Uwe maarufu au la, usijifanye una hela wakati huna! Utakuja umbuka msibani

Leo narudi kwa Babu yangu Kariakoo Mtaa wa Kariakoo kufungua juzuu na kupata mawaidha kuhusu husda.

Naomba msikilizeni Sheikh akitoa mawaidha dhidi ya husda, na mjiondoe kwenye kufanya dhambi ya husda mpaka misibani.

To be sure, mimi sina dini lakini mafunzo mazuri yaliyomo katika dini nayapenda.

Karibuni.

Kiranga wewe unaijua hali yenu ya kule Singida

Umesikiliza mawaidha dhidi ya husda?

Singida wapi huko? Mimi si mtu wa Singida naona unanifananisha na mtu mwingine.

Kwetu walishajenga wazee, wamejenga vizuri kuanzia nyumba mpaka makaburi.

Kuna makaburi mazuri mpaka ukiyaona unatamani kufa uzikwe.

Ndiyo maana mara nyingine sitaki kutembelea sana.
 
Mniache nifanye yangu,hela ni zangu hamjui nilipopata.
Kwa kweli mwanamme kufuatilia mwanamme mwenzako hela zake anazitumia vipi ndiyo mwanzo wa kuolewa.

Na kumfuatilia mwanamke ndiyo kabisaa aibu.

Mambo ya Ngoswe, muachie Ngoswe mwenyewe.

Nina swali moja kwa hao wenye viherehere vya kufuatilia matumizi ya pesa za watu.

Mnafuatilia watu wanavyotumia pesa zao kwani nyie maofisa wa TRA?
 
Kama umefanikiwa na husaidii kwenu we Ni mzigo
Mambo ya familia ni mengi na mazito.

Si haki kum judge mtu bila kujua kwa undani.

Hilo la kwanza.

La pili, mzigo ni mtu mzima ambaye hajaondoka kwa baba yake. Aliye na negative impact. Mtu mzima aliyeondoka kwa baba yake si mzigo. Unaweza kusema hasaidii kwao, lakini si mzigo.

Mtu kutosaidia kwao si sawa na kuwa mzigo. Haya ni mambo mawili tofauti.

Mzigo ni mtu mwenye negative impact kwa familia. Mtu mzima anayelishwa na baba yake ni mzigo. That is negative impact.

Mtu mzima anayemlisha baba yake, huyo ni mchangiaji kwenye hiyo familia. That is positive.

Mtu aliyejitenga na familia yake kwa sababu ambazo sisi hatuzijui, halishwi na baba yake wala hamlishi baba yake, huyo si mzigo - hana negative impact- wala si mchangiaji kwa baba yake - hana positive impact.

Wazazi wanatakiwa kujipangia maisha ya uzeeni, wasiwafanye watoto wao kuwa ni vitegauchumi vya maisha yao ya baadaye. Ukipanga hivyo halafu mtoto akafariki kabla ya mzazi utafanyaje?

Na nyie Watanzania baki msiowajua watu na familia zao kwa undani, na maisha familia hizi ilimopitia, msiwe na viherehere vya kutaka kukariri mambo na kupangia maisha watu ambao hata hamuwajui na hamjui habari za ndani za familia.

Mnaweza kulaumu mtu hajampa msaada baba yake, kumbe kuna ugomvi wa familia baba kapewa msaada kakataa.

Na hata mtu akiamua kutomsaidia baba yake mwenyewe. Ni sawa. Ni haki yake. Hela zake. Hujamsaidia kutafuta.

Sasa kwa nini unataka kumpangia mtu matumizi ya hela zake?

Akikupangia wewe matumizi ya hela zako anavyotaka yeye kinyume na unavyotaka wewe utafurahi?
 
Watoto huficha aibu ya nyumbani kwao
 
Back
Top Bottom