Uwe maarufu au la, usijifanye una hela wakati huna! Utakuja umbuka msibani

Uwe maarufu au la, usijifanye una hela wakati huna! Utakuja umbuka msibani

Mambo ya familia ni mengi na mazito.

Si haki kum judge mtu bila kujua kwa undani.

Hilo la kwanza.

La pili, mzigo ni mtu mzima ambaye hajaondoka kwa baba yake. Aliye na negative impact. Mtu mzima aliyeondoka kwa baba yake si mzigo. Unaweza kusema hasaidii kwao, lakini si mzigo.

Mtu kutosaidia kwao si sawa na kuwa mzigo. Haya ni mambo mawili tofauti.

Mzigo ni mtu mwenye negative impact kwa familia. Mtu mzima anayelishwa na baba yake ni mzigo. That is negative impact.

Mtu mzima anayemlisha baba yake, huyo ni mchangiaji kwenye hiyo familia. That is positive.

Mtu aliyejitenga na familia yake kwa sababu ambazo sisi hatuzijui, halishwi na baba yake wala hamlishi baba yake, huyo si mzigo - hana negative impact- wala si mchangiaji kwa baba yake - hana positive impact.

Wazazi wanatakiwa kujipangia maisha ya uzeeni, wasiwafanye watoto wao kuwa ni vitegauchumi vya maisha yao ya baadaye. Ukipanga hivyo halafu mtoto akafariki kabla ya mzazi utafanyaje?

Na nyie Watanzania baki msiowajua watu na familia zao kwa undani, na maisha familia hizi ilimopitia, msiwe na viherehere vya kutaka kukariri mambo na kupangia maisha watu ambao hata hamuwajui na hamjui habari za ndani za familia.

Mnaweza kulaumu mtu hajampa msaada baba yake, kumbe kuna ugomvi wa familia baba kapewa msaada kakataa.

Na hata mtu akiamua kutomsaidia baba yake mwenyewe. Ni sawa. Ni haki yake. Hela zake. Hujamsaidia kutafuta.

Sasa kwa nini unataka kumpangia mtu matumizi ya hela zake?

Akikupangia wewe matumizi ya hela zako anavyotaka yeye kinyume na unavyotaka wewe utafurahi?
[emoji817][emoji3581]
 
Unajirusha mitandaoni maisha bora, kubadilisha magari makali, unaishi apartment kali, Bata kwa Sana! Kumbe sirini maisha feki, mke elimu Hana Zaid ya kuuza sura. Siku ya msiba mnaumbuka Mbele ya makamera!
***Msibani watu wanalia kwa mengi (aibu/fedheha mixer huzuni).
Uzuri ni kwamba ushakufa hata wakikuimba huumii wala kudhalilika
 
Inasikitisha lakini mambo yao waachie wenyewe...
 
Picha zako unapigia sehemu ya nyumba kali na masofa ya bei, ukitamba ni nyumbani, msiba ukija unatamani ardhi ipasuke! Acheni hizo!! Ni uuuuungwana?
 
Wakati tupo chuo kuna binti fulani rafiki yangu alikuwa anawafanyia dharau sana watu, siku akafiwa na mama yake wanadarasa walipoenda msibani walimsema sana maisha ya kwao yalikuwa duni wakati yeye alijidai maisha mazuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakati tupo chuo kuna binti fulani rafiki yangu alikuwa anawafanyia dharau sana watu, siku akafiwa na mama yake wanadarasa walipoenda msibani walimsema sana maisha ya kwao yalikuwa duni wakati yeye alijidai maisha mazuri

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapa jirani imetokea hivo hivo kama uliyoandika hivo unakuta mtu ana madharau kufika msibani kwao hamna kitu
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Tutafute pesa, tupendezeshe kwetu (zikiwemo nyumba za ibada wanapoabudu wazazi nyumbani). Wenzetu wachaga wanachangia hata wakiwa huku mijini. Sisi toka Singida sijui tunakwama wapi?
**Haifurahisi unaendesha Gari Kali (Range Rover, VW, Ford au BMW) halafu home picha za kuibia, unavizia palipopambwa tu!
 
Back
Top Bottom