Tetesi: Uwazi wa RC Makonda na StarTv siri hii hapa nje ndani

Tetesi: Uwazi wa RC Makonda na StarTv siri hii hapa nje ndani

Word.

Maarifa hayaishiii kwenye kufaulu mitihani ya darasani.

Bahati mbaya sana Wasomi wetu wa Kitanzania hudhani GPA za University ndiyo kuwa na uwezo mkubwa wa Kimaarifa wakati kumbe kiuhalisia siyo kweli. Kuna kupata bahati ya kusoma lakini ili uwe mzuri zaidi yakupasa pia uwe na IQ ya kutosha ambayo umezaliwa nayo na ndiyo maana katika hili huwa sifichi kulisema japo Mimi ni Mshabiki wa CCM kuwa japokuwa Elimu ya Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA Mheshimiwa Freeman Alkaeli Mbowe ni ndogo ila amebarikiwa sana na Mwenyezi Mungu kuwa na IQ nzuri tena pengine inayowashinda Viongozi wengine wengi wenye Degree, Masters na Doctorates zao. Kuna Viongozi wa CCM yangu huwa wakiongea halafu nikijua hata Viwango vyao vikubwa vya Elimu walivyonavyo huwa nazima Tv na hata kupandwa na hasira kwa aina ya upupu / upuuzi wanaousema ila nisiwe mnafiki huwa nikimsikia tu Mbowe anazungumza huwa navutiwa kumsikiliza na huwa namwelewa sana Baba wa Watu na nadhani busara, staha na hekima yake ingeigwa na Viongozi wengine pengine hizi takataka kero za Kiuongozi tunazoziona sasa zisingekuwepo abadan.
 
Gentamicin Intravenous Infusion [emoji382] for fast relief!

Hongera Mkuu kwa dose Mubashara,
Wenye macho wameona, wenye kuhitaji wamechukua na wasiohitaji nao ni chaguo lao

Akhasante sana Mkuu na kama kawaida yangu Kazi yangu Kuu ni kunyoosha tu bila unafiki, uwoga wala upendeleo wowote ule.
 
Bahati mbaya sana Wasomi wetu wa Kitanzania hudhani GPA za University ndiyo kuwa na uwezo mkubwa wa Kimaarifa wakati kumbe kiuhalisia siyo kweli. Kuna kupata bahati ya kusoma lakini ili uwe mzuri zaidi yakupasa pia uwe na IQ ya kutosha ambayo umezaliwa nayo na ndiyo maana katika hili huwa sifichi kulisema japo Mimi ni Mshabiki wa CCM kuwa japokuwa Elimu ya Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA Mheshimiwa Freeman Alkaeli Mbowe ni ndogo ila amebarikiwa sana na Mwenyezi Mungu kuwa na IQ nzuri tena pengine inayowashinda Viongozi wengine wengi wenye Degree, Masters na Doctorates zao. Kuna Viongozi wa CCM yangu huwa wakiongea halafu nikijua hata Viwango vyao vikubwa vya Elimu walivyonavyo huwa nazima Tv na hata kupandwa na hasira kwa aina ya upupu / upuuzi wanaousema ila nisiwe mnafiki huwa nikimsikia tu Mbowe anazungumza huwa navutiwa kumsikiliza na huwa namwelewa sana Baba wa Watu na nadhani busara, staha na hekima yake ingeigwa na Viongozi wengine pengine hizi takataka kero za Kiuongozi tunazoziona sasa zisingekuwepo abadan.
Kweli mkuu, nadhani kuna gap kati ya intellectual ability na uwezo wa kufaulu mitihani. Wengi wetu tuna uwezo wa kukariri na kufaulu mitihani ya darasani tu. Intellectuals wapo wachache sana.
 
Napata tabu sana kuuamini huu uzi moja kwa moja, sjui kwanini. Hayo mazungumzo ya siri kati ya Makonda na Dialo kayaskiaje ilihali kasema walikuwa wawili?. Duu hiyo inshu ya kupewa ukatibu sasa ndio kaniacha hoi, Ccm ni taasisi kubwa, hata kama ni Manyumbu ukatibu hauwezi kuuzwa kijinga hivyo, Tena na Makonda? Hapana nakataa, mleta Uzi mi nipo neutral ila nimeshindwa kuelewa na kuamini
 
Kweli mkuu, nadhani kuna gap kati ya intellectual ability na uwezo wa kufaulu mitihani. Wengi wetu tuna uwezo wa kukariri na kufaulu mitihani ya darasani tu. Intellectuals wapo wachache sana.

