Uwapi "wembe wa Mdude uliotumika kumnyoa Mwendazake" ambao Samia Alitishiwa nao majuzi?

Shida kubw inayoikumba chadema kwa sasa ni mipango yao mibovu wameiga mavazi ya EFF wameshindwa kuiga mfumo wao .

Wao wameshika ajenda isiyokuwa na nguvu kwa Watanzania KATIBA .

Watafute ajenda zenye tija
Ajenda gani kwa sasa mkuu? Ajenda yao kubwa waliipoteza 2015 baada ya kumkumbatia Lowassa (Na ulifanyika uvunjifu mkubwa wa katiba yao kumpitisha Lowassa kugombea urais, leo hii nao wanadai katiba, wakati ya chama chao tu hawaiheshimu)
 
Shida kubw inayoikumba chadema kwa sasa ni mipango yao mibovu wameiga mavazi ya EFF wameshindwa kuiga mfumo wao .

Wao wameshika ajenda isiyokuwa na nguvu kwa Watanzania KATIBA .

Watafute ajenda zenye tija
Kama ajenda gani kwa mfano?!
 
Kwamba kilichojiri Mwanza hakipendezi, ni suala la wazi kwa mtu yeyote anayetaka kuona Tanzania yenye amani na mshikamano.

Hata hivyo, matukio kama haya yanaibua tafakuri ambazo baadhi ya wenzetu wanaweza wasizipende.

Majuzi tulimsikia Mdude akimtahadharisha Mama Samia kuwa "wembe uliotumika kumnyolea Magufuli utatumika kwake (Mama Samia) pia." Hakukuwa na wembe as such bali alimaanisha kuwa endapo "Mama Samia akiwazingua Chadema nao watamzingua."

Well, kwa kilichojiri Mwanza, ni wazi "Mama kawazingua Chadema." Swali ni je, nao wana uwezo wa kumzingua?

Nimeona Mheshimiwa Lissu akiwataka Watanzania kuingia mtaani kutokana na kukamatwa kwa Mbowe na viongozi wenzake. Nadhani Mheshimiwa ameshasahau kuwa alipotoa wito kama huo kuwa watu waingie mtaani Novemba 2 mwaka jana baada ya "uchafuzi wa kihistoria," hata viongozi wenzie hawakujitokeza mtaani.

Lakini hata tukiacha tukio hilo, tangu 1995 hadi 2005, Mkapa aliwazingua Wapinzani lakini hakuna aliyemfanya chochote. Jk nae akarudia 2005 hadi 2015, na hakufanywa chochote, na majuzi Magufuli akafanya aliyotaka kufanya dhidi ya Wapinzani na hakupata resistance yoyote mpaka anaingia kaburini.

Kwahiyo, hata Mama Samia akiamua "kuiga mfano wa watangulizi wake" hakuna wa kumfanya chochote. Sad but true.

Majuzi walipokamatwa akina Lwaitama, ilisubiriwa "huruma ya serikali" kuwatoa rumande. Hakukuwa na jitihada zozote zaidi ya kelele za mtandaoni. Na leo inakatika, same story. "Oh Mama Samia ni dikteta," "Oh atakiona," same empty words.

Ukweli mchungu ni huu, endapo Mama Samia ataamua "kuwazingua wapinzani" hakuna wa kumzuwia. Ukweli huu mchungu unapaswa kuwa sehemu ya mikakati ya upinzani katika kupanga ajenda zao. Kwamba kujimwambafai mitandaoni ilhali likitokea la kutokea watu wanaufyata, ni mkakati fyongo. Kwa kifupi, confrontational politics haziwezi kuuwezesha upinzani kutimiza ajenda zake. Kunahitajika njia mbadala. Hiyo ni mada ya wakati mwingine.

Baadhi yetu tulionya, though, baada ya Mama Samia kutahadharisha kuhusu "chokochoko"

Nimecheka kwa nguvu hiki ulichoandika, kweli nimeamini sasa ww umeshazeeka. Ngoja nikupe ukweli, cdm wameamua kutumia hiyo mbinu ya kulazimisha, inaweza isiwe na impact ya haraka hivyo, lakini itazaa matunda. ANC ya Afrika kusini ilipambana kwa mabavu zaidi ya nusu karne, na ilikuja kufanikiwa, itakuwa hiyo miaka 30 uliyoitaja ww? Tulitawaliwa na wakoloni zaidi ya miaka 70, na sio kwamba watu walikuwa hawapambani.

Kama kujinyenyekeza kunasaidia, basi ACT ya Zito walipaswa kufanikiwa. Kumefanyika chaguzi zaidi ya tano za marudio, mbona ACT wamejinyenyekeza na bado wanafanyiziwa? Hivi tunavyoongea, leo ACT wamemsusia sherehe za Iddy Mwiny huko Pemba, kisa uchaguzi wa wiki iliyopita huko konde wameporwa japo wako kwenye serikali ili kuponya madonda. Ni hivi, mtu hata kama hamuwezi pigana naye atakuheshimu. Kama kujinyenyekeza kunalipa, jinyenyekeze ww ili wakuonee huruma urudi nyumbani kumalizia uzee wako ukiwa hai.
 
Jitahidi evalist unaweza kupata nafasi ya kurudi mwaka huu. Mi nadhani hii approach ni nzuri ya kujishusha kwa watawala na wakitaka kukunyoa unaweka kichwa vizuri. Wanakunyoa... Inasaidia. Unaweza ruhusiwa kurudi tanzania.

Kwamba kilichojiri Mwanza hakipendezi, ni suala la wazi kwa mtu yeyote anayetaka kuona Tanzania yenye amani na mshikamano.

