Uwanja wa Taifa | Dar Derby, Vodacom Premier League (VPL) Yanga SC yaibamiza Simba SC kwa goli 1 - 0 ; Morrison akata mzizi wa fitina

Uwanja wa Taifa | Dar Derby, Vodacom Premier League (VPL) Yanga SC yaibamiza Simba SC kwa goli 1 - 0 ; Morrison akata mzizi wa fitina

Pole Mtani. Ndo soka hilo.

Japo nasikitika mukidai tumefanya ndumba. Hivi zingekuwepo si tungekuwa tunawakimbiza kule kileleni? Au ndumba tunazitumia kwa Simba tu?
Hahaha ndumba timu zote mbili zinatumia mtani sema Jana babu yenu alituzidi.

Ukiachana na yote Jana mlikuwa kwenye ubora wenu mtani.

Mimi nakawa najisemea na hawa hawa yanga utoporo ama?
 
NAANZA KUWATAJA MMOJA MMOJA WALE NILIOKUWA NABISHANA NAO WIKI ILIYOPITA NILIWAAMBIA TUNASHINDA 🤣🤣🤣🤣

Bill
Naam mtani, nshakuwa nyau tena, umenikata sharubu tehe tehe, ila ubingwa sikuachii
 
Binafsi ninajivunia kuwa shabiki wa SIMBA SC. Timu ambayo ikifungwa Mashabiki wake wanakubali walizidiwa mbinu za mchezo ila jana ingelishinda Simba SC mashabiki wa Vyura FC ungeliwasikia Simba wamebebwa.
Hongereni wanawake kwa Kupata furaha kwenye siku yenu. SIMBA SC Mabingwa watarajiwa kwa miaka 8 mfululizo ijayo. DIE HAD FAN.
Nilimkubali sana yule jamaa wa kibanda umiza jana... Mpira ulivoisha tu akaweka crop ya kile kipande cha Babalao sehemu hii

"Tumewachapa kidude, Kimewanasa kidude, Hakichomoki kidude, Wanatapatapa"

Endeleeni kutapatapa wakati kimoja tu, kitumbo ndii... mimba
 
Walisahau kumjumuisha refa kwenye Mipango yao
Alikuwepo kwenye intelijensia ila Mafyetelo Fc wakazembea... Walivobebwa ki-SGR wao wakanyoosha miguu, walivyowekwa miguu sawa kumbe walikuwa na viwembe, si wakachana mbeleko bana.... Hahahaaah!

Na wananchi si wamezoea kushikwa mkono na kuburuzwa na lijamaa lenye mihatua yake wakaamua kushikilia guu moja na kubembea... Kila likijaribu kupiga hatua moja liwaache nyuma, litakavopiga ya pili linakuta vimwananchi vipo mbele

Kiujumla Yanga jana walicheza mpira safi sana. Walitumia akili nyingi na maarifa ya kutosha, kuanzia kipa hadi mafowadi... Hata kama wangefungwa lakini mpira walicheza, hadi refa wa kati pale akashindwa afanyaje ili kuwabambikizia hata kapenati ka uongo tu... hahahaaah!
 
Nimeumia Sana Jana tumeshindwa kunywa supu ya vyura,kwani waliongeza Nini mpaka supu ikawa chungu ?any way asiyekubali kushindwa si mshindani.Tujipange kwa michezo ijayo na kuhakisha tunashinda Magoli mengi,mpaka UbInGwA SiMba[emoji123][emoji123] [emoji123] moja .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli kabisa, Yanga wamecheza mpira mkubwa Sana.
Hata ningekuwa mimi unaachaze zawadi nono ya m 200. Kwa kazi ya dakika 90 tu.
Hapo kila mchezaji hakosi M5 au Zaidi, Kwa usawa huu.
Hapo lazima mtu ajitume Kwa asilimia Zote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu jana tumeshuhudia kandanda safi na la kuvutia kwa timu zote mbili hasa timu iliyopata ushindi Dar es Salaam Young Africans.Sasa ni wakati wa kuchambua na kupata mchezaji stahiki wa kuwa Man of the Match.Kiupande wangu Feisal Salum Abdallah anastahili kuwa man of the match kwa kile alichoonesha mbele ya rais wa JMT na rais wa CAF ndugu Ahmad Ahmad.Alikua aggressive sana na utulivu wa hali ya juu katika kutoa maamuzi ya wapi pa kupeleka mpira.Kiufupi roho na engine ya Yanga jana ililala kwa huyu bwana mdogo Feitoto..Je,nani alistahili kuwa MoTM kwa upande wako,kwako Mwalimu Kashasha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yanga Vs Simba......Udhaifu na Ubora wao Kuelekea Kariakoo Derby.