Umemaliza kila kitu Mkuu akhsante sana. Uko vizuri mno!
 
UWAZI WA MAKONDA STAR TV SIRI HII HAPA NJE NDANI!

Baada ya Paul Makonda hali yake kisiasa kuchafuka kutokana na matendo yake hivi karibuni alikuja Mwanza na kubaini kuwa kwa sasa amepoteza mvuto Kabisa kutokana na kukosa kiki kwenye vyombo vya habari na baadhi ya marafiki zake kuanza kumkimbia.


Inasemekana ujio wa Makonda Mwanza ilikuwa ni Kwa ajili ya kuweka mambo sawa na Mkurugenzi wa Star Tv ndugu Antony Dialo, ambaye walikutana Kwa siri na Mkurugenzi huyo.

Imebainika kuwa Makonda alikuja Kwa malengo matatu la kwanza ni kujaribu kuweka mambo sawa na Dialo ambaye pia ni mwenyekiti wa chama mkoa wa Mwanza ambaye anaunga mkono tamko la Jukwaa la wahariri kutokurusha habari za Makonda.

Imefahamika katika lengo la kwanza walimtisha mzee Dialo kama atashindwa kufanya kazi pamoja na Makonda watamuondoa mara moja ndani ya chama Kwa kumvua nyadhifa zote za uongozi.

Jambo la pili tulilodokezwa ni kwamba Hali ya uchumi ni mbaya katika kampuni ya Sahara iliyopelekea MD wake ndugu Sammy Nyala kuondoka kutokana kushuka sana kibiashara katika kampuni hiyo inayomilikiwa na Mzee Dialo siku hizi hawafanyi vizuri kibiashara na ukichangia na Deni la zaidi ya shilingi bilioni nne kutoka TRA.

Makonda alimuhaidi atamsaidia kuongea na mamlaka za juu kumpatia TAX HOLIDAY endapo atakubali kufanya naye kazi na kurusha taarifa zake Yeye Makonda.

Makonda katika safari ya Mwanza aliambatana na Ray pamoja JB ambaye hivi karibuni amemteua kuwa mhamasishaji wa wasanii katika kusambaza taarifa za Makonda mitandaoni.

Katika Siku ya Pili pale Malaika Resort Makonda alisikika akiongea kwenye simu na mtu ambaye alionekana kumtii sana ndani ya chama na kumpatia taarifa juu ya adhima ya Antony Dialo kuifikiria zaidi nafasi ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi.

Jioni walipokutana Katika hotel ya Malaika Resort Majira ya Jioni Gari ya mzee Dialo ilifika, Makonda na Dialo walizungumza tena Kwa kirefu na kupanga jinsi gani wataweza kufanya kazi pamoja mojawapo ni kujisafisha kuhusu uvamizi wa Clouds Media ili kuizima ishu ya Uvamizi mipango ipangwe haikuwa ishu ya Gwajima bali tetesi za uwepo wa Dawa za kulevya rejea tamko aliloliandika Mzee Dialo.

Pia wakati wanazungumza na Mzee Dialo, Makonda alimjulisha kuwa tayari mipango ya kumuandalia nafasi ya Ukatibu mkuu ndani ya chama CCM Taifa imekwishaiva hivyo asiwe na wasiwasi pale Mkutano Mkuu Taifa utakapoitishwa muda wowote kuanzia sasa kumjadili Nape Nnauye basi ndiyo utakuwa muda muafaka wa jambo lake kuingizwa kwenye ajenda ya Mkutano Mkuu.



Chanzo kilidokeza kuwa Makonda alimuhaidi kumpatia Dialo Kiasi cha fedha ambacho atachukua kutoka kwa Wafanyabiashara marafiki zake wa Dar kwa ajili ya kumsaidia kulipa madeni na Mishahara kwa wafanyakazi wake Kwa mwezi wa 3 hadi wa 6 kwani inasemeka wafanyakazi hao wengi wao bado hawajalipwa Mishahara yao isipokuwa posho ndogo zilizopo Kwa ajili ya kujikimu kwa kuwa hali ya Uchumi kwenye kampuni hiyo ni Mbaya sana.

Kingine Makonda amehaidi kumsaidia Anthony Dialo kwa kumpatia ulinzi kwa kipindi Chote watakachokuwa wanafanya kazi pamoja kumlinda na hasira kutoka Kwa waandishi wasio unga mkono harakati za Makonda.

