Uwekezaji huu wa Diamond Platnumz, kamwe hatafulia kama wengi wanavyodhani

Uwekezaji huu wa Diamond Platnumz, kamwe hatafulia kama wengi wanavyodhani

Benki ana Bilioni 5.

Lakini awe muangalifu.Walifulia akina Whitney Houston na MICHAEL Jackson sembuse Diamond wa Mbagala.

Hayati Notorioua B.I.G alishawahi kuimba ;"More Money More Problemz".
Hao unaowasema kufulia kwao ni kwa kujitakia maana walijitumbukiza kwenye dimbwi la matumizi ya madawa ya kulevya, lazma wapoteze muelekeo.
 
Kwanza kuwa na heshima kwa Mr Nice. Huwezi kuweka andiko bila wa kumtolea mfano? Kama Mr Nice angewekeza, pengine huyo unae muona asingejua lolote kuhusu kuwekeza. Pili hivyo vitu vyote unavyo vitaja hatujaona evidance yoyote kama ni vyake., weka evidance hata hati ya mahuziano basi ili tukuamini, msitufanye watoto zenu kila mkijamba tuvumilie.
Team kiba wazee wamajungu katika ubora wake
 
Ujue namimi natamani siku moja niwe upande wa wanaopenda Mtanzania mwenzao mchapakazi afulie.... Maana sijui inakuaje yani au unajisikiaje... Isije ikawa wanaenjoy peke yao.
 
Nasib Abdul ni mfano mzuri sana kwa vijana tujifunze kwake
 
Nyumba ya South Africa iko kwa jina lake?
uwekezaji wa brand ya hawara sio guaranteed..
siku mkimwagana hupati hata senti....hawara sio mke
Diamond sio mjinga kiasi hicho. Hivi ulimsikia hata ile kuwa Video Queen wa Utanipenda jamaa alimlipa pesa like anyone else ingawaje Zari mwenyewe alitaka kufanya for free! Unadhani kwanini alifanya hivyo? It's a message kwamba "this's my job and not our job!" Asije kesho na kesho kutwa akadai hata kazi walikuwa wanashirikiana!! Hata kama sijaona hati but am certain nyumba itakuwa na jina la Tiffa! Hawezi kuwa bwege aandike jina la Zari!!
 
Ungekuwa shabiki namba moja wa chama chetu CCM ndiyo nigeona kuna ukweli kwani CCM itaendelea kutawala siku zote na haitakuja kufirisika kamwe maana ni tajiri wa viongozi na uongozi. Ila kwa huyu kijana mwenzetu hali inaweza kubadilika, kumbuka kama akina Jackson etc waliishiwa sembuse yeye. Kumbuka pia umaarufu + uwekezaji==Ghararama hupanda, na ikitokea mirija imekata basi kila kitu huporomoka. Kikubwa kijana anatakiwa awe na watalaamu wa uchumi na mahesabu ili wamsharui vizuri asiwekeze tu ili mradi kaambiwa na mganga wa kienyeji.

Unaitwa nani?
 
Nikihesabu umri wangu na bwana mdogo naaweza kumlinganisha na first born wangu japokua kamzidi miaka mitatu hakika anastahili pongezi
 
Back
Top Bottom