutoa maamuzi ya wapi pa kupeleka mpira.Kiufupi roho na engine ya Yanga jana ililala kwa huyu bwana mdogo Feitoto..Je,nani alistahili kuwa MoTM kwa upande wako,kwako Mwalimu Kashasha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yanga wamefanya kile nilichokizungumza kwenye post yangu ya nyuma hongereni sanaa watani [emoji110][emoji110]
 
Nimekuelewa mkuu.

Mimi natamani kuona Simba ikibadilika, na hata mwekezaji wetu ana shauku hiyo hiyo na ndo maana jana alikuwa bored sana.

Kama vipi tukomae pia na kombe la FA, na tujenge mtazamo kuwa hawa Vyura FC wamechokoza nyuki ili hasira zetu tuzielekeze kunako kuwanyoosha kwenye kombe hilo. Tatizo michezaji yetu haieleweki.
 
Kwangu mm ni Tshitshimbi,aliwalinda mabeki na kuwarahisishia kazi Balama,Nionzima kwenda mbele.

Japo Fei toto naye pale kati aliituliza timu katika majukumu yake kama double pivot na Tshishimbi
 
Stori iko hivi, jana ilikuwa balaa maeneo ya uwanja wa taifa kuna Simba alitoroka huko mbugani Manyara akaja town akazua taharuki na kizaazaa kwa kunguruma kama Radi! watu wote waliokuwepo maeneo yale walipoteana wakaingia ndani ya majumba hadi uvunguni na kujificha huku wanatweta na wameloana jasho chapachapa. Bahati nzuri Metacha, Mapinduzi, Feisal na Niyonzima walichungulia dirishani wakamuona Morrison anakuja kwa mbwembwe huku akipanda mpira aliokuja nao!

wakatoka nje fasta na kumuwahi kumwambia kuna jisimba lazingua watu , Morrison akacheka tu akawauliza kwahiyo mnaogopa? wakasema hatuna panga kama lako hatuogopi, mara Hamad! Simba akatokea ghafla akanguruma kama radi Morisson akawasukuma jamaa zake nyuma na kutazamana na Simba yule tayari kuanza masumbwi! Morrison akamtisha Simba kama anampa jeb (ngumi) , Simba akakubali kutingishika,

Morrison akamrukia na kumchinja huku kamkaba kila mahali! Simba akaugulia maumivu na kulala chini na kuanza kukoroma na kupigapiga miguu! Morrison akawaita watu wote waje wamnyonyoe Simba tayari kuwa kitoweo cha pilau ya kusherehekea siku ya wanawake duniani, akaenda zake akiacha Simba anyonyolewa na maji ya moto, nani anabisha Morrison akiwa peke yake uwanjani anaweza kuifunga Simba yenye wachezaji 11? ukibisha uwe na point na ushahidi!
 

Attachments

  • D1CB902B-2CB7-4726-BF7C-89C9A95A1748.png
    112.2 KB · Views: 1
Stori iko hivi, jana ilikuwa balaa maeneo ya uwanja wa taifa kuna Simba alitoroka huko mbugani Manyara akaja town akazua taharuki na kizaazaa kwa kunguruma kama radi. watu wote waliokuwepo maeneo yale walipoteana wakaingia ndani ya majumba hadi uvunguni na kujificha huku wanatweta na wameloana jasho chapachapa.

Bahati nzuri Metacha, Mapinduzi, Feisal na Niyonzima walichungulia dirishani wakamuona Morrison anakuja kwa mbwembwe huku akipanda mpira aliokuja nao. wakatoka nje fasta na kumuwahi kumwambia kuna jisimba lazingua watu, Morrison akacheka tu akawauliza kwahiyo mnaogopa? Wakasema hatuna panga kama lako hatuogopi, mara Hamad! Simba akatokea ghafla akanguruma kama radi Morisson akawasukuma jamaa zake nyuma na kutazamana na Simba yule tayari kuanza masumbwi.

Morrison akamtisha Simba kama anampa jeb (ngumi), Simba akakubali kutingishika, Morrison akamrukia na kumchinja huku kamkaba kila mahali! Simba akaugulia maumivu na kulala chini na kuanza kukoroma na kupigapiga miguu! Morrison akawaita watu wote waje wamnyonyoe Simba tayari kuwa kitoweo cha pilau ya kusherehekea siku ya wanawake duniani, Morrison akaenda zake akiacha Simba anyonyolewa na maji ya moto, nani anabisha Morrison akiwa peke yake uwanjani anaweza kuifunga Simba yenye wachezaji 11? ukibisha uwe na point na ushahidi!

Pole sana Simba followers wote kuanzia leo timu ya Wananchi mkiiona muwe mnakimbia uwanjani msije mmepaka rangi usoni na majezi yenu mtaaibika sana kama Morrison yupo! Jana mawakala wa Man United, Real Madrid na Zamalek wote walikuwepo shamba la bibi kudaka Saini ya Morrison!

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…