Kama utakuwa umezicheki Simba na Yanga kwa jicho la haki kabisa .Basi Utakubaliana na mimi kuwa......

■ Simba.
Simba imekuwa bora sana kwenye eneo la juu la ushambuliaji. Simba wana options zaidi ya Sita za kuchagua nani Aanze nani abaki benchi na hata subs hazina mashaka sana....Deo Kanda,Luis Kondeboy,Bocco,Dilunga,Chama,Kahata,Kagere,Kichuya na hata Ibrahim Ajib.

Mabeki wa pembeni Shabalala/Gadiel au Kapombe /Shamte nao wanajitahidi kupanda na kuongeza watu juu na kuifanya Simba ishambulie na watu 7 hivi...Ndo maana Simba ina idadi kubwa sana ya magoli ya kufunga na GD. Asilimia 90 ya wachezaji wa Simba wanapenda kupanda kufunga...hata Wawa na Erasto unawaona tu ni attacking minded players kuna muda wanaenda juu

Tatizo la Simba ni Ukabaji....Simba haina mchezaji mwenye character ya ukabaji toka. ameondoka James Kotei.......Sio Mzamiru wala Mkude.....Mkude ni holding midfielder( Kiungo mtuliza timu) na sio diffensive midfielder .Mzamiru nae ana kiherehere cha kwenda mbele sana japo anajitahidi.

So udhaifu mkubwa wa Simba upo kwenye mfumo wao wote wa kukaba..Simba wanaamini njia bora ya kuzuia ni kushambulia ndo maana Simba wamewekeza sana kwenye attacking minded players
.....Sasa ukitaka umpate Simba basi wewe Piga presha kwa kushambulia tu( Yanga chukueni hiyo).

■ Yanga.

Yanga imekuwa bora sana kwenye spirit ya mechi ,hasa zile mechi muhimu.......Yanga ina wachezaji ambao wanaweza kujituma na kufunika madhaifu ya timu. Wachezaji wa Yanga ni wapambanaji sana na wakiamua kukichafua unaweza kushangaa...

Papy Shishimbi ,Haruna Niyo,Balama Mapinduzi ,Kelvin Yondani .......Hawa wana mapafu ya mbwa na wanaweza kucheza Jihad na kulazimisha matokeo....Pia Yanga wana Morrison ambae amejiamini mapema licha ya ugeni wake kwenye VPL..

Kama Yanga wataweza kupandisha juu ari yao mapema na kujituma wanaweza kufanya kitu maana wakati mwingine soka ni nidhamu na kujituma.

Madhaifu makubwa ya Yanga yapo kwenye Idara ya Ushambuliaji...Yanga hawana strikers wa uhakika....Wale Molinga ,Yikpe na Tariq bado sana...Nchimbi anajikongoja ila bado hajauzoea mfumo wa Yanga na nadhani anachezeshwa eneo ambalo sio.( Simba chukueni hii)

Mwisho

Kwa Quality ya Mchezo Simba ipo vizuri ila kwa spirit ya mechi nadhani Yanga wapo vizuri zaidi.

Nani atapigwa kesho?

Kwanza kajiangalie kwenye kioo kama ukifumba macho unapendeza halafu Chukua mzani pima madhaifu na ubora wa timu zote kama nilivyoelezea hapo juu ..unaweza kumpata mshindi.....
Yanga wamefanya kile nilichokizungumza kwenye post yangu ya nyuma hongereni sanaa watani [emoji110][emoji110]
 
Punguza Hasira na Matusi Mdau kwani yawezekana kuna wengine tumeumia kuliko hata Wewe ukizingatia hata katika Kamati za Kiutamaduni wa Mwafrika tumo na tumejitahidi huku wengine hadi tukikufuru kwa Mwenyezi Mungu ila Simba SC yetu ishinde jana lakini Mambo hayakuenda kama tulivyotaka na hata bahati pia haikuwa Upande Wetu. Najua umeumia ila punguza Munkari lakini pia tusiwabeze Yanga FC kwani nao ni Timu tena Kubwa sana na hata Kihistoria imetuzidi Mafanikio kwa mambo mengi. Kuwa Mwanamichezo zaidi na usiwe Shabiki Mpumbavu. Tujipangeni kwa Mechi zijazo za Ligi ili tubebe tena Ubingwa kisha Mwekezaji wetu atatusajilia Majembe zaidi. Simba SC haichezi Ligi Kuu ili Kumfunga Yanga FC bali inacheza Ligi Kuu ili Kutafuta Mataji na hata ikitokea tumewafunga Yanga FC basi jua ni Chachandu tu katika Michezo yetu tunayoicheza.
Nimekuelewa mkuu.

