Uwanja wa Uhuru umefurika sana!, watu Washindwa kuaga. Watakiwa kujipanga barabarani kuelekea Uwanja wa ndege ili waweze kupunga mkono

Uwanja wa Uhuru umefurika sana!, watu Washindwa kuaga. Watakiwa kujipanga barabarani kuelekea Uwanja wa ndege ili waweze kupunga mkono

Wanachi wa dar es salaam wanataka kumuaga rais wao. Kwa yanayoendelea hapa uwanjani leo hawamalizi


Mungu baba wa mbinguni endelea kulipigania taifa lako la Tanzania.
Kama ulivyofanya kwa wana wa Israel ukafanye na Tanzania pia.
Uliwachukua Mussa na Haruni lakini ulikua umewaandalia Joshua.
Tunakushukuru sababu umemchukua John Pombe Magufuli na kutuachia Samia Suluhu Hassan.

Tunakuomba kwa rehema zako umpe hekima, muepushe na watu wasio sahihi na ukampe wasaidizi sahihi na wazalendo ili aweze kutufikisha kule tunakotaka kufika🙏
 
Kwaiyo nyie wa dar es sallam nd mna uchungu nae sana
 
Ubinafsi huo. Basi aje na huku chuga tumuage
 
Ili kuwatendea haki Wakazi wa Dar es salaam tunaomba kamati ya mazishi ya hayati Magufuli muongeze walau siku moja ili zoezi hili liitimishwe kesho.

Uwanja umefurika na nje misururu ni mirefu sana.

Maendeleo hayana vyama!
Acheni kurudia rudia, nimekuona mara 3 ukipita kuaga
 
Ni ushauri tu hapa Dar es salaam zoezi la kumuaga mpendwa wetu kwa siku ya leo limeenda kienyeji sana na sasa watu wanapungia mkono kibanda badala ya jeneza la hayati Magufuli.

Naelewa Zanzibar wana kamati ndogo ambayo naamini itafanya vizuri.

Wasiwasi wangu ni Dodoma, Mwanza na Geita ambako kutakuwa na maelfu ya waombolezaji kutoka mikoa mbalimbali.

Ni vema kamati ikajitathmini na kuchukua hatua stahiki haraka ili hayati Magufuli aagwe na wapendwa wake wote kwa heshima na utamaduni unaostahili.

Maendeleo hayana vyama!
 
Hivi ni kwa nini wachukua picha za video hawachukui sehemu ambayo na sisi tunaoomboleza tukiwa nyumbani tunaweza kuona sura ya Mh. Kwa dakika za mwisho? Au wanakatazwa? Au ndio maadili ya kazi yanawataka hivyo!? Ningetamani waonyeshe kama ilivyokuwaga kwa Hayati Baba Wa Taifa!
 
Habari,

Kusema kweli nathibitisha na ninazidi kuthibitisha kwa Magu was Peoples Choice, kumbe hata zile kura 2020 zilikuwa ni za haki wakasema aliiba.

Kwa nyomi hii ya watu wanaomlilia wakiomboleza kifo chake yatosha kusema kuwa, Alikuwa chaguo la waTanzania... Wale waliompinga ni watu wachache tuu wenye chuki binafsi, ambao ilibidi waumie ili wengi tuishi kwa furaha.

Nawasilisha,
 
Ili kuwatendea haki Wakazi wa Dar es salaam tunaomba kamati ya mazishi ya hayati Magufuli muongeze walau siku moja ili zoezi hili liitimishwe kesho.

Uwanja umefurika na nje misururu ni mirefu sana.

Maendeleo hayana vyama!
View attachment 1730918
Serikali isipochukua hatua za tahadhari, especially wizara ya afya, baada ya msiba huu, corona itamaliza watu.
 
Ili kuwatendea haki Wakazi wa Dar es salaam tunaomba kamati ya mazishi ya hayati Magufuli muongeze walau siku moja ili zoezi hili liitimishwe kesho.

Uwanja umefurika na nje misururu ni mirefu sana.

Maendeleo hayana vyama!
View attachment 1730918

Barakoa za kuhesabu tahadhari za kujikinga hamna.

Eeh mola wetu utupishilie mbali na kirusi huyu mtoa roho za watu pasipo na kujali vyeo vyao.
 
Kwa kweli aliyepanga huku utaratibu wa kumtembeza marehemu kama bidhaa, alaaniwe.

Umefiwa, halafu unaambiwa kuwa wewe na marehemu Wako, twende Zanzibar, twende Dodoma, twende Mwanza, twende Geita, halafu Chato!!

Walio hai wanatakiwa kumfuata marehemu. Walio hai ndio wanatakiwa kusafiri na kwenda kumuaga marehemu. Kinachofanyika sasa ni kumtembeza marehemu, kuwafuata walio hai ili akawaage.

Hapa Serikali imechsha sana.

Ilitakiwa Magufuli aagwe Dar. Wananchi wa Zanzibar, Dodoma na mikoa yote ya pwani na Kusini, wangeenda Dar kukuaga.

Baada ya hapo mwili ungepelekwa airport, moja kwa moja Chato. Watu wa Geita na Mwanza wangeenda Chato, kumpokea marehemu na kumuaga. Kama ilivyofanyika kwa Mwalimu. Ilikuwa Dar - Butiama.
 
Mtu anaependwa sana na Gwajima yupo. Mbwe nyingi zisizo na msaada kwa marehemu, mtabadirisha majeneza ili iweje. Gwajima si amfufue tuone.
 
Wengine wanaenda kutazama huo umati
Wengine ni event tu..hawana cha huzuni wala nini...

Busara azikwe mapema yaishe..
Hata tukiombeleza mwezi mzima nothing will change ..
Kuna watu wanapiga hela za mwisho..ni upuuzi mtupu kuzurura na mfu ambae hata hawaoni mkimuaga
 
Wengine wanaenda kutazama huo umati
Wengine ni event tu..hawana cha huzuni wala nini...

Busara azikwe mapema yaishe..
Hata tukiombeleza mwezi mzima nothing will change ..
Ni kweli wamzike mapema masuala ya kuutembeza mwili huko na huko si busara...
Afu wanaomwombea kwa sasa ni kupteza muda tu sababu hukumu hutolewa immediately baada ya nafsi kuchukuliwa....kilichopo hapo ni cover tu!!
Cha msingi sisi tukiobaki tuna mengi sana ya kujifunza hasa kwenye suala zima la Haki na kuvumiliana.
 
Back
Top Bottom