Joseverest
JF-Expert Member
- Sep 25, 2013
- 52,812
- 71,392
MPIRA MUDA WOWOTE UNAISHA
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu usinisahau
Full Time Yanga 2 Mbao FC 0Mkuu usinisahau
Hahahaaaa , nipo mkuu nawaona mkikaribia kunyakua point zote tatu toka kwa hao madogo
Habari mbaya hii kwa mbumbumbu fcAhahaha usijali mkuuFull Time Yanga 2 Mbao FC 0
Rekebisha hapo ni 2 bilaKatika Ligi Kuu Tanzania Bara VPL, leo Yanga SC, kukipiga na Mbao FC katika dimba la Taifa jijini Dar es salaam.
Mchezo wa leo unatabiriwa kuwa wa ushindani kufualitia kumbukumbu ya mchezo wa awali ambapo Mbao FC waliibuka kwa ushindi wa 2-0.
Kwa sasa ligi ikiwa ukingoni tayari bingwa ameshapatika kwa Simba SC kunyakua Kombe hilo kabla ligi kumalizika rasmi, huku Azam FC hadi sasa ikiwa nafasi ya pili kwa kuizidi Yanga alama saba imebakiwa na mchezo mmoja dhidi ya Yanga.
Yanga inayoshika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi, inahitaji kushinda mchezo huo,ili kumaliza rekodi mbaya ya kucheza michezo tisa bila ya kushinda ikiwemo michezo sita bila ya kufunga bao.
View attachment 783691View attachment 783692
Naam wakati wowote mpira utaanza
0' Mpira umeanza kwa Yanga kushambulia vilivyo lango la Mbao FC
5' Yusuf Mhilu alitaka kuwanyanyua wana Yanga kwa shambulizi lake lakini haikuwa hivyo
10' Yanga SC 0-0 Mbao FC uwanja wa Taifa.
Mchezo hauna kasi sana kwa pande mbili ingawa Yanga wanajitahidi kulifikia lango la Mbao FC
Wanachukua Mbao FC..lakini mpira wanapoteza na kuchukua Yanga
12' mchezaji Buswita anakosa bao la wazi kwa mpira wake kupaa lango la Mbao FC
18' Daud anashindwa kukaa vizuri kwenye lango la Mbao FC hivyo kushindwa kukwamisha mpira wavuni
23' Bado milango ni migumu Yanga SC dhidi ya Mbao FC.
25' Mchezaji wa Mbao FC anaunawa mpira ni faulo...Inapigwa na Kamusoko
28' Gooooooooaaaal, Yanga wanaandika bao la kwanza kufuatia Free Kick ya Kamusoko
Yanga SC 1-0 Mbao FC
35' Amos anapiga kona lakini golikipa wa Yanga anapangua na wanachukua Yanga sasa.
40' Kombo anakwenda mbele na mpira. Lakini Youthe Rostand golikipa anawahi mpira ule
42' Kamusoko anaumia anatoka nje..Na anaingia tena baada ya matibabu
44' Ndikumana anapiga shuti na kutoka nje ya lango la Yanga SC
45' Mpira ni mapumziko uwanja wa Taifa ambapo Yanga wako mbele kwa goli moja dhidi ya Mbao FC
Kipindi cha lala salama kimeanza..Mabadiliko kwa Yanga SC
Anatoka Yusuf Mhilu na nafasi yake inachukuliwa na Matheo
48' Matheo anapiga shuti kali..Lakini ni goal kick..!
Mbao wanapiga kona..Lakini haijazaa matunda.
55' Ndaki anakwenda kwenye benchi anaingia Kevin upande wa Mbao FC
58' Mwasa anapiga shuti na kuwa kona ya Nne...Inapigwa kona ambayo haikuzaa matunda upande wa Mbao FC
Njinja anapiga mpira mbele na kuondosha hatari zote lango la Yanga
65' Mbao FC wanashindwa kuandika bao baada ya wachezaji wa Yanga kuzubaa
Ni faulo kuelekea Yanga SC..Inapigwa nje.
69' Emmanuel anakwenda kwenye benchi na anainga Mwashiuya upande wa Yanga
Nafasi kwa Mbao FC..Lakini wanapoteza kwa kupaka sana rangi
Buswita anapiga shuti kali..Lakini linashindwa kulenga lango la Mbao FC
75' Daud anakwenda kwenye benchi anangia Paul Godfrey upande wa Yanga
79' Mwashuiya anakosa goli la wazi..Ilikuwa nafasi nzuri kuandika bao la pili.
Inapigwa shuti golikipa Youthe anadaka na kuanza kwa mchezaji wake
83' Yanga SC 1-0 Mbao FC uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam
Wakati wowote mpira utamalizika hapa uwanja wa Taifa..Mwamuzi anaangalia saa yake.
90' Naam mpira umekwisha uwanja wa Taifa ambapo Yanga wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Mbao FC ikiwa ni ushindi wao wa kwanza baada ya kupita mechi tisa mfululizo katika michuano yote
Hii ndio Yanga sasaHahahaaaa , nipo mkuu nawaona mkikaribia kunyakua point zote tatu toka kwa hao madogo
Hajar anamalizia majukumu mawili matatu, usipomuona leo basi kesho mapema tu atakuja kushangilia huku
Hawatalala leo huko, wanawaza wao watafunga lini goli kama hiliIBRAHIMU AJIBU KAFUNGA GOLI LA KIMATAIFA HAHAHA
Mikia Fc wakiona lile goli wanazimia[emoji2][emoji2][emoji2][emoji41][emoji6][emoji3][emoji23][emoji23]
Habari mbaya hii kwa mbumbumbu fc
Vipi unalionaje goli la Ajibu?Yanga tia maji tia maji. Hawawezi kucheza dk 90. Wakati Simba inatamani mpira uwe dk 120 mashabiki wapati raha ya pasi gonga
Watakaa sana mpaka waje wafunge goli safi na murua kama lileHawatalala leo huko, wanawaza wao watafunga lini goli kama hili
Hahaaaa watapata tabu sana mwaka huuWatakaa sana mpaka waje wafunge goli safi na murua kama lile
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Hahaaaa watapata tabu sana mwaka huu
Goli la ajibu linaweza kukuponya presha ingawa kwa mikia fc linawaongezea ugonjwa wa presha
Hahahaha haya bana mkuu ila safari bado sana ujuePoint 3 zote tumezibebaHii ndio Yanga sasa
Lile goli Ronaldo anasubiriYANGA 2 MBAO 0
AJIBU IBRAHIM ANAPIGA GOLI MOJA MARIDADI HAPA