Mimi natamani kuona Simba ikibadilika, na hata mwekezaji wetu ana shauku hiyo hiyo na ndo maana jana alikuwa bored sana.

Kama vipi tukomae pia na kombe la FA, na tujenge mtazamo kuwa hawa Vyura FC wamechokoza nyuki ili hasira zetu tuzielekeze kunako kuwanyoosha kwenye kombe hilo. Tatizo michezaji yetu haieleweki.
 
Kwangu mm ni Tshitshimbi,aliwalinda mabeki na kuwarahisishia kazi Balama,Nionzima kwenda mbele.

Japo Fei toto naye pale kati aliituliza timu katika majukumu yake kama double pivot na Tshishimbi
 
Stori iko hivi, jana ilikuwa balaa maeneo ya uwanja wa taifa kuna Simba alitoroka huko mbugani Manyara akaja town akazua taharuki na kizaazaa kwa kunguruma kama Radi! watu wote waliokuwepo maeneo yale walipoteana wakaingia ndani ya majumba hadi uvunguni na kujificha huku wanatweta na wameloana jasho chapachapa. Bahati nzuri Metacha, Mapinduzi, Feisal na Niyonzima walichungulia dirishani wakamuona Morrison anakuja kwa mbwembwe huku akipanda mpira aliokuja nao!

wakatoka nje fasta na kumuwahi kumwambia kuna jisimba lazingua watu , Morrison akacheka tu akawauliza kwahiyo mnaogopa? wakasema hatuna panga kama lako hatuogopi, mara Hamad! Simba akatokea ghafla akanguruma kama radi Morisson akawasukuma jamaa zake nyuma na kutazamana na Simba yule tayari kuanza masumbwi! Morrison akamtisha Simba kama anampa jeb (ngumi) , Simba akakubali kutingishika,

Morrison akamrukia na kumchinja huku kamkaba kila mahali! Simba akaugulia maumivu na kulala chini na kuanza kukoroma na kupigapiga miguu! Morrison akawaita watu wote waje wamnyonyoe Simba tayari kuwa kitoweo cha pilau ya kusherehekea siku ya wanawake duniani, akaenda zake akiacha Simba anyonyolewa na maji ya moto, nani anabisha Morrison akiwa peke yake uwanjani anaweza kuifunga Simba yenye wachezaji 11? ukibisha uwe na point na ushahidi!
 

Attachments

  • D1CB902B-2CB7-4726-BF7C-89C9A95A1748.png
    D1CB902B-2CB7-4726-BF7C-89C9A95A1748.png
    112.2 KB · Views: 1
Stori iko hivi, jana ilikuwa balaa maeneo ya uwanja wa taifa kuna Simba alitoroka huko mbugani Manyara akaja town akazua taharuki na kizaazaa kwa kunguruma kama radi. watu wote waliokuwepo maeneo yale walipoteana wakaingia ndani ya majumba hadi uvunguni na kujificha huku wanatweta na wameloana jasho chapachapa.

Bahati nzuri Metacha, Mapinduzi, Feisal na Niyonzima walichungulia dirishani wakamuona Morrison anakuja kwa mbwembwe huku akipanda mpira aliokuja nao. wakatoka nje fasta na kumuwahi kumwambia kuna jisimba lazingua watu, Morrison akacheka tu akawauliza kwahiyo mnaogopa? Wakasema hatuna panga kama lako hatuogopi, mara Hamad! Simba akatokea ghafla akanguruma kama radi Morisson akawasukuma jamaa zake nyuma na kutazamana na Simba yule tayari kuanza masumbwi.

Morrison akamtisha Simba kama anampa jeb (ngumi), Simba akakubali kutingishika, Morrison akamrukia na kumchinja huku kamkaba kila mahali! Simba akaugulia maumivu na kulala chini na kuanza kukoroma na kupigapiga miguu! Morrison akawaita watu wote waje wamnyonyoe Simba tayari kuwa kitoweo cha pilau ya kusherehekea siku ya wanawake duniani, Morrison akaenda zake akiacha Simba anyonyolewa na maji ya moto, nani anabisha Morrison akiwa peke yake uwanjani anaweza kuifunga Simba yenye wachezaji 11? ukibisha uwe na point na ushahidi!

Pole sana Simba followers wote kuanzia leo timu ya Wananchi mkiiona muwe mnakimbia uwanjani msije mmepaka rangi usoni na majezi yenu mtaaibika sana kama Morrison yupo! Jana mawakala wa Man United, Real Madrid na Zamalek wote walikuwepo shamba la bibi kudaka Saini ya Morrison!

5C222BD1-455E-4E25-9669-BE848292AA29.png
 
Back
Top Bottom