mama kubwa
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 6,230
- 9,889
Mambo ya familia ni changamoto hasa kwenye Mali. Nilikarabati nyumba ya familia na wazazi kuhamia kwangu nilipojenga. Nyumba ina wapangaji na hela inaingia Kwa ajili ya kuendesha familia. Cha ajabu ikitakiwa ukarabati naangaliwa Mimi. Ni ngumu jamani sababu Ile ni Mali ya familia sio ya MTU mmoja na mara nyingi wale ndugu wajanja wajanja wasiochangia kitu huwa Wana Fujo Sana wazazi wakitangulia.Ndio maana watu wanajitenga na Mali za familia.