Hata hivyo, matukio kama haya yanaibua tafakuri ambazo baadhi ya wenzetu wanaweza wasizipende.

Majuzi tulimsikia Mdude akimtahadharisha Mama Samia kuwa "wembe uliotumika kumnyolea Magufuli utatumika kwake (Mama Samia) pia." Hakukuwa na wembe as such bali alimaanisha kuwa endapo "Mama Samia akiwazingua Chadema nao watamzingua."

Well, kwa kilichojiri Mwanza, ni wazi "Mama kawazingua Chadema." Swali ni je, nao wana uwezo wa kumzingua?

Nimeona Mheshimiwa Lissu akiwataka Watanzania kuingia mtaani kutokana na kukamatwa kwa Mbowe na viongozi wenzake. Nadhani Mheshimiwa ameshasahau kuwa alipotoa wito kama huo kuwa watu waingie mtaani Novemba 2 mwaka jana baada ya "uchafuzi wa kihistoria," hata viongozi wenzie hawakujitokeza mtaani.

Lakini hata tukiacha tukio hilo, tangu 1995 hadi 2005, Mkapa aliwazingua Wapinzani lakini hakuna aliyemfanya chochote. Jk nae akarudia 2005 hadi 2015, na hakufanywa chochote, na majuzi Magufuli akafanya aliyotaka kufanya dhidi ya Wapinzani na hakupata resistance yoyote mpaka anaingia kaburini.

Kwahiyo, hata Mama Samia akiamua "kuiga mfano wa watangulizi wake" hakuna wa kumfanya chochote. Sad but true.

Majuzi walipokamatwa akina Lwaitama, ilisubiriwa "huruma ya serikali" kuwatoa rumande. Hakukuwa na jitihada zozote zaidi ya kelele za mtandaoni. Na leo inakatika, same story. "Oh Mama Samia ni dikteta," "Oh atakiona," same empty words.

Ukweli mchungu ni huu, endapo Mama Samia ataamua "kuwazingua wapinzani" hakuna wa kumzuwia. Ukweli huu mchungu unapaswa kuwa sehemu ya mikakati ya upinzani katika kupanga ajenda zao. Kwamba kujimwambafai mitandaoni ilhali likitokea la kutokea watu wanaufyata, ni mkakati fyongo. Kwa kifupi, confrontational politics haziwezi kuuwezesha upinzani kutimiza ajenda zake. Kunahitajika njia mbadala. Hiyo ni mada ya wakati mwingine.

Baadhi yetu tulionya, though, baada ya Mama Samia kutahadharisha kuhusu "chokochoko"

Umesahau kuwa Mbowe hana kisomo ? Binafsi sikuwa najua Mbowe ni mjinga kiasi hiki. ,mama kahitahidi mno kuwapa polotical space ,wao wakamuu kufanya tofauti ,inatia kinyaaaa kwa kweli ,kwa wale amabao sia wachanga humu nawapeni jina la mtu mjinga kama mbowe ni huwa anaitwa TONDO ,wanajamvi kuanzia leo naombeni kabisa hili jina linamfaa Mbowe
Hilo Jina litakufaa wewe na aliyefanya makosa kukuleta duniani
 
Kwa ujinga huu ulioandika, wewe ni typical mtanzania.

We na mimi hatupaswi kuwashambulia kina Mbowe bali yatupasa kuhoji tumechukua hatua gani kuwaunga mkono.
Wewe ni mpumbavu unawaunga mkono wazee wa jinai hawa ,uko unampikia mmeo eti unawaunga mkono

USSR
 
Kijana aka "jasusi" fahamu hili Tanzania haijawahi kuwa na upinzani bali ni watu waliokosa fursa CCM na kisha kupata hasira na kuhama..
Ccm ndio sehemu yenye fursa sio?! Ndio maana hamtaki katiba mpya ili muendelee kuwanyonya Watanzania
 
Mbona wewe umekimbia Nchi na unarudi Nchini mwako kama mwizi?
 
Kwa ujinga huu ulioandika, wewe ni typical mtanzania.

We na mimi hatupaswi kuwashambulia kina Mbowe bali yatupasa kuhoji tumechukua hatua gani kuwaunga mkono.

Nchi za wenzetu ujinga kama huu haupo isipokuwa Bongo tu.

Sasa lipeni tozo za simu na muache kulalamika maana hakuna mnachoweza.

kwani lazima kuwaunga mkono? kama tumegundua harakati zao ni kwa maslahi yao binafsi kuna haja gani yakuendelea kuwashabikia...?
 
Mdude ana cheo gani ndani ya Chadema?
Hizi mada nyingine sijui mnafikiria nini

Niliwahi kusema, iwapo huyo mama ataonyesha yeye ni nani kisa maneno ya huyo Mdude, basi nitadhibitisha kuwa mama ni rais mwenye upeo mdogo kwelikweli. Nilitarajia kuona hatua dhidi ya watu waliojiunganishia bomba la mafuta, lakini unaona jeshi lote la polisi likifanya ubabe wa kijinga kisa rais hataki kuonekana dhaifu kwa maneno ya kina mdude. Kwahiyo rais anaonyesha uimara wake kwa maneno ya wahuni waliobambikiwa kesi.
 
kwani lazima kuwaunga mkono? kama tumegundua harakati zao ni kwa maslahi yao binafsi kuna haja gani yakuendelea kuwashabikia...?
Cdm hawahitaji ww au ndugu zako wawaunge mkono, bali wanataka haki ya kufanya kongamano, tena la ndani kupaza sauti ya madai yao halali. Hulazimishwa kuwaunga mkono kwa jambo usiloliamini.
 
Back
Top Bottom