Tetesi: Uwazi wa RC Makonda na StarTv siri hii hapa nje ndani

Tetesi: Uwazi wa RC Makonda na StarTv siri hii hapa nje ndani

Sikumbuki mara ya mwisho kuitazama star tv ni lini, ila nikitumia majira ya vipindi kama masika, kianga na vuli, mara ya mwisho ni wakati ule wa kampeni waliooanza kumsema Lowasa vibaya basi ikawa mwisho, ila tbc ni kwa awamu yote ya nne.
 
UWAZI WA MAKONDA STAR TV SIRI HII HAPA NJE NDANI!

Baada ya Paul Makonda hali yake kisiasa kuchafuka kutokana na matendo yake hivi karibuni alikuja Mwanza na kubaini kuwa kwa sasa amepoteza mvuto Kabisa kutokana na kukosa kiki kwenye vyombo vya habari na baadhi ya marafiki zake kuanza kumkimbia.

Inasemekana ujio wa Makonda Mwanza ilikuwa ni Kwa ajili ya kuweka mambo sawa na Mkurugenzi wa Star Tv ndugu Antony Dialo, ambaye walikutana Kwa siri na Mkurugenzi huyo.

Imebainika kuwa Makonda alikuja Kwa malengo matatu la kwanza ni kujaribu kuweka mambo sawa na Dialo ambaye pia ni mwenyekiti wa chama mkoa wa Mwanza ambaye anaunga mkono tamko la Jukwaa la wahariri kutokurusha habari za Makonda.

Imefahamika katika lengo la kwanza walimtisha mzee Dialo kama atashindwa kufanya kazi pamoja na Makonda watamuondoa mara moja ndani ya chama Kwa kumvua nyadhifa zote za uongozi.

Jambo la pili tulilodokezwa ni kwamba Hali ya uchumi ni mbaya katika kampuni ya Sahara iliyopelekea MD wake ndugu Sammy Nyala kuondoka kutokana kushuka sana kibiashara katika kampuni hiyo inayomilikiwa na Mzee Dialo siku hizi hawafanyi vizuri kibiashara na ukichangia na Deni la zaidi ya shilingi bilioni nne kutoka TRA.

Makonda alimuhaidi atamsaidia kuongea na mamlaka za juu kumpatia TAX HOLIDAY endapo atakubali kufanya naye kazi na kurusha taarifa zake Yeye Makonda.

Makonda katika safari ya Mwanza aliambatana na Ray pamoja JB ambaye hivi karibuni amemteua kuwa mhamasishaji wa wasanii katika kusambaza taarifa za Makonda mitandaoni.

Katika Siku ya Pili pale Malaika Resort Makonda alisikika akiongea kwenye simu na mtu ambaye alionekana kumtii sana ndani ya chama na kumpatia taarifa juu ya adhima ya Antony Dialo kuifikiria zaidi nafasi ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi.

Jioni walipokutana Katika hotel ya Malaika Resort Majira ya Jioni Gari ya mzee Dialo ilifika, Makonda na Dialo walizungumza tena Kwa kirefu na kupanga jinsi gani wataweza kufanya kazi pamoja mojawapo ni kujisafisha kuhusu uvamizi wa Clouds Media ili kuizima ishu ya Uvamizi mipango ipangwe haikuwa ishu ya Gwajima bali tetesi za uwepo wa Dawa za kulevya rejea tamko aliloliandika Mzee Dialo.

Pia wakati wanazungumza na Mzee Dialo, Makonda alimjulisha kuwa tayari mipango ya kumuandalia nafasi ya Ukatibu mkuu ndani ya chama CCM Taifa imekwishaiva hivyo asiwe na wasiwasi pale Mkutano Mkuu Taifa utakapoitishwa muda wowote kuanzia sasa kumjadili Nape Nnauye basi ndiyo utakuwa muda muafaka wa jambo lake kuingizwa kwenye ajenda ya Mkutano Mkuu.

Chanzo kilidokeza kuwa Makonda alimuhaidi kumpatia Dialo Kiasi cha fedha ambacho atachukua kutoka kwa Wafanyabiashara marafiki zake wa Dar kwa ajili ya kumsaidia kulipa madeni na Mishahara kwa wafanyakazi wake Kwa mwezi wa 3 hadi wa 6 kwani inasemeka wafanyakazi hao wengi wao bado hawajalipwa Mishahara yao isipokuwa posho ndogo zilizopo Kwa ajili ya kujikimu kwa kuwa hali ya Uchumi kwenye kampuni hiyo ni Mbaya sana.

