Mzalendo_Mwandamizi
JF-Expert Member
- Dec 12, 2007
- 1,117
- 4,772
Kwamba kilichojiri Mwanza hakipendezi, ni suala la wazi kwa mtu yeyote anayetaka kuona Tanzania yenye amani na mshikamano.
Hata hivyo, matukio kama haya yanaibua tafakuri ambazo baadhi ya wenzetu wanaweza wasizipende.
Majuzi tulimsikia Mdude akimtahadharisha Mama Samia kuwa "wembe uliotumika kumnyolea Magufuli utatumika kwake (Mama Samia) pia." Hakukuwa na wembe as such bali alimaanisha kuwa endapo "Mama Samia akiwazingua Chadema nao watamzingua."
Well, kwa kilichojiri Mwanza, ni wazi "Mama kawazingua Chadema." Swali ni je, nao wana uwezo wa kumzingua?
Nimeona Mheshimiwa Lissu akiwataka Watanzania kuingia mtaani kutokana na kukamatwa kwa Mbowe na viongozi wenzake. Nadhani Mheshimiwa ameshasahau kuwa alipotoa wito kama huo kuwa watu waingie mtaani Novemba 2 mwaka jana baada ya "uchafuzi wa kihistoria," hata viongozi wenzie hawakujitokeza mtaani.
Lakini hata tukiacha tukio hilo, tangu 1995 hadi 2005, Mkapa aliwazingua Wapinzani lakini hakuna aliyemfanya chochote. Jk nae akarudia 2005 hadi 2015, na hakufanywa chochote, na majuzi Magufuli akafanya aliyotaka kufanya dhidi ya Wapinzani na hakupata resistance yoyote mpaka anaingia kaburini.
Kwahiyo, hata Mama Samia akiamua "kuiga mfano wa watangulizi wake" hakuna wa kumfanya chochote. Sad but true.
Majuzi walipokamatwa akina Lwaitama, ilisubiriwa "huruma ya serikali" kuwatoa rumande. Hakukuwa na jitihada zozote zaidi ya kelele za mtandaoni. Na leo inakatika, same story. "Oh Mama Samia ni dikteta," "Oh atakiona," same empty words.
Ukweli mchungu ni huu, endapo Mama Samia ataamua "kuwazingua wapinzani" hakuna wa kumzuwia. Ukweli huu mchungu unapaswa kuwa sehemu ya mikakati ya upinzani katika kupanga ajenda zao. Kwamba kujimwambafai mitandaoni ilhali likitokea la kutokea watu wanaufyata, ni mkakati fyongo. Kwa kifupi, confrontational politics haziwezi kuuwezesha upinzani kutimiza ajenda zake. Kunahitajika njia mbadala. Hiyo ni mada ya wakati mwingine.
Baadhi yetu tulionya, though, baada ya Mama Samia kutahadharisha kuhusu "chokochoko"