Klabu ya
Simba Sports Club leo Jumapili inajitupa katika dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, kuanza harakati za kupambana kimataifa kwa kucheza na klabu ya
Gendarmarie Nationale FC, ya nchini Djibout kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya awali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Simba SC, Mnyama wanarejea michuano ya kimataifa huku wakiwa na matokeo mazuri kwenye Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara
VPL, hali inayoaminiwa na mashabiki na wanachama wao kuwa huenda furaha ikawa chachu ya wachezaji wao kuendeleza furaha.
Utashuhudia pambano hili Live kupitia Azam Sports 2 kuanzia saa 10: jioni. Kaa nasi kukuletea yatakayojiri, usikose ukaambiwa
Vikosi vya timu zote zimetoshana nguvu kwa upande wa Simba SC;
Aishi Manula, Shomari Kapombe, Asante Kwasi, James Kotei, Yusuf Mlipili, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Said Ndemla, John Bocco, Emmanuel Okwi.
Sub; Emmanuel Mseja, Mzamir Yassin, Mwinyi Kazimoto, Moses Kitundu, Paul Bukaba, Ally Shomari, Juuko Murshid.
Coaches; Pierre Lechantre - Head Coach
Masoud Djuma - Assistant Coach Mohamed Aymen - Fitness Coach Muharam Mohamed - Gk Coach
Timu uwanjani tayari kwa mtanange huu. Na Rais Mstaafu Ndugu Ali Hassan Mwinyi ambaye ni mgeni rasmi kwenye mchezo huu tayari anakagua timu zote mbili.
Wakati wowote mpira utaanza hapa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Naam mpira umekwisha ananza uwanja wa Taifa
00' Simba SC 0-0 Gendarmarie Nationale FC.
02 ' Goooooooooaal Said Ndemla amepiga faulo na kutinga wavuni moja kwa moja
Simba SC 1-0 Gendarmarie FC
15' uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam
Simba SC 1-0 Gendarmarie Nationale FC
30' uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam
Simba SC 1-0 Gendarmarie FC
32 ' Goooooooooaal John Bocco anaandika bao la pili kwa kichwa kazi mzuri kutoka upande wa kushoto.
Simba SC 2-0 Gendarmarie Nationale FC
45' Goooooooooaal goooooooooaal goooooooooaal John Bocco anaandika bao la tatu upande wa Simba SC
45' Naam mpira ni mapumziko hapa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam
Simba SC wanakwenda wakiwa mbele ya magoli tatu bila majibu dhidi ya Gendarmarie Nationale FC
Naam mpira umeanza kipindi cha pili uwanja wa Taifa.
50' Gendarmarie FC wanapata penati. Inapigwa Penaltiiiiiiiii lakini golikipa Aishi Manula anapangua mkwaju huo na kuwa konaa.
Konaaaaa inapigwaaaa la la la nje!
65' Simba SC 3-0 Gendarmarie Nationale FC