Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Dk ya 24 kipindi cha pili Simba 3, Gendarmarie 0Klabu ya Simba Sports Club leo Jumapili inajitupa katika dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, kuanza harakati za kupambana kimataifa kwa kucheza na klabu ya Gendarmarie Nationale FC, ya nchini Djibout kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya awali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.![]()
Simba SC, Mnyama wanarejea michuano ya kimataifa huku wakiwa na matokeo mazuri kwenye Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara VPL, hali inayoaminiwa na mashabiki na wanachama wao kuwa huenda furaha ikawa chachu ya wachezaji wao kuendeleza furaha.
Utashuhudia pambano hili Live kupitia Azam Sports 2 kuanzia saa 10: jioni. Kaa nasi kukuletea yatakayojiri, usikose ukaambiwa
Vikosi vya timu zote zimetoshana nguvu kwa upande wa Simba SC;
Aishi Manula, Shomari Kapombe, Asante Kwasi, James Kotei, Yusuf Mlipili, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Said Ndemla, John Bocco, Emmanuel Okwi.
Sub; Emmanuel Mseja, Mzamir Yassin, Mwinyi Kazimoto, Moses Kitundu, Paul Bukaba, Ally Shomari, Juuko Murshid.
Coaches; Pierre Lechantre - Head Coach
Masoud Djuma - Assistant Coach Mohamed Aymen - Fitness Coach Muharam Mohamed - Gk Coach
Timu uwanjani tayari kwa mtanange huu. Na Rais Mstaafu Ndugu Ali Hassan Mwinyi ambaye ni mgeni rasmi kwenye mchezo huu tayari anakagua timu zote mbili.
Wakati wowote mpira utaanza hapa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Naam mpira umekwisha ananza uwanja wa Taifa
00' Simba SC 0-0 Gendarmarie Nationale FC.
02 ' Goooooooooaal Said Ndemla amepiga faulo na kutinga wavuni moja kwa moja
Simba SC 1-0 Gendarmarie FC
15' uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam
Simba SC 1-0 Gendarmarie Nationale FC
30' uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam
Simba SC 1-0 Gendarmarie FC
32 ' Goooooooooaal John Bocco anaandika bao la pili kwa kichwa kazi mzuri kutoka upande wa kushoto.
Simba SC 2-0 Gendarmarie Nationale FC
45' Goooooooooaal goooooooooaal goooooooooaal John Bocco anaandika bao la tatu upande wa Simba SC
45' Naam mpira ni mapumziko hapa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam![]()
![]()
Simba SC wanakwenda wakiwa mbele ya magoli tatu bila majibu dhidi ya Gendarmarie Nationale FC
Naam mpira umeanza kipindi cha pili uwanja wa Taifa.
50' Gendarmarie FC wanapata penati. Inapigwa Penaltiiiiiiiii lakini golikipa Aishi Manula anapangua mkwaju huo na kuwa konaa.
Konaaaaa inapigwaaaa la la la nje!
65' Simba SC 3-0 Gendarmarie Nationale FC
sijatumwa, hii siyo timu ya kujivuna kuwa tumeifunga. mimi ni mpenzi wa Simba kwa miaka kama 40 iliyopita.. lkn ukweli ni huo. Hivi ni vitimu vidogo kutoka nchi hoeehae!umetumwaa??!!
Sasa hapa kuna timu kweli??? Simba tusubili mechi zijazo tupewe dozi yetu then tuludi bara kwenye ligi kuu ya nyanya
Wewe acha kutulisha Matango hapa wewe sio Mpenzi was Simba,wapenzi was Simba Tunawajua....mbona Jana Yanga kashinda Ka goli kamoja kwa Timu Dhaifu hukuongea....tena wao Yanga wanasema Ushindi ushindi Tuuu!sijatumwa, hii siyo timu ya kujivuna kuwa tumeifunga. mimi ni mpenzi wa Simba kwa miaka kama 40 iliyopita.. lkn ukweli ni huo. Hivi ni vitimu vidogo kutoka nchi hoeehae!
If you face reality, and make reformation, you improve! Hiki ni kitimu kidogo, huko mbele kuna timu kubwa (nadhani???), inabidi kiwango cha mchezo kiwe juu sana kwa vitimu kama hivi! Mpaka kinaleta penalty! huoni kuwa pamoja na kukifunga lkn standard ya uchezaji siyo that much high kwa kitimu kama hiki!Wewe acha kutulisha Matango hapa wewe sio Mpenzi was Simba,wapenzi was Simba Tunawajua....mbona Jana Yanga kashinda Ka goli kamoja kwa Timu Dhaifu hukuongea....tena wao Yanga wanasema Ushindi ushindi Tuuu!
Point 3.