Kingine Makonda amehaidi kumsaidia Anthony Dialo kwa kumpatia ulinzi kwa kipindi Chote watakachokuwa wanafanya kazi pamoja kumlinda na hasira kutoka Kwa waandishi wasio unga mkono harakati za Makonda.

Baada ya kumaliza Maongezi na na Makonda inasemekana Dialo aliwaita wafanyakazi wake na kujadiliana wajipange jinsi gani ya kufanya kazi na Makonda kitu ambacho Wafanyakazi wametafsiri kuwa ni ishara mbaya kwa kituo hicho cha habari hasa ikichangiwa na uhusiano mbovu na dharau alizozionyesha Makonda kipindi cha nyuma kwa wafanyakazi wa kituo hicho.

Unaambiwa Baada ya Antony Dialo kumaliza kile kikao aliwashinikiza wafanyakazi wake kuwa asiyetaka aondoke akatafute kazi sehemu nyingine Kwa kuwa tayari ajenda pekee alizobaki nazo kwa siri kichwani ni Ukatibu Mkuu wa chama na kusamehewa madeni anayodaiwa.

Kwa Taarifa zilizopo mzee Dialo alikwenda South Africa haijulikani alikwenda kufanya nini, nitaendelea kuwajuza kwa kadri iwezekanavyo juu ya ziara hiyo na kila kitu kitakuwa wazi.

Hii sasa ni kufuru kama Paul Makonda ataendelea kutumia ukaribu wake na Mamlaka za juu ili tu aendelee kujinufaisha Kwa maslahi yake binafsi.
Umbea wa kiwango hiki ukitolewa na mwanaume ni hatari sana!umbea ni sifa za wanawake!ukitolewa na mwanaume kuna mengi ya kujiuliza![emoji15]
 
Dialo angejikaza kiume kama Meck Sadick asingeyumbishwa
 
Umbea wa kiwango hiki ukitolewa na mwanaume ni hatari sana!umbea ni sifa za wanawake!ukitolewa na mwanaume kuna mengi ya kujiuliza![emoji15]
toa facts ...sasa una ushahidi gani kwamba huyo ni mmbea....utu uzima akili sio ujinga ndugu
 
Halafu mada za kuelimisha kama hizi tukichangia ili kuanika upuuzi wa bashite wanakuja mods kwa spidi kukupiga ban ili kulitetea hili dude linalohangaisha taifa zima kwa siri kubwa iliyojificha kati yake na anayelibeba.
Mods hasa Maxence Melo wafunze umod hao uliowapa vyeo vya umod wajue kazi yao si kupiga ban ovyo bali kurekebisha kilichokosewa na kutoa tahadhali kwa muhusika na asipozigatia ndipo apigwe ban.
Mimi wakinipa ban kwenye ukweli siogopi hata kisu kiwe shingini
Matako kampa Mungu akiyatumia kwa ujinga wake ndio asumbue taifa na aliyepewa na lubuvu
Kifo
Kifo
Kifo
Kifo
Kifo
Cha kuongea ukweli ni peponi
 
Halafu akina jb na wapuuzi wenzake wanakuja kujiuliza kwanini soko la filamu zao limeshuka. Wakati majibu wanayo. Mtapata mlo wa siku moja kuambatana na uyo bwana lkn mjue mnaharibia wenzenu wengi ktk tathinia yenu kwa ajir ya njaa yenu tu mnayoiponesha kwa muda mfupi tu.
 
Go, go, go, go Makonda kama umeandikiwa yes binadamu ni nani? acha waongee, watunge uongo wawezao hadi midomo ipinde.
 
Nikupongeze na "like" nitakugongea.
Habari zozote watakazotangaza hawa sahara "midia" kumhusu bashite TUTAZIPUUZA.
 
Kuna siku nilireply kama ulivyoreply nikapigwa ban ya wiki mbili. Hawa mod wanalitetea sana hili dubwasha sijui limewapa nini na wao?
Duuuuu

Mkuuuuuu umenifanya nihisi barid hadi kwenye mifupa. I cant imagine kupigwa ban two weeks consecutively.
 
Mtabaki na majungu hivyohivyo

mwenzenu ndio ashatoka hivyo

Ni Mtu tu Mpumbavu wa aina yako na asiye na exposure yoyote yale anaweza akawa na blanketed remarks kama hizi zako halafu hapo ulipo unajiita Great Thinker. Hivi hapa duniani kuna Watu waliokuwa Matajiri, Wafujaji, Watesaji na Wanyanyasaji wa Raia kama walivyokuwa Watoto wa aliyekuwa Rais wa Zaire ( leo DRC ) akina Jose Kongolo Mobutu na Dada yake Ngawali Mobutu?