Baada ya kumaliza Maongezi na na Makonda inasemekana Dialo aliwaita wafanyakazi wake na kujadiliana wajipange jinsi gani ya kufanya kazi na Makonda kitu ambacho Wafanyakazi wametafsiri kuwa ni ishara mbaya kwa kituo hicho cha habari hasa ikichangiwa na uhusiano mbovu na dharau alizozionyesha Makonda kipindi cha nyuma kwa wafanyakazi wa kituo hicho.

Unaambiwa Baada ya Antony Dialo kumaliza kile kikao aliwashinikiza wafanyakazi wake kuwa asiyetaka aondoke akatafute kazi sehemu nyingine Kwa kuwa tayari ajenda pekee alizobaki nazo kwa siri kichwani ni Ukatibu Mkuu wa chama na kusamehewa madeni anayodaiwa.

Kwa Taarifa zilizopo mzee Dialo alikwenda South Africa haijulikani alikwenda kufanya nini, nitaendelea kuwajuza kwa kadri iwezekanavyo juu ya ziara hiyo na kila kitu kitakuwa wazi.

Hii sasa ni kufuru kama Paul Makonda ataendelea kutumia ukaribu wake na Mamlaka za juu ili tu aendelee kujinufaisha Kwa maslahi yake binafsi.
Ni sawa ndugu lakini wewe ni nani na umeyatoa wapi haya maneno?ujiseme na utupe ushahidi wa uliyoyasema
 
Mmmmh,huyu Jamaa ana agenda gani hasa.,mbna anatumia nguvu kubwa kiasi hichi...,kwani hzo harakati zake zina manufaa gani ki ivo mpka kwa taifa mpka kufikia kutaka kufanya mpango Wa kulipia deni kubwa namna hiyo analodaiwa Dialo...!!!????
 
Hii habari naweza kuiamini kwa sababu nilimuona makonda kwa macho yangu pale malaika akiwa na kundi la malaya
 
Hata shetani anajua kushika kalamu!!!!
USI-CONFUSE MWANDIKO WA THE ALMIGHT JAH NA WA baali.
Povu la nini sasa, nina uhuru wa kuchangia hapa,ama lazima tufanane mitizamo nawewe?najua nawe kesho ni miongoni mwa mtakaotizama kipindi cha Makonda.

Mlisusa kuandika habari zake lakini now kila uzi unaomhusu mnafungua na kuchangia jamani mtakonda bure kwa chuki.
 
Tatizo la Serekali legelege iliyo jikimbikizia mafaraka kwa watu wache tu...... Mtu kama makonda kibongo bongo ni kama PM kwa sasa, agusiki..... Wakati RC ni kiongozi wa kawaida tu.
 
Na baada ya Kuoa sasa anatumia neno gani katika kuwasilisha hicho Kiungo korofi lakini kitamu kwa Mwanaume yoyote yule aliye rijali?
Alipitia changamoto flani sasa hivi amemrudia muumba hataki kabisa kuzungumzia hicho kiungo
 
Hahaha..wazee wa ngada wanatetemeka, mnachokiogopa ni nini hasa? nishaanda popcorn za kesho asubuhi, kwa nini hamtaki kuusikiliza ukweli lakini?
 
Hahaha..wazee wa ngada wanatetemeka, mnachokiogopa ni nini hasa? nishaanda popcorn za kesho asubuhi, kwa nini hamtaki kuusikiliza ukweli lakini?
Hawa wivu na chuki tu zinawasumbua hawana kingine yaani wamejaa povu kuliko clouds yenyewe.
 
Huyu Makonda anawahangaisha sana.
Sasa kama walikutana wawili kwa siri haya yote umeyapata wapi au ndio m'mbea mpe picha story ataandika mwenyewe..?
Mlisema hamtaangalia kipindi chake sasa haya yote ya nin..?
Huko huko Malaika mlisema Alivamia kipindi XXL wapo kwenye show mpaka watangazaji wakakesha ili tu wasidhurike leo mnasema alikuja mapema tu na kuonana na Dialo.
Mbona mnasahau mliloongea juzi kila siku mnakuja na jipya?
 
Hakuna kibaya hapa. Kila upande kwa maana ya Makonda na Diallo wanafaidika na hii mission.
Maslahi Kwanzaa, hutakiwi kua na Adui au Rafiki wa kudumu.

Wanastahili pongezi Sana
 
Acha atengeneze pesa, acheni majungu.
Anapofirisika huna msaada wowote kwake
 
  • Thanks
Reactions: nao
Back
Top Bottom