Uwe maarufu au la, usijifanye una hela wakati huna! Utakuja umbuka msibani



Kuna kisa cha mshikaji yuko ughaibuni. Kakaake kakopa benki kupitia nyumba ya familia. Hela zote katumbua, benki ikabidi wanataka kuchukua nyumba. Jamaa akachukua savings zake zote ikabidi anunue ile nyumba. Ndugu kuona msala wa benki umeisha wakamgeukia. Wengine wakaangusha vilio kwamba unatunyasasa kwa vile we unakaa Ulaya. Mshikaji ikabidi arudi ughaibuni mikono mitupu. Huku nyuma ndugu zake nyumba wakaipiga bei tena hela wakagawana.
Yaani mbele ya mali ndugu wengine hawana hata huruma
 
Hii inawahusu wote wenye maisha ya kuigiza igiza.Unajiujua unavyo fake life.Kwenu kijijini unajua wazazi wako wanapolala,halafu wewe unajifanya huku unaishi kwenye apartment.

watu mnasubiri mpaka mpigiwe simu na wazazi wenu ili muwasaidie

Kila mtu apambane na maisha yake, kama wao wanaishi maisha magumu ndo waliyoyachagua

Sasa nisiendeshe gar zuri kisa familia yangu maskin mxieew, nisiishi sehem nzuri kisa kwetu pabaya

Tofautisha kwetu na kwangu, vitu viwil tofaut hata magufuli kwake na kwao ni tofauti
 
Tumefikia hukoo
 
Acha unafiki wewe shekhe.

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Kuna moja Kali Baba alimwambia binti yake ambae hakuwa na mume ajenge Ka apartment kwenye kiwanja chake Mzee, dada akajidunduliza akajenga akaanza kuishi na wanae ndugu Zake 7 wanaona na wanajua kinachoendelea. Mipango ya MUNGU wazazi wakatangulia. In short walikaa kikao wakaamua nyumba zote mbili ni za familia Kodi zikitoka zinagawanywa mara 8 idadi ya watoto WA Mzee. Na kama dada anataka kuishi pale alipe Kodi. Dada Yule akaondoka na mgao kazira hachukui hata elfu.
 
Hakuna kuumbuka kwenye umaskini. Kama ww ni maskini ni maskini hata kama ni maarufu, uchungu wa umaskini utaupata tu bila kujali watu wanajua ww ni maskini au la.
 
Kuna Maisha Ya Insta,FB,Tiktok na Youtube Channel.

Ni maamuzi yako na akili zako uweje.
 
Hii inawahusu wote wenye maisha ya kuigiza igiza.Unajiujua unavyo fake life.Kwenu kijijini unajua wazazi wako wanapolala,halafu wewe unajifanya huku unaishi kwenye apartment.

watu mnasubiri mpaka mpigiwe simu na wazazi wenu ili muwasaidie
Hivi hapo anajifanya anaishi kwenye apartment au kiukweli anaishi kwenye apartment?
 
๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†Fisi kala fisi mwenzake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