Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,067
- 10,938
Wakuu habari,
Mimi ni shabiki mnazi wa Diamond Platnumz kwa muda mrefu.
Nimekuwa nikosoma sehemu mitandao mbalimbali hata humu JF watu wakisema kuwa Diamond siku zake zinahesabika kushuka kimuziki na mkwanja. Wanadai hajui kuimba na nyimbo zake ni Big G. Kuhusu nidhamu ya pesa wanadai ana matumizi makubwa sana halafu ana msururu wa wategemezi usiopungua 50.
Pamoja na hayo kijana ameonesha kupiga hatua kubwa sana kuzidi wasanii wote nchini. Ndani ya muda mfupi usiozidi miaka minne kijana ameweza kujiwekea vitega uchumi ambavyo mpaka anakufa vitakuwa vinamuingizia kipato.
- Ana mikataba kibao na makampuni
- Zari, Tiffah, Mama Mond wote ni brand wana mikataba
- Anamiliki nyumba za kutosha
- Anamiliki studio ya Muziki
- Anamiliki studio ya kupiga picha
- Soon kujiunga na lebo kubwa ya muziki inayomilikiwa na msanii mkubwa Marekani
- Ana wasanii (Wasafi) wanaoingiza pesa nzuri tu
- Ana mke/hawara mwenye akili
- Ana mashabiki lukuki
- Anapata show za kutosha na msanii anayelipwa pesa nyingi
- Vitega uchumi vingine ambavyo sivijui
Diamond sasa kila wimbo anaogusa ni moto huko youtube na ameweza kuvunja rekodi hadi alizoweka mwenyewe. Mfano...
- Salome unafanya vizuri duniani
- Zigo remix, huu bado ni moto na gumzo dunia (Una views za kutosha Youtube), Nani anajua AY katoa wimbo mpya unaitwa EL Chapo? Wachache sana maana Mond hajatia maguu.
- Waache waoane , Chege hakuwahi kufikisha views hata 700k youtube lakini uwepo wa Mond,Chege kavunja rekodi ndani ya wiki.
- Make me Sing, A.K.A alisherekea kuvunja rekodi SA ndani ya wiki, hakuwahi kabla
- Sweet Love, Akothee kila siku anamshukuru Diamond kumvunjisha rekodi na kupelekea kujulikana Afrika
- Watora Mari, Jah Prayzah kaporomosha bonge la party kwa mara ya kwanza kufikisha views 1m tokea aanze kuimba.
- Bado, nani asoujua huu wimbo. Uwepo wa Diamond ulisababisha kuwa wimbo wa taifa na Harmo kuvunja rekodi ya views etc etc
Kijana pia ana moyo wa kurudisha kwa jamii wahitaji.Katoa madawati kwa wanafunzi, katoa 20m kwa GSM wengine wakajikweza kuongeza 1m ili wamzidi.
Ndani ya wiki mbili kanunua nyumba mbili, Tabata na SA
Kijana kama huyu sio wa kumbeza, anajua anachokifanya.
Poleni kwa kuwachosha.