Huyu Kongolo alikuwa hana tofauti na Makonda wetu lakini hakuna Mtu ambaye alikufa Kifo kibaya sana nchini Congo DR kama yeye huku akiwa kawaachia Warembo kibao wa DRC ugonjwa wake wa UKIMWI / SIDA na kwani karibia Wanawake wengi wa Kongo alikuwa akiwaingilia kwa nguvu ( kuwabaka ) na wapo pia ambao alikuwa akifanya nao ngono akimaliza anawapiga risasi na kuwauwa huku wengine akiwaamrisha wale askari waliokuwa wakimtii sana Baba yake wawachukue wale wanawake na kwenda kuwatupa Mto Congo ili waliwe na Mamba.

Ilifika kipindi huyo Mtoto Kipenzi wa Hayati Mobutu ( Jose Kongolo ) alipewa Madaraka makubwa na Baba yake hadi akawa anaiba Mali za Wakongo huku akimteulia Baba yake Mawaziri na Viongozi wa nafasi nyeti hasa za Usalama wa Taifa na za Ukuu wa Majeshi lakini pia huyu Mtoto Jose Kongolo alikuwa pia hata akichukua jukumu la Kuwaua Viongozi wa ngazi za juu wa Congo DR ( zamani Zaire ) ambao ama aliwaona au aliwahisi kwenda kinyume na Baba yake.

Cha kushangaza sasa kama siyo kusikitisha pamoja na jeuri yote ya kuwa Watoto wa Rais Tajiri Africa wakati huo huku wakiwa na kila kitu huwezi amini macho na masikio yako kwani Mtoto Mkubwa wa Kike wa Hayati Mobutu Seseko aitwae Ngawali au jina la Utani Mama Mibeko sasa ni Bar Maid katika Baa moja kubwa tu pale jijini Paris mji Mkuu wa Ufaransa kiasi kwamba hata Wakongo au Waafrika wengine wanaomjua huwa wakienda Paris hupita hapo kumwangalia na wengi wao hutokwa na machozi ya huruma kwa jinsi alivyochoka na kupigika sana Kimaisha.

Ninachotaka tu kukuambia na kukufundisha hapa ni kwamba katika maisha haya ya sasa hakuna kitu kizuri na cha baraka kama kuishi vizuri na Watu, kuwa na kiasi na kutenda haki na mema kwa Watu wote kwani huyu Makonda wenu akiendekeza hizi tabia zake atakuwa anapita mule mule ambapo alipita Jose Kongolo Mobutu na kujikuta hata siku akitutangulia mbele ya haki anazikwa na Watu saba tu hadi tisa kama ambao walimzika Jose kisha baadae Wakongo wakawa wanaenda pale Kaburini wanakojoa na hadi wengine Kunya pale juu huku wakilivunja vunja Kaburi lake na kumlaani.

Tujifunze na yaliyokwisha tokea na kamwe tuache kujifanya sisi ni Vichwa ngumu na Paul Makonda ajue kuwa Maisha ni kama Matokeo ya mpira ambapo leo unaweza ukawa unashinda sana lakini kuna wakati nawe utakuwa unafungwa mno na kuambulia sare nyingi na hata kupelekea kushuka daraja na kupotea kabisa Kimafanikio.

Kila la kheri.
 
Go, go, go, go Makonda kama umeandikiwa yes binadamu ni nani? acha waongee, watunge uongo wawezao hadi midomo ipinde.
Hata shetani anajua kushika kalamu!!!!
USI-CONFUSE MWANDIKO WA THE ALMIGHT JAH NA WA baali.
 
Duuuuu

Mkuuuuuu umenifanya nihisi barid hadi kwenye mifupa. I cant imagine kupigwa ban two weeks consecutively.
Mkuu hapo ndo ujue bashite ana nguvu za ajabu sana kuanzia Ikulu mpaka jf na sijui anawapaga nini hadi wanamgwaya kiasi hiki? Ndiyo, nilikula ban ya wiki mbili kavu kwa kosa la kumkemea huyo mjinga wa taifa anayebebwa kwa udi na uvumba hata akivamia kwako inabidi eti unyamaze. Subiri siku atavamia ofisi za jf akiwa na LMG ndipo wataacha kulitetea.
 
Hivi clouds nao si walikua karibu sana na RC makonda lkn badae eti ikafikia hpo dah ss dialo nae aangalie yasije yakafikia huku
 
Ni Mtu tu Mpumbavu wa aina yako na asiye na exposure yoyote yale anaweza akawa na blanketed remarks kama hizi zako halafu hapo ulipo unajiita Great Thinker. Hivi hapa duniani kuna Watu waliokuwa Matajiri, Wafujaji, Watesaji na Wanyanyasaji wa Raia kama walivyokuwa Watoto wa aliyekuwa Rais wa Zaire ( leo DRC ) akina Jose Kongolo Mobutu na Dada yake Ngawali Mobutu?

Huyu Kongolo alikuwa hana tofauti na Makonda wetu lakini hakuna Mtu ambaye alikufa Kifo kibaya sana nchini Congo DR kama yeye huku akiwa kawaachia Warembo kibao wa DRC ugonjwa wake wa UKIMWI / SIDA na kwani karibia Wanawake wengi wa Kongo alikuwa akiwaingilia kwa nguvu ( kuwabaka ) na wapo pia ambao alikuwa akifanya nao ngono akimaliza anawapiga risasi na kuwauwa huku wengine akiwaamrisha wale askari waliokuwa wakimtii sana Baba yake wawachukue wale wanawake na kwenda kuwatupa Mto Congo ili waliwe na Mamba.

Ilifika kipindi huyo Mtoto Kipenzi wa Hayati Mobutu ( Jose Kongolo ) alipewa Madaraka makubwa na Baba yake hadi akawa anaiba Mali za Wakongo huku akimteulia Baba yake Mawaziri na Viongozi wa nafasi nyeti hasa za Usalama wa Taifa na za Ukuu wa Majeshi lakini pia huyu Mtoto Jose Kongolo alikuwa pia hata akichukua jukumu la Kuwaua Viongozi wa ngazi za juu wa Congo DR ( zamani Zaire ) ambao ama aliwaona au aliwahisi kwenda kinyume na Baba yake.

Cha kushangaza sasa kama siyo kusikitisha pamoja na jeuri yote ya kuwa Watoto wa Rais Tajiri Africa wakati huo huku wakiwa na kila kitu huwezi amini macho na masikio yako kwani Mtoto Mkubwa wa Kike wa Hayati Mobutu Seseko aitwae Ngawali au jina la Utani Mama Mibeko sasa ni Bar Maid katika Baa moja kubwa tu pale jijini Paris mji Mkuu wa Ufaransa kiasi kwamba hata Wakongo au Waafrika wengine wanaomjua huwa wakienda Paris hupita hapo kumwangalia na wengi wao hutokwa na machozi ya huruma kwa jinsi alivyochoka na kupigika sana Kimaisha.

Ninachotaka tu kukuambia na kukufundisha hapa ni kwamba katika maisha haya ya sasa hakuna kitu kizuri na cha baraka kama kuishi vizuri na Watu, kuwa na kiasi na kutenda haki na mema kwa Watu wote kwani huyu Makonda wenu akiendekeza hizi tabia zake atakuwa anapita mule mule ambapo alipita Jose Kongolo Mobutu na kujikuta hata siku akitutangulia mbele ya haki anazikwa na Watu saba tu hadi tisa kama ambao walimzika Jose kisha baadae Wakongo wakawa wanaenda pale Kaburini wanakojoa na hadi wengine Kunya pale juu huku wakilivunja vunja Kaburi lake na kumlaani.

Tujifunze na yaliyokwisha tokea na kamwe tuache kujifanya sisi ni Vichwa ngumu na Paul Makonda ajue kuwa Maisha ni kama Matokeo ya mpira ambapo leo unaweza ukawa unashinda sana lakini kuna wakati nawe utakuwa unafungwa mno na kuambulia sare nyingi na hata kupelekea kushuka daraja na kupotea kabisa Kimafanikio.

Kila la kheri.
Mkuu naona umeamua kutema nyongo yote,
mwenye kuelewa na aelewe.
 
Halafu mada za kuelimisha kama hizi tukichangia ili kuanika upuuzi wa bashite wanakuja mods kwa spidi kukupiga ban ili kulitetea hili dude linalohangaisha taifa zima kwa siri kubwa iliyojificha kati yake na anayelibeba.
Mods hasa Maxence Melo wafunze umod hao uliowapa vyeo vya umod wajue kazi yao si kupiga ban ovyo bali kurekebisha kilichokosewa na kutoa tahadhali kwa muhusika na asipozigatia ndipo apigwe ban.
Haswaaaaa
 
Back
Top